Dalai Lama kiongozi wa Tibet aliyekufa na kurudi mara 14

Dalai Lama kiongozi wa Tibet aliyekufa na kurudi mara 14

Gordian Anduru

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2021
Posts
369
Reaction score
747
28e7420d1e8d35e2.jpg

Dunia inamfahamu kama Dalai Lama wa 14 kiongozi mkuu wa nchi iitwayo Tibet lakini pia Kiongozi huyu ni kiongozi mashuhuri zaidi wa imani ya kibuddha kama ilivyo Baba Mtakatifu (Papa) kwa wakristo au Ayatollah Khomeini kwa waislamu. Dalai Lama pia ni mtaalam wa maswala ya electronics

Hata hivyo cha ajabu alipewa madaraka hayo mwaka 1938 akiwa na umri wa miaka mitatu tu(3).

Ilikuwaje?
Mwaka 1937 Akiwa na umri wa miaka miwili kuna wageni watatu walifika nyumbani kwao na kuomba hifadhi Tenzin alimfuata mmoja wa wageni wale na kuvuta kitu cha mfano wa rozari akasema ” ya kwangu hii” Mgeni Yule alishtushwa akamuuliza unajua mimi ni nani?

Mtoto Yule akajibu “wewe ni Lobsang Tsewang wa hekaluni “

Kumbe wale hawakuwa wageni wa kawaida, walikuwa ni Watawa kutoka hekaluni, kumbe kwa miaka miwili watawa hawa wamekuwa wakizunguka maeneo mbali mbali vijijini Tibet kumtafuta mtoto huyu waliyempata leo Katika imani ya kibuddha mtu akifa huzaliwa tena nitafafanua zaidi hapo chini dhana hii kwa hiyo wageni hawa waliamini kabisa kwamba mwenzao Thubten aliyefariki mwaka 1933 ndiye huyu amezaliwa kama Tenzin yuko mbele yao kama mtoto wa miaka miwili

Thubten alikuwa Dalai Lama wa kumi na tatu (13) na hapa walikuwa wamempata dalai lama wa kumi na nne (14)

Kikawaida Dalai lama akishagundulika hupelekwa hekaluni na kupewa heshima zote akiwa na umri huo huo. Pia analetwa waalimu mbali mbali kutoka katika kila fani ambayo itamwezesha kuwa kiongozi mkuu wa nchi ya Tibet. Hapa ndipo Dalai lama alikojifunza electronics hata kuwa na uelewa mkubwa kwenye masuala ya kiuongozi hata kuweza kutunukiwa nishani ya nobeli ya amani mwaka 1989

Sisi wabuddha tunaamini kwa dhati kabisa kwamba huyu dalai lama mnayemuona ndiye Yule Yule Gendun Drupa, Dalai Lama wa kwanza aliyezaliwa mwaka 1391 na kufa mwaka 1474. Amekuwa akizaliwa na kurudi mara 14!

Kuzaliwa tena (Reincarnation)
Katika imani ya kibuddha binadamu anapofariki kuna mambo matatu yanaweza kutokea

Jambo la kwanza
Mtu huyu kama siyo mtakatifu vya kutosha, yaani kama bado anayapenda sana mambo ya ulimwengu huu basi mtu huyo atazaliwa tena duniani. Utakapofika wakati wa roho kuachana na mwili roho ya mtu huyu itaingia kwenye mwili wa kiumbe ambacho kitazaliwa. Hivyo asilimia kubwa sana ya sisi binadamu tumekuwa tukizalliwa na kufa na kuzaliwa tena na tena na tena kutokana na tamaa zetu za mwili na kuupenda sana ulimwengu huu.

Jambo la pili
Kama mtu amefikia hatua ya juu ya kujitambua kwa lugha nyingine tunasema amepata ‘enlightment’ basi mtu huyo ataitwa Buddha maana yake “enlightened one” na ikitokea mtu huyo akafariki basi roho yake haitarudi duniani, hatozaliwa tena, roho yake itaingia “Nivarna”

Nivarna ni nini?
Nivarna haina tafsiri ya moja kwa moja lakini tunaweza kusema kwamba roho yako inakwenda kuchanganyika na ile roho kuu kama ambavyo uchukue maji ya kwenye kikombe ukayatie kwenye bahari yachanganyike yawe kitu kimoja

Jambo la tatu
Mtu anaweza kuwa amefikia hatua ya juu ya kujitambua kiasi kwamba akatakiwa asizaliwe tena duniani lakini kutokana na huruma aliyonayo kwa viumbe wengine anaamua kwa makusudi kuzaliwa tena duniani kwa ajili ya kuwasaidia watu mtu wa hivyo anaitwa Bodhisatva.
Hivyo Dalai Lama anaangukia kwenye kundi hili la tatu, ni mtu safi anakufa akitakiwa kwenda nivarna lakini kwa makusudi amekuwa akirudi kuwasaidia watu wake wa tibet

