mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,151
Si ndivyo isemwavyo? Kwamba cheap is expensive!?Tatizo Bargain, mchina huenda alitaka mara 2 ya anachokula mturuki
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si ndivyo isemwavyo? Kwamba cheap is expensive!?Tatizo Bargain, mchina huenda alitaka mara 2 ya anachokula mturuki
Unabisha huwek data kwa sasa stesheni ya Morogoro tayr na ya DSM tayr now kuna ujenzi wa daraja la juu kabla hujaingia Dodoma ambapo juzi juzi treni ilisombwa na maji daraja la juu DSM wameandika reli tayar na wameweka pembe za ndovu like.Sgr unazindua baada ya kuijenga kichawi? Dodoma to tabora mtapajenga usiku kichawi?
Mkuu upo?
Hii tuna shida kubwa, unajiuliza tunakosaje vipaumbele kama taifa?!Hii nchi imejaa wasomi waoga hawawezi kumwambia ukweli mkuu.
ukikutana naye usiku inakuwaje?
Mkuu kama ilikuwa hujuwi waturuki ndio wauza maneno number moja Duniani usiwahi Kumwamini wala kufanya naye biashara! Yani ni Malaya wa maneno sijuwi ata ni tumie neno ganiHuo mradi kwa wingi wa graduates mtaani wangetangaza dau mradi ungeisha ndani ya miezi 6 tu. Kupanga matofali na kufunga reli ndio iwe ishu hivyo? Waturuki wao wangejenga sehemu zenye madaraja tu
Ilikua ni 70% ya 10% sijui mwananchi wa kule kijijini anaelewaa ??Tuliambiwa eti 70% imekamilika.
Naomba mwenye uelewa, technical/economical aniambie kulikuwa ma sababu gani kuruka vipande vyote hapa kati na kuanza ujenzi wa reli Mwanza to Isaka? Hapa TL ndio anashindwa kupata jibu, kama ni akili au matope yanatumika kufanya maamuziSanga hatamki maneno haya bure bure.
Tuendelee kunywa mtori nyama
Majigambo ya mwanzo haikuwa kuonyesha njia bali kujenga, tena kwa fedha za ndani. Kiburi hicho ndio kilipelekea watu kutekwa, kupigwa risasi, kuuwawa, kukataa katiba mpya kuwa watu wanataka maendeleo na sio makatiba. Kuminya uhuru wa vyombo vya habari. Hata hii kunajisi chaguzi za nchi, ziko kwenye kisingizio cha wananchi kukubali huo ujenzi jambo ambalo si kweli.Siyo vibaya ila kaonyesha njia au wewe ulitakaje mkuu
Ahaaaaa.Hiyo kampuni ya "Yapo Maelekezo" ni ya kutoka nchi gani?
Jamaa kumbe ma CON Artists wa kiwangoMkuu kama ilikuwa hujuwi waturuki ndio wauza maneno number moja Duniani usiwahi Kumwamini wala kufanya naye biashara! Yani ni Malaya wa maneno sijuwi ata ni tumie neno gani
Mimi sipingi maelezo yako ila kwa maoni yangu unaweka miundombinu kwanza kuvutia hayo yote uliyosema. ukijenga sehemu barabara, maji, umeme basi ujuwe watakuja watu kujenga makazi. Serikali kazi yake kuweka miundombinu na sera. Kilimo na viwanda ni sera tu wala haihitaji mtaji weka sera rafiki watakuja tu.Hii tuna shida kubwa, unajiuliza tunakosaje vipaumbele kama taifa?!
Una deploy mradi wa train ya umeme, sawa ni jambo jema lakini je, huo umeme tunao wa kuendesha train? Maana huu wa kuchajia simu tu bado unaleta utata.
Reli kwa kiasi kikubwa ni miundombinu inayo tarajiwa kusafirisha mizigo mingi na pengine mizito ambayo kwa barabara si efficient kuisafirisha, na kwa nchi yetu hiyo volume tungetarajia itokane na bidhaa za kilimo, viwanda na imports.
Imports zimedorora kutokana na kodi kubwa pale bandarini, kilimo ndio hivyo tena na viwanda kila mtu anaelewa sinema za awamu hii ya viwanda elfu 4.
Kwa maoni yangu nadhani ingepaswa kuwa;
-Boresha sekta ya kilimo ambayo inagusa watu wengi (>75%) ya watanzania, kisha tutapata boost kwenye uchumi kutokana na uzalishaji wa kilimo.
-Stimulate sekta ya viwanda na umeme kwa pamoja ili tuanze kusindika bidhaa kuongeza thamani kuanzia huko mashambani.
-Kisha wekeza kwenye transportation, hapa ndipo reli ingekuwa na tija kwa kuwa tuna volume ya mizigo kufeed trains zetu na kupeleka maeneo mengine ya masoko.
Aliyekwambia SGR inafika Tabora ndani ya awamu ya 5 ya miaka 10 nani?Bandugu sehemu pekee ya kuambiana ukweli hapa Tanzania imebaki Jf maana sioni gazeti, radio au Tv ambayo inaweza kujilipua na kusema ukweli au kutoa wazo lenye mantiki ya ukweli ili kuiambia ukweli serikali yetu.
Mfano ni dhahiri kuwa ujenzi wa Sgr toka Dar to Morogoro ulipangwa kukamilika 2019 na kipande hiki kina umbali wa km 202. Lakini leo hii tupo mwaka 2021 lakini nimezungumza na wadau ambao wapo site wanasema huu mwaka hawawezi kukamilisha.
Mmmoja wa wadau alie site japo kuwa sio mtaalamu sana wa civil works ila kwa uzoefu wake ameniambia kuwa kampuni ya Yapi merkez wapo slow katika kuchapa kazi. Maana anasema amefanya kazi za ujenzi kwa muda mrefu na haoni ugumu wa ujenzi wa reli maana kazi kubwa ni kujaza tuta na kisha kutandaza reli.
Kwa hiyo kukata udongo na kujaza tuta sio kazi ya kuchukua miaka minne,japokuwa kuna ujenzi wa madaraja,vituo na miundo mbinu ya umeme. Bora hii tenda wangepewa wachina tangu awali hizo km 202 zingekamilika.
Kuambia watu kuwa tutamilisha ujenzi wa Sgr ndani ya miaka 5 iliyobaki ya utawala wa JPM ni ndoto za mchana. Maana kwa kasi hii ya kampuni ya Yapi merkez ni kujidanganya kuwa vipande vya Makutupora to Moro,Dom to Tabora na Tabora to Isaka vitakamilika kwa wakati.
Inashangaza kwa nini PM majaliwa haoni aibu kila mara kutuambia kuwa tupo karibu kuanza kupanda treni ya umeme wakati kiuhalisia bado sana.
Mkuu we acha, afu watu wameshupaza shingo kusifu ujinga. Unawatazama wale wanaomsifia unaona dhahiri zile ni dhihaka wanamfanyia Rais labda sababu wamegundua anapenda kusifiwa.Wazo hili mkubwa angelipata mapema leo tungekuwa tungekuwa tunaongea mafanikio
Maamuzi ya mihemuko,kutokuwasikiliza wataalamu tumejikuta tuna miradi mikubwa inatekelezwa kwa pamoja(Bwawa la umeme mto rufiji, Treni ya mwendo kasi).
Na kuamua kufanya matumizi makubwa ya fedha yasiyozingatia bajeti na ushauri wa wataalam.