TISHETI PLAIN DODOMA
JF-Expert Member
- Jan 30, 2025
- 617
- 1,910
Hakuna mtu aliyetarajia hivi. Mwaka 2021 tulipompokea Samuya tulidhani tumepata Mama , aliyeahidi kufungua nafasi ya kisiasa. Leo, miaka minne tu baadaye, vijana wetu wengi wamepotezwa hawaonekani tena.Video za mochwari za Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya ndo zinazidi kutia simanzi kubwa sana, je haya yote yalifanyika ili kulinda madaraka ya samuya tu. Uchafuzi wa Oktoba 29, 2025 uliokuja na “ushindi feki ” wa asilimia 98 umegeuka kuwa janga la damu. Ripoti za ndani za hospitali zinasema zaidi ya watu 1000 wameuawa na risasi za polisi, maelfu wamejeruhiwa, mamia wamepotea. Na sasa, kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kesi imefunguliwa rasmi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