Tudefine ushamba kama hali ya mtu kutojua utamaduni wa mjini au wa kisasa unataka nini. Mtu mshamba ni kazi sana kuendana naye au kuelewana naye.
Ni kazi sana kuishi na mtu mshamba au kufanya naye makubaliano. Hata ukioa au kuolewa na mshamba utapata taabu sana humo ndani. Ni vema kuwatambua na kuwaepuka.
Sasa basi, kuna dalili nyingi za kumtambua mtu mshamba, lakini kwa Tz dalili moja ya wazi ni mtu kujua kuongea kilugha. Ukiona mtu anaongea kilugha, taa ya hatari iwake kichwani mwako. Si wote wanaoongea kilugha ni washamba, lakini hilo ni moja ya dalili kuu za mtu mshamba.
Mkuu, fahamu hata kiswahili ni kilugha fulani hivi.
kwa mantiki yako nawe ni mshamba unayepaliilia bustani ya ujinga.
Kwa taarifa yako ushamba ni mazoea yanayofanywa na mtu yeyote kwenye mazingira yasiyokubalika kufanywa hivyo na wakazi wa eneo husika!
Kwa mfano, ukienda nchi za ulaya, hata uwe umezaliwa kariakoo, ukakulia postai Dar es salaam, lakini ukinunua kitu ukatupa kifungashio barabarani, mbali ya kwamba ni uchafu kwao, ila tena ni ushamba, wakati kwa wabongo ni kawaida tu.
Hili neno ushamba ni pana mno!
Kinyume chake ni neno USTAARABU!
Sijui kama unafahamu kwamba
kugombana.
Kuiba.
kukata foleni kwenye huduma fulani.
Kugombania daladala.
Kufungua mziki kwa sauti kubwa
Misifa ya kijinga.
Kujidai ni mtoto wa mjini.
Na ushamba mwingine kibao kwa aina zake, wote ni huohuo mmoja.
Lakini lugha kwa yenyewe haiwezi kunasibishwa na ushamba.
Samahani lakini.