Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Damascus: Waasi wa HTS wauzingira mji wa Homa nchini Syria

Iran, sijui Al jazeera, Assad, Ayatola, Uturuki, Tahariri ya shama, Hawa wote ni wahuni tu wanatumia mgongo wa dini kupigania maslahi binafsi.

Jiulize Utawala wa kiislamu wa Iran unamuunga mkono Assad mwenye utawala wa kisecular, halafu unawapinga waasi wanaotaka kuanzisha utawala wa kiislamu!

Huu si ni uhuni tu.

Halafu akina Ritz wanatokwa povu kila siku kushabikia ujinga.
Unawajua vizuri hao waasi wanayoitaka Syria? Nenda kawasome objectives zao kwanza usikurupuke wote wako nchini ya mmarekani na Israel na mturuki. Hao ndio IS wanaosumbua mpaka Huku Africa wanachinja kupitia shingo very dangerous Lebanon itapitia wakati mgumu chini Hawa waasi pia Iraq na Iran wajiandae kuvamiwa Kama Hawa jamaa wataikamata Syria hivyo huwezi kumwambia Iran akae pembeni dhidi ya Hawa jamaa never
 
Mkutano wa Mashia umefanyika Leo Baghdad wamekubaliana kutuma msaada kwa Bashar Al Assad lakini Marekani inawapiga Mikwara 🤭
Mashia ndio nini ?

Wewe ni muislam ?
 
Dah roho inaniuma sana mimi hasa nikiwafikilia wakristo tu jamani watu wa MUNGU wale wataonewa sana jaman

MUNGU awatie nguvu sana
Wazee wa Madhehebu Druze pia wanahofia Usalama wao, wameamrisha Askari wote wa Kidruze walioko Jeshini waondoke waende kwenye Vijiji vya Druze huko Jebel Druze.

Sijui itakuwaje kwa Wakristo na Wayahudi na Minorities wengine kama Alawites.
 
Naona
BREAKING NEWS

Misafara ya Wanajeshi wa Urusi na Silaha nzito inaonekana ikihamishwa kutoka kambi ya jeshi la Urusi ya AIN ISSA nchini Syria kuelekea kambi iliyoko mbali na mji wa Damascus ya TABQA AIRFIELD.

Bado haijulikana kama Urusi inarudisha majeshi yake Nyuma(RETREAT) huko Syria au inaongeza nguvu (RESUPLY).

Baada ya Kuiteka miji ya ALEPPO na HAMA,Waasi wanaelekea kwenye mji wa tatu kwa ukubwa nchini Syria wa HOMS. Mji wa HOMS Upo umbali wa Kilometa 140 kutoka mji mkuu wa Damascus.

Jeshi la Israel linaanda kikosi cha Makomando 10,000 kuelekea Milima ya Golan (Golan Height) ili kujiandaa na lolote endapo waasi hao wataukaribia mji mkuu wa Damascus.

Jeshi la Uturuki linajiandaa kupeleka mifumo ya ulinzi wa Anga kasikazini mwa Syria maeneo yanayodhibitiwa na Wapiganaji wa SYRIAN NATIONAL ARMY(SNA) ambao wanaungwa mkono na Uturuki.
Mkuu Kwan Damascus iko karibu sana Golan?
 
Uzuri vita haitapigwa siku moja au wiki moja bali ni muda mrefu sasa hapa itategemeana na mwenye pumzi ndefu.

Acha waasi waendelee kufurahia honeymoon Russia anavyopigana Ukraine na Syria ni tofauti kabisa nahofia uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu hapo Syria.

Russia hapo Syria ni kama hana anacho hofia au jamii anayo ionea huruma.

Hapo Syria hamna ndugu zake warusi kama huko Ukraine useme atakuwa na ka chambe ka huruma.

Napata hofu kwa yanayo enda kutokea hapo Syria labda kama Russia aamue kumtupa Assad japo sina hakika sana.
 
