Dalili moja ya mtu mshamba ni kujua kuongea 'kilugha'

Umeongea vyema lakini hata bongo kutupa kifungashio barabarani ni uchafu wala si jambo la kusema ni kawaida. Sasa basi hizo dalili zote ulizotaja za kukosa ustaarabu ni rahisi sana kuzikuta kwa mtu anayejua kilugha. Ndiyo maana nasema, kujua kilugha ni dalili moja kubwa sana ya ushamba.
 
Kuna Mzee anaitwa Ngugi Wa Thiong'o, mwandishi wa vitabu kama 'petals of blood na 'Wizard of the crow'. Hembu Google hilo jina uone ushamba wake.
Anaanza kuandika vitabu vyake kwa lugha ya asili ya Kikuyu, ila vinaishia kwenye lugha mbalimbali za kimataifa kama hivyo nilivyokutajia, na vinauzwa karibu ulimwenguni kote.
 
Navyopenda kuongea kilugha😂😂😂hata kwenye kamchezo ketu kalee nikinoga nakimwaga,, hapana raha naipata km kuongea lugha yangu mama,
 
Wewe ndio mshamba. Kiswahili, kiingereza, kireno., kijerumani etc "vilugha" vya wazaliwa wa maeneo hayo. Lugha unayodhani ni ya maana ni kilugha cha watu wengine. Hacha uzuzu.
 
Wewe ndio mshamba. Kiswahili, kiingereza, kireno., kijerumani etc "vilugha" vya wazaliwa wa maeneo hayo. Lugha unayodhani ni ya maana ni kilugha cha watu wengine. Hacha uzuzu.
Kama unajua kilugha uwezekano wa kuwa mshamba ni mkubwa sana.
 
Ushamba ni kuiga lugha za watu, mtu anajikunja na Kifaransa mpaka anashika pua ili atamke vizuri. Chukuwa neno la Kifaransa Tomb, inamaanisha kuanguka, sasa congugate wanavyosema uone utakavyohangaika. Mtu mstaarani ni yule anaetumia lugha yake ya asili anapokutana na watu wa asili yake. Mzungu mstaarani ni yule anaetumia kiswahili akiwa hapa Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…