Kama wao ni sunni wasingekuwa wanauwa sunni wenzao!
Wameuwa sunni kibao hapo Syria mfano mwanawazuoni wa kiislamu mkubwa hapo Syria anaitwa Sheikh Bouti. Wamemuuwa akiwa msikitini anatoa darasa kwa bomu la kujitoa mhanga.
Wamechinja sunni kibao huko Iraq. Wameuwa Sunni kibao huko Yemen mfano mwalimu wa Sheikh Al Habib Ally ibn Jifry ambaye ni Sunni. Tena huyu Sheikh ni kitukuu wa Mtume ila wamemuulia sheikh wake.
Hao watu ni mpango maalumu wa wakubwa! Kuna kipindi walipigwa wakaenda kutibiwa Israel na Netanyahu akaenda kuwatembelea.
Sasa jiulize hao waislamu ni wa aina gani ambao wanaonekana ni watata sana halafu wanafanya hivyo kwenda kutibiwa Israel? Au hata sikumoja hata kwa bahati mbaya hawajawahi kurusha kombora hata Israel?
Mbona Houth anarusha? Wao kipi kinawazuia? Hao ni project maalumu ya wakubwa.
Vikundi vya wana mgambo kutokea Iraq wanaenda kupambana nao huko Syria, Marekani anatumia helicopter zake kuwashambulia ili wasiende Syria, hapa unapata picha gani?
Yaani Marekani inawasidia magaidi?!