Glen Hoddle

Glenn_Hoddle_2014_(cropped).jpg


Timu ya taifa ya uingereza iliwahi kuwa na kocha aitwae Glenn Hoddle ambaye alikuwa ni muumini wa imani ya kibuddha. Siku moja tarehe 30 januari 1999 alitoa maoni katika mahojiano na vyombo vya habari akasema “ Nyinyi wachezaji mna bahati mmezaliwa na viungo timamu na akili za wastani lakini kuna wenzenu wengine kwa sababu ya madhambi ya yao ya maisha yaliyopita wamezaliwa na ulemavu wa aina mbali mbali”
Watu walilalamikia maoni hayo ya kocha huyo na kusababisha chama cha soka cha uingereza kumsimamisha kazi kocha huyo kwa sababu ya kuwabagua walemavu lakini kimsingi sisi wabuddha huwa tunaamini kwamba unapozaliwa unabeba yale mmatendo ya maisha yako yaliyopita kama ulikuwa mtu mwovu basi unaweza kuzaliwa kama mtu fukara au mlemavu hata hivyo haupaswi kumcheka kilema kwa vile hata wewe hujui pengine lisaa limoja lijalo unaweza kugongwa na gari ukapata ulemavu kwa sababu ya madhambi gani uliyafanya katika maisha yako yaliyopita

Ni misconception tu lakini kimsingi wabuddha huwaonea huruma sana walemavu na kuwasaidia

Kwenye Biblia
Kuna andiko Fulani kwenye biblia linaashiria imani ya kuzaliwa tena pale watu wanapomshangaa

Mara tatu Bwana Yesu aaliwaambia wanafunzi wake kuwa yohana mbatizaji ni Elia

Marko 9:13

Mathayo 11:13-14)
Mathayo 17:12-13)
 
Sasa ndugu zetu sababu ya kwanza na ya tatu zinafanana kwa msingi wake..sababu ya pili kuungana na roho kuu hapo mnalimbia tu kusema Mungu...walau nimeelewq kwa kiasi kuhusu ubudda
 
sasa huyu dalai lama kwa mujibu wa aina yako ya watu wanaozaliwa upya yeye anakua na sifa zipi???

maana aina ya kwanza,pili na tatu wote sifa zinafanana na si dalai lama kati yao.

kuna kitu nakihisi mwilini mwangu.
 
Sasa mbona watu wanaongezeka duniani? Kama ndivyo basi idadi ya watu isingeongezeka.
Dini kweli ni mzigo wa misumari
 
sasa huyu dalai lama kwa mujibu wa aina yako ya watu wanaozaliwa upya yeye anakua na sifa zipi???

maana aina ya kwanza,pili na tatu wote sifa zinafanana na si dalai lama kati yao.

kuna kitu nakihisi mwilini mwangu.
sifa ya tatu, anakuwa amejitambua lakini makusudi anarudi kuwaokoa wa tibet wenzake
 
Sasa mbona watu wanaongezeka duniani? Kama ndivyo basi idadi ya watu isingeongezeka.
Dini kweli ni mzigo wa misumari
Unapozaliwa upya siyo lazima uzaliwe kama binadamu, unaweza kuzaliwa kama kiumbe kingine, kuna watu wana roho za kinyama kiasi kwamba hawawezi kuzaliwa kama binadamu vivyo hivyo viumbe wengine kama samaki huweza kuzaliwa kama binaadamu na tayari kuna ushahidi wa viumbe vya majini kupungua huenda hilo likajibu swali lako
 
hizi dini hizi
we acha tu, kuna dini pia zinadai kuwa binadamu aliumbwa kwa udongo, yesu alipaa against gravity, mtume muhammad alipaa pia kwa kutumia farasi maalum aitwae burak against gravity, musa aligawanya maji yakasimama kama kuta mbili watu wakapita kati kati yake
 
Sasa ndugu zetu sababu ya kwanza na ya tatu zinafanana kwa msingi wake..sababu ya pili kuungana na roho kuu hapo mnalimbia tu kusema Mungu...walau nimeelewq kwa kiasi kuhusu ubudda
chifu nenoMungu labda limekuja na Yesu miaka 2000 iliyopita au muhamad mwaka 622AD lakini vitu nilivyoandika hapo vilisemwa na Siddarta Gautama BUDDHA miaka 2500 iliyopita yaani Buddha alizaliwa miaka 500 kabla ya Yesu mzee
 
chifu nenoMungu labda limekuja na Yesu miaka 2000 iliyopita au muhamad mwaka 622AD lakini vitu nilivyoandika hapo vilisemwa na Siddarta Gautama BUDDHA miaka 2500 iliyopita yaani Buddha alizaliwa miaka 500 kabla ya Yesu mzee
Sasa ikiwa Dalai Lama wa kwanza alizaliwa 1391 akaja kufariki 1474 hapo ni around miaka 83 sasa tukisema tuzidishe mara 14 x 83 = tunapata maika 1,162 yani hao madalai lama wameishi kwa miaka 1,162 sasa huoni kwamba Yesu aliezidi hio miaka 2000 bila ni kaka mkubwa wa akina Dalai Lama bila kumsahau Mohammad?...halafu hapo juu nimezungumzia Mungu siku sema Yesu...
 
