Dalili za kuonesha tayari una ugonjwa wa Figo: Wanywa Pombe Kali Mnasalimiwa!

Dalili za kuonesha tayari una ugonjwa wa Figo: Wanywa Pombe Kali Mnasalimiwa!

Lengo lako mleta mada ni kututisha sisi wanywa pombe au una ajenda ya siri? Kwani ugonjwa wa figo unawapata wanywa pombe peke yao?
Usitutishe.
 
Ebo, kwani serikali ipige marufuku hizo 'spirit" wakati imejenga mahospitali ya kulaza wagonjwa wanaotokana na figo kufeli?
Hospitali inapata fedha nyingi za kununua magari na safari za nje za kikazi za viongozi kwa wagonjwa wanaolipa mamilioni
Acha tunywe tu hakuna atakayeishi milele
 
Kwahiyo tusinywe k_vant?
Piga kama kawaida, ila pia ukumbuke kuandika WOSIA mkeo asije porwa mali zote na wadogo zako.
Pia, uandike pahala pa kuzikwa ili kwenye kikao cha mazishi pale Mwika Bar ndugu zako wasivutane sana.
Lakini pia, unaweza kuacha maagizo kama mtu hajawahi kukuletea maua kipindi upo mzima asikuletee maua ya bei ghali ukiwa mfu maana hata hutaweza kumshukuru,.
 
Profesa Janabi kwenye uzinduzi wa Professor Jay Foundation ametaja dalili za mtu ambaye tayari anaugonjwa wa figo. "Ukiwa na hizi dalili sio za mwanzo tena, tayari wewe umeingia kwenye ugonjwa wa Figo

Katika kutaja dalili hizo, salamu hizo amelekeza kwa wale Wazee wa bapa, k-vant, Nyagi na wote wanaopiga vileo vikali ili kukomesha mademu na mengine kama hayo.
Prof J hata kwenye interview yake alisema kwa siku alikuwa anachoma sindano za laki 8,

Dalili za ugonjwa wa Figo

1. Kuchokachoka ambako hakuelezeki.
2. Kulala siku inakuwa shida.
3. Hamu ya kula inapungua bila kujielewa.
4. Huwezi kufikiria sawa.
5. Mwili unaanza kuwasha.
6. Miguu inaanza kuvimba.
7. Ukiamka asubuhi jiangalie kwenye kioo uso wako utakuwa wa mduara na kadiri siku zitakavyokwenda inapotea.
8. Taste ya chakula inaanza kupotea
9. Kupumua hata rafiki zako wanaanza kugundua harufu yako ya kupumua inakuwa si nzuri sana.
10. Tumbo kuuma
11. Usiku kutoka mara kwa mara kwenda haja ndogo
12. Haja ndogo kuanza kuwa na povu
13. Unaanza kuona chembechembe za damu kwenye mkojo" - P Jb
Hivi janab ni Prof wa nini hasa maana naona amekuwa akizungumzia karibia kila kitu kuanzia mambo ya maisha, magonjwa ya moyo, mambo ya misosi n.k. maana nakumbuka ni mtaalamu dokta ndodi pekee ndo aliyeweza kufanya haya yote hadi nayeye alipotokewa kitambi ndo akatulia
 
Prof. Mohamed Yakub Janabi (MD, MSc. Tropical Health, PhD) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya THPS. Ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kwanza na wa sasa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya jijini Dar es Salaam; aliteuliwa Septemba, 2015. Prof Janabi anahudumu kama mjumbe wa kitivo katika Vyuo Vikuu mbalimbali vikiwemo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia mwaka 2000 hadi sasa na Chuo Kikuu cha South Carolina, Marekani.

Kitaaluma, tangu 2002- hadi sasa, Prof. Janabi ni Daktari Bingwa Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili; Mkaguzi wa Matibabu wa Usafiri wa Anga aliyeidhinishwa kwa Mamlaka ya Shirikisho la Usafiri wa Anga- Marekani (2003-leo) na Profesa wa Heshima katika MUHAS pamoja na Jaribio la Chanjo ya VVU ya Mwanasayansi (TaMoVac) kutoka 1998 hadi sasa
 
Starehe isiyo na majuto kiafya, kiakili, kimwili na kiroho ni kumwabudu Mungu Muumba mbingu na nchi katika roho (imani) na kweli (vitendo).

Pombe majanga = Huharibu figo, ini, kisukari, mtikisiko kiuchumi..

Sigara majanga = Huharibu mapafu, kansa, pumzi ndogo kimazoezi.

Bangi = Maamuzi yasiyo na akili.

Uzinzi + Uasherati + Kunyaduana = Magonjwa ya zinaa, UKIMWI, UTI, tezi dume, mikosi, mtikisiko kiuchumi. Watoto wengi wa mitaani sababu ya mimba zisizotarajiwa na mivunjiko ya mahusiano/talaka za ndoa, visasi na mauaji sababu ya wivu uliopitiliza na usaliti.

"Dunia ni uwanja wa fujo, Dunia hadaa walimwengu shujaa"
Tezi dume na uasherati vinahusiana vipi?
 
Kila kitu tufanye Kwa kiasi, pombe, soda juice maji na chakula tule Kwa kiasi, naamini tutaishi maisha marefu, HATA HIVYO kuishi Nako ni Kwa neema tu.
 
Prof. Mohamed Yakub Janabi (MD, MSc. Tropical Health, PhD) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya THPS. Ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kwanza na wa sasa wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya jijini Dar es Salaam; aliteuliwa Septemba, 2015. Prof Janabi anahudumu kama mjumbe wa kitivo katika Vyuo Vikuu mbalimbali vikiwemo Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia mwaka 2000 hadi sasa na Chuo Kikuu cha South Carolina, Marekani.

Kitaaluma, tangu 2002- hadi sasa, Prof. Janabi ni Daktari Bingwa Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili; Mkaguzi wa Matibabu wa Usafiri wa Anga aliyeidhinishwa kwa Mamlaka ya Shirikisho la Usafiri wa Anga- Marekani (2003-leo) na Profesa wa Heshima katika MUHAS pamoja na Jaribio la Chanjo ya VVU ya Mwanasayansi (TaMoVac) kutoka 1998 hadi sasa
sawa. itoshe kusema ni mtaalamu wa magonjwa ya kitropiki. hayo mavyeo mengine yasikutishe kijana.
 
Sasa kwahiyo wauzaji wakale wapi? Huoni sisi tunawachangia pesa nao wale?

Kama yesu alikuwa anakunywa why me?
 
Sasa mnapoumwa mnataka michango ya wanyonge ya nini?
Unaongea tu hapa ila ukimkuta mgonjwa wa figo anavyoumwa , usingeandika ulichoandika hapa.
MItume na manabii wote walikufa, kansa je, Inasababishwa na pombe kali? Maishani jiandae kupitia uzee, ugonjwa na kifo, haviepukiki
 
Back
Top Bottom