Unawajua vizuri hao waasi wanayoitaka Syria? Nenda kawasome objectives zao kwanza usikurupuke wote wako nchini ya mmarekani na Israel na mturuki. Hao ndio IS wanaosumbua mpaka Huku Africa wanachinja kupitia shingo very dangerous Lebanon itapitia wakati mgumu chini Hawa waasi pia Iraq na Iran wajiandae kuvamiwa Kama Hawa jamaa wataikamata Syria hivyo huwezi kumwambia Iran akae pembeni dhidi ya Hawa jamaa never
Kwan Iran inapakana na Syria ndugu?
 
Wazee wa Madhehebu Druze pia wanahofia Usalama wao, wameamrisha Askari wote wa Kidruze walioko Jeshini waondoke waende kwenye Vijiji vya Druze huko Jebel Druze.

Sijui itakuwaje kwa Wakristo na Wayahudi na Minorities wengine kama Alawites.
Alawites si waislam hao Amna shida
 
Israel huwa ina solutions, alternative solutions na "bahati" za kutosha zilizopangwa.

Hamas wamekurupuka kuua mamia ya Wayahudi, Israel inawadhibiti na kuingia Gaza kusafisha. Hezbollah wanaanzisha mashambulizi, Israel inawashambulia taratibu haiendi kwa fujo. Baadae inaonekana Iran inatishia sana itasaidiana na haya makundi mawili, Rais wa Iran anakufa kwa ajali "bahati mbaya".

Hamas inapigwa inaelekea ukingoni, Hezbollah inaanzishiwa lakini Iran wala haiisaidii maana Rais mkorofi hayupo tena. Hezbollah inapigwa inaanzisha mazungumzo ya amani hapohapo Syria ambapo inapitisha silaha waasi wanaanzisha mapigano.

Hivyo waasi hawa wakiiletea changamoto Israel, bado solutions za kutosha zipo mikononi mwa Israel. Ndio maana measure ya kwanza ni kupeleka majeshi Golan heights mpakani na Syria.

Kwenye mlinganyo huwezi ona msaada wa Israel kwa hao waasi ila Israel yenyewe inafanya vitu kwa hesabu inaenda mbele inarudi nyuma. Sasa hawa wakurupukaji wanashangilia tukio moja kumbe yenyewe iko na strategic responses.

Yani Israel inaweza ona inashambulia magaidi huku inalaumiwa na dunia, ikaomba mazungumzo yakafanyika huku ikijua wakurupukaji wataishambulia tena. Ikakaaa ikaandaa vifungu vya kuiruhusu kushambulia ikichokozwa, ikatulia kama mnyonge ikakusanya ushahidi na vithibitisho kuwa inavunjiwa amani. Alafu ikashambulia vikali kwa kisingizio sisi hatuna fujo tunajitetea tu.
Update: Israel ina solution nyingine. Imeitaarifu Marekani kuwa itafanya operation Kusini Magharibi mwa Syria endapo waasi watauteka mji wa Homs. Itaenda kuweka buffer zone ili waasi wasiijie Golan heights.

Mambo yanazidi kuharibika hapo ME.
 

View: https://x.com/Osint613/status/1864746846591046027

Safari hii Israel Ndio inaweza ikawa nchi itakayomtoa Assad hapo Damascus.

Utawala wa Assad umebakia miji mitatu ya Kuilinda Latakia, Homs na Damascus, hii situation inampa wakati mgumu Assad kubaki madarakani bila msaada wa Iran, Hezbollah ameumizwa sana hakuna impact ataleta.

Kama Iran hatomsikiliza Israel basi, Itabidi Israel aishambulie Serikali ya Syria jambo ambalo litazidi kumdhoofisha Sana na pengine Israel inaweza kuingia ndani kabisa ya Syria... Kutoka Golan heights hadi Damascus ni KM 60.

Assad akubali kuigawa Syria kwenye Federation
 
Uzuri mnaandika wenyewe kuwa Israel inawasaidia waasi(magaidi yanayo chinja chinja wakristo).

Na kule kwengine mnasema Israel vita vyake ni dhidi ya magaidi.

Kwa hakika dunia ya leo tunashuhudia uongo wa muda mrefu katika mambo mbalimbali tuliyo kuwa tukiaminishwa na ulimwengu wa magharibi.
 
Back
Top Bottom