Mimi Sio Budhist ila naamni katika Reincarantion.Naamini katika incarnation katika mtazamo huu:

  1. Kwanza kabisa dunia/ulimwengu ni mkubwa sana kiasi kwamba hautakaa ujae yaani ulimwengu ni infinite.
  2. Pili mwili ni kiungo katika Roho/au ni zana katika roho kama vilivyo viumbe vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vyote kiungo/zana kwa ajili ya matumiz fulani.(Ndio maana unakula chakula kinakuwa recycled then unakuja kukila tena.
  3. Hii tabia ya mzunguko,Recycle ni tabia ya Nature (Roho ikiwa ndio main component ta Nature})
  4. Mtu anapozaliwa mara ya pili huwa kuna nama mbili ama arudi kama multiple versions zake yaani mtu zaidi ya mmoja au arudi kama single version yake yaani kama alivoondoka arudi hivo hivo.
  5. Mara zote mtu anaporudi anakuwa the best version yake kwani ulimwengu wote unaeleke katika ukamilifu uliotulia(Perfect harmony)Kwa hio kila toleo jipya linakuwa bora kuliko la zamani.
  6. Kwa mfano mtu akiwa muovu sana,ila akapata nafasi ya kutubia uovu wake kwa imani yoyote ila basi atakporudi mara ya pili takuwa sio muovu kama yulie atakufa bila kutubia uovu wake ingawa atakuwa na wema fulani
  7. Unapozaliwa mara yapili unakuja a ubora wote uliokuwa nao hapa awali.Kwa mfano kama ulikuwatu Daktari(Clinical officer lakini ulikuwa na hamu ya kuwa Full MD au kuwa Specialist basi katia toleo jipya utakuwa na hamu ya kufikia huko na unaweza kufikia huko
Sasa nini cha kufanya ili uweze kuwa na control katia huu mzunguko wa incaranation?Kwanza unatakiwa daima utafute kuwa the best version yako.Jifunze vitu vingi kadiri uwezavyo,Tenda wema kwa watu wengi kadiri uwezavyo,Furahia maisha yako na kuyatahamini kadiri uwezavyo.Jizuie sana kutenda mamabo ambayo yanaondoa furaha za wengine na kuwatia huzuni.Epuka sana kuwa mchoyo wa maarifa kwa wengine na jitahidi sana kuwa na ndote kubwa na hamu ya kufanya maisha ya mwanadamu yawe bora zaidi.

Kadiri unavokuwa hivo ndio uwezekano wa wewe kuzaliwa katia version bora ya maisha yako inaongezeka na kadiri unapozembea kujiboresha ndo uwezekano waw wewe kubaki katika level za chini chini unaongezeka.

Ukiweza kusimamia mduara wako wa incarnation unawez akuchagua uzaliwe wapi na katika mazingira gani wewe mwenyewe ili kufikia kiwango lazima kwanza ukubaliane na kifo na uachane na maisha haya in good terms huku ukitarajia maisha mapya kwa hamasa.

Naendelea kusisitiza kwamba mimi sio Budhist ila Pamoja na IMANI YANGU ya KIKRISTO imani yangu personal imejengwa katika Msingi huo.

BE BETTER,BE HAPPY
 
Sasa ikiwa Dalai Lama wa kwanza alizaliwa 1391 akaja kufariki 1474 hapo ni around miaka 83 sasa tukisema tuzidishe mara 14 x 83 = tunapata maika 1,162 yani hao madalai lama wameishi kwa miaka 1,162 sasa huoni kwamba Yesu aliezidi hio miaka 2000 bila ni kaka mkubwa wa akina Dalai Lama bila kumsahau Mohammad?...halafu hapo juu nimezungumzia Mungu siku sema Yesu...
looh hujaelewa kabisa tunapomzungumzia Dalai Lama tunazungumzia dhehebu moja tu la tibetan Buddhist lakini ubuddha kama ubudha ulianza zamani kabla ya dalai lama miaka 2500 iliyopita
 
we acha tu, kuna dini pia zinadai kuwa binadamu aliumbwa kwa udongo, yesu alipaa against gravity, mtume muhammad alipaa pia kwa kutumia farasi maalum aitwae burak against gravity, musa aligawanya maji yakasimama kama kuta mbili watu wakapita kati kati yake
tatizo la dini ukishazisoma ukazielewa ndo unatatizika zaidi maana maswali hua mengi kuliko majibu.
 
Back
Top Bottom