Dalili za kuonesha tayari una ugonjwa wa Figo: Wanywa Pombe Kali Mnasalimiwa!

Dalili za kuonesha tayari una ugonjwa wa Figo: Wanywa Pombe Kali Mnasalimiwa!

Kila siku natamani kumwambia profesa atulie kidogo aangalie afya yake.
Ashazoea kamera, nini sasa kwenda kukodi na kuandaa hafla kubwa namna ile michango yenyewe imetolewa na na akina Lissu, Mbowe, Lema na Juma Nature na Lady Jay Dee.

CCM hawawezi changia mtu mpinzani hata kama yupo at deathpoint.
 
Haya mambo yasikieni tu, kwa kifupi hili tatizo likiingia katika familia basi ni iwe utakufa haraka kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu ambazo ni ghali sana, au kama mna mali mtaishia kuuza zote mtaishia kufilisika na hazitoshi kutibu tatizo , vinginevyo atokee msamaria mwema wa ku donate figo inaweza kuwa nafuu
 
Father mdogo alitumia sana hayo madude akiwa kweny kitengo serikalini, anajiona mjanja alipofika umri kama miaka 55 ~56 balaa likaaza ....Kaumwa miaka 4 mpaka alistaafu akiwa kitandani .

Alianza kuvimba miguu mwishoe ikaacha ikawa midogo kama mikono...Mara avimbe shavu moja akaanza kulalama haoni vizuri huku kaka zake wanakaribia miaka 70 ila wapo fresh...Kateseka sana miaka kama 8 mpaka amefariki.
 
Starehe isiyo na majjuto kiafya, kiakili, kimwili na kiroho ni kumwabudu Mungu Muumba mbingu na nchi katika roho (imani) na kweli (vitendo).

Pombe majanga = Huharibu figo, ini, kisukari, mtikisiko kiuchumi..

Sigara majanga = Huharibu mapafu, kansa, pumzi ndogo kimazoezi.

Bangi = Maamuzi yasiyo na akili.

Uzinzi + Uasherati + Kunyaduana = Magonjwa ya zinaa, UKIMWI, UTI, tezi dume, mikosi, mtikisiko kiuchumi. Watoto wengi wa mitaani sababu ya mimba zisizotarajiwa na mivunjiko ya mahusiano/talaka za ndoa, visasi na mauaji sababu ya wivu uliopitiliza na usaliti.

"Dunia ni uwanja wa fujo, Dunia hadaa walimwengu shujaa"
inafikieisha sana.
Sasa inasemekana kwenye pombe ndio kuna connection.
Wanywa juisi utawakuta KFC na vijimighahawa wapo na watoto, hakuna mazungumzo zaidi ya kupiga picha tu.
 
Profesa Janabi kwenye uzinduzi wa Professor Jay Foundation ametaja dalili za mtu ambaye tayari anaugonjwa wa figo. "Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo

Katika kutaja dalili hizo, salamu hizo amelekeza kwa wale Wazee wa bapa, k-vant, Nyagi na wote wanaopiga vileo vikali ili kukomesha mademu na mengine kama hayo.
Prof J hata kwenye interview yake alisema kwa siku alikuwa anachoma sindano za laki 8,

Dalili za ugonjwa wa Figo

1. Kuchokachoka ambako hakuelezeki.
2. Kulala siku inakuwa shida.
3. Hamu ya kula inapungua bila kujielewa.
4. Huwezi kufikiria sawa.
5. Mwili unaanza kuwasha.
6. Miguu inaanza kuvimba.
7. Ukiamka asubuhi jiangalie kwenye kioo uso wako utakuwa wa mduara na kadiri siku zitakavyokwenda inapotea.
8. Taste ya chakula inaanza kupotea
9. Kupumua hata rafiki zako wanaanza kugundua harufu yako ya kupumua inakuwa si nzuri sana.
10. Tumbo kuuma
11. Usiku kutoka mara kwa mara kwenda haja ndogo
12. Haja ndogo kuanza kuwa na povu
13. Unaanza kuona chembechembe za damu kwenye mkojo" - P Jb
Kama ni hivyo mbona serikali haijapigwa marufuku mvinywaji vikali kama ilivyopata marufuku bangi nk ?
 
Starehe isiyo na majjuto kiafya, kiakili, kimwili na kiroho ni kumwabudu Mungu Muumba mbingu na nchi katika roho (imani) na kweli (vitendo).

Pombe majanga = Huharibu figo, ini, kisukari, mtikisiko kiuchumi..

Sigara majanga = Huharibu mapafu, kansa, pumzi ndogo kimazoezi.

Bangi = Maamuzi yasiyo na akili.

Uzinzi + Uasherati + Kunyaduana = Magonjwa ya zinaa, UKIMWI, UTI, tezi dume, mikosi, mtikisiko kiuchumi. Watoto wengi wa mitaani sababu ya mimba zisizotarajiwa na mivunjiko ya mahusiano/talaka za ndoa, visasi na mauaji sababu ya wivu uliopitiliza na usaliti.

"Dunia ni uwanja wa fujo, Dunia hadaa walimwengu shujaa"
Nakubaliana nawe kwenye mengineyo mkuu ila ndumu inanipa focus hasa ninapokuwa nawasiliana na Mungu wangu.Pia vyote ulivyotaja vimekatazwa kwenye Biblia ila ndumu wamekataza sirikali.
 
Back
Top Bottom