OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Wakuu,
Maisha yamekuwa magumu sana, sio kwa wazee sio kwa vijana ni kila sehemu mambo yamebana
Zifuatazo ni dalili zinazoashiria kuwa umeanza kupigika kimaisha
1. Ukiingia chooni unajisahau unaanza kwa kuvua shati badala ya suruali
2. Kusahau ndani sabuni ya kuogea then unakumbuka baada ya kufika bafuni huku ukiwa umekwisha vua nguo zote
3. Kuanza kubaini mapungufu ya mpenzi au mchepuko wako (slay queen) kuwa hakufai yupo kwaajili ya pesa
4. Kuanza kuwaogopa wanawake warembo wanaofuga kucha ndefu, wanaovaa suruali/sketi za kubana zinazoishia magotini au mapajani.
5. Kiatu kutoboka kwa chini na huoni kuwa ni tatizo ila aunatembea nacho bila kujali kuwa kimetoboka
6. Kulipia nauli ya dala dala au bajaji kwa kutumia sarafu za mia mia au miambili
7. Kuanza kununua mafuta ya kupima yale ya kupikia /kuanza kupaka mafuta ya mgando ya miatano
8. Kupata njaaa haraka, au kupoteza kabisa hamu ya kula wakati mwingine kupata maumivu ya kichwa
9. Kuwagawa mafungu mafungu dagaa wa buku kisha kuwapika kwa siku mbili au zaidi
10. Kukosa usingizi mida ya saa 8 usiku wakati mwingine kujiongelesha mwenyewe
11. Kushona zaidi ya mala mbili ndala/Malapa yaliyokatika
12. Kusahau kufunga begi la mgongoni lenye vyeti au nyaraka muhimu huku ukitembea nalo mjini katikati then wapita njia wanakushtua kuwa umesahau kufunga begi
13. Kuanza kuazima simu yenye kifurushi cha dakika umpigie mtu mwingine wakati unasimu yako iko full chaji tena ni smartphone
Wakuu ongezeeni hapo chini