DOKEZO Dampo katika Soko la Stereo lililopo Temeke ni kero kubwa, Mamlaka ziongeze nguvu katika kuzoa taka

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Dampo lililopo kwenye soko la Stereo hapa Tekeme, Dar es Salaam ambapo ni sehemu kwa Wauzaji wa soko hili kuhifadhi takataka baada ya wao kufanya usafi kwenye maeneo yao, limekuwa ni kero kubwa kwa Wafanyabiashara na Wanunuaji wa bidhaa katika Soko hilo.



Wafanyabiashara katika soko hili kwa kiwango fulani wanajitahidi kufanya usafi na kuweka mazingira safi katika vichanja/meza zao za bishara lakini takataka hizo ambazo zinakusanywa katika sehemu moja karibu na geti la kutokea/kuingilia sokoni ili Mamlaka husika kuja kuchukua na kupeleka kutupwa zimekuwa kero kwani zimakuwa zikirundikana na kutoa harufu kali



Watumiaji wa soko hilo wamesema japo Mamlaka huwa inapunguza (Bila kuzitoa zote) takataka hizo kila baada ya muda, wanaomba mmalaka iongeze nguvu ya kuzizoa na kuzimaliza kabisa kwa kila siku kwani bila kufanya hivyo sehemu hiyo imegeuka dampo kubwa na eneo hilo halistahili kuwa Dampo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…