Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Dalili za mvua ni mawingu: Mradi wa SGR hautakamilika wote ndani ya utawala wa Magufuli

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Bandugu sehemu pekee ya kuambiana ukweli hapa Tanzania imebaki Jf maana sioni gazeti, radio au Tv ambayo inaweza kujilipua na kusema ukweli au kutoa wazo lenye mantiki ya ukweli ili kuiambia ukweli serikali yetu.

Mfano ni dhahiri kuwa ujenzi wa Sgr toka Dar to Morogoro ulipangwa kukamilika 2019 na kipande hiki kina umbali wa km 202. Lakini leo hii tupo mwaka 2021 lakini nimezungumza na wadau ambao wapo site wanasema huu mwaka hawawezi kukamilisha.

Mmmoja wa wadau alie site japo kuwa sio mtaalamu sana wa civil works ila kwa uzoefu wake ameniambia kuwa kampuni ya Yapi merkez wapo slow katika kuchapa kazi. Maana anasema amefanya kazi za ujenzi kwa muda mrefu na haoni ugumu wa ujenzi wa reli maana kazi kubwa ni kujaza tuta na kisha kutandaza reli.

Kwa hiyo kukata udongo na kujaza tuta sio kazi ya kuchukua miaka minne,japokuwa kuna ujenzi wa madaraja,vituo na miundo mbinu ya umeme. Bora hii tenda wangepewa wachina tangu awali hizo km 202 zingekamilika.

Kuambia watu kuwa tutamilisha ujenzi wa Sgr ndani ya miaka 5 iliyobaki ya utawala wa JPM ni ndoto za mchana. Maana kwa kasi hii ya kampuni ya Yapi merkez ni kujidanganya kuwa vipande vya Makutupora to Moro,Dom to Tabora na Tabora to Isaka vitakamilika kwa wakati.

Inashangaza kwa nini PM Majaliwa haoni aibu kila mara kutuambia kuwa tupo karibu kuanza kupanda treni ya umeme wakati kiuhalisia bado sana.
 
Sanga hatamki maneno haya bure bure.

Tuendelee kunywa mtori nyama zipo ndani
IMG_20210205_121310_702.jpg
 
Back
Top Bottom