Gordian Anduru
JF-Expert Member
- Apr 16, 2021
- 369
- 747
Dunia inamfahamu kama Dalai Lama wa 14 kiongozi mkuu wa nchi iitwayo Tibet lakini pia Kiongozi huyu ni kiongozi mashuhuri zaidi wa imani ya kibuddha kama ilivyo Baba Mtakatifu (Papa) kwa wakristo au Ayatollah Khomeini kwa waislamu. Dalai Lama pia ni mtaalam wa maswala ya electronics
Hata hivyo cha ajabu alipewa madaraka hayo mwaka 1938 akiwa na umri wa miaka mitatu tu(3).
Ilikuwaje?
Mwaka 1937 Akiwa na umri wa miaka miwili kuna wageni watatu walifika nyumbani kwao na kuomba hifadhi Tenzin alimfuata mmoja wa wageni wale na kuvuta kitu cha mfano wa rozari akasema ” ya kwangu hii” Mgeni Yule alishtushwa akamuuliza unajua mimi ni nani?
Mtoto Yule akajibu “wewe ni Lobsang Tsewang wa hekaluni “
Kumbe wale hawakuwa wageni wa kawaida, walikuwa ni Watawa kutoka hekaluni, kumbe kwa miaka miwili watawa hawa wamekuwa wakizunguka maeneo mbali mbali vijijini Tibet kumtafuta mtoto huyu waliyempata leo Katika imani ya kibuddha mtu akifa huzaliwa tena nitafafanua zaidi hapo chini dhana hii kwa hiyo wageni hawa waliamini kabisa kwamba mwenzao Thubten aliyefariki mwaka 1933 ndiye huyu amezaliwa kama Tenzin yuko mbele yao kama mtoto wa miaka miwili
Thubten alikuwa Dalai Lama wa kumi na tatu (13) na hapa walikuwa wamempata dalai lama wa kumi na nne (14)
Kikawaida Dalai lama akishagundulika hupelekwa hekaluni na kupewa heshima zote akiwa na umri huo huo. Pia analetwa waalimu mbali mbali kutoka katika kila fani ambayo itamwezesha kuwa kiongozi mkuu wa nchi ya Tibet. Hapa ndipo Dalai lama alikojifunza electronics hata kuwa na uelewa mkubwa kwenye masuala ya kiuongozi hata kuweza kutunukiwa nishani ya nobeli ya amani mwaka 1989
Sisi wabuddha tunaamini kwa dhati kabisa kwamba huyu dalai lama mnayemuona ndiye Yule Yule Gendun Drupa, Dalai Lama wa kwanza aliyezaliwa mwaka 1391 na kufa mwaka 1474. Amekuwa akizaliwa na kurudi mara 14!
Kuzaliwa tena (Reincarnation)
Katika imani ya kibuddha binadamu anapofariki kuna mambo matatu yanaweza kutokea
Jambo la kwanza
Mtu huyu kama siyo mtakatifu vya kutosha, yaani kama bado anayapenda sana mambo ya ulimwengu huu basi mtu huyo atazaliwa tena duniani. Utakapofika wakati wa roho kuachana na mwili roho ya mtu huyu itaingia kwenye mwili wa kiumbe ambacho kitazaliwa. Hivyo asilimia kubwa sana ya sisi binadamu tumekuwa tukizalliwa na kufa na kuzaliwa tena na tena na tena kutokana na tamaa zetu za mwili na kuupenda sana ulimwengu huu.
Jambo la pili
Kama mtu amefikia hatua ya juu ya kujitambua kwa lugha nyingine tunasema amepata ‘enlightment’ basi mtu huyo ataitwa Buddha maana yake “enlightened one” na ikitokea mtu huyo akafariki basi roho yake haitarudi duniani, hatozaliwa tena, roho yake itaingia “Nivarna”
Nivarna ni nini?
Nivarna haina tafsiri ya moja kwa moja lakini tunaweza kusema kwamba roho yako inakwenda kuchanganyika na ile roho kuu kama ambavyo uchukue maji ya kwenye kikombe ukayatie kwenye bahari yachanganyike yawe kitu kimoja
Jambo la tatu
Mtu anaweza kuwa amefikia hatua ya juu ya kujitambua kiasi kwamba akatakiwa asizaliwe tena duniani lakini kutokana na huruma aliyonayo kwa viumbe wengine anaamua kwa makusudi kuzaliwa tena duniani kwa ajili ya kuwasaidia watu mtu wa hivyo anaitwa Bodhisatva.
Hivyo Dalai Lama anaangukia kwenye kundi hili la tatu, ni mtu safi anakufa akitakiwa kwenda nivarna lakini kwa makusudi amekuwa akirudi kuwasaidia watu wake wa tibet
Glen Hoddle
Timu ya taifa ya uingereza iliwahi kuwa na kocha aitwae Glenn Hoddle ambaye alikuwa ni muumini wa imani ya kibuddha. Siku moja tarehe 30 januari 1999 alitoa maoni katika mahojiano na vyombo vya habari akasema “ Nyinyi wachezaji mna bahati mmezaliwa na viungo timamu na akili za wastani lakini kuna wenzenu wengine kwa sababu ya madhambi ya yao ya maisha yaliyopita wamezaliwa na ulemavu wa aina mbali mbali”
Watu walilalamikia maoni hayo ya kocha huyo na kusababisha chama cha soka cha uingereza kumsimamisha kazi kocha huyo kwa sababu ya kuwabagua walemavu lakini kimsingi sisi wabuddha huwa tunaamini kwamba unapozaliwa unabeba yale mmatendo ya maisha yako yaliyopita kama ulikuwa mtu mwovu basi unaweza kuzaliwa kama mtu fukara au mlemavu hata hivyo haupaswi kumcheka kilema kwa vile hata wewe hujui pengine lisaa limoja lijalo unaweza kugongwa na gari ukapata ulemavu kwa sababu ya madhambi gani uliyafanya katika maisha yako yaliyopita
Ni misconception tu lakini kimsingi wabuddha huwaonea huruma sana walemavu na kuwasaidia
Kwenye Biblia
Kuna andiko Fulani kwenye biblia linaashiria imani ya kuzaliwa tena pale watu wanapomshangaa
Mara tatu Bwana Yesu aaliwaambia wanafunzi wake kuwa yohana mbatizaji ni Elia
Marko 9:13
Mathayo 11:13-14)
Mathayo 17:12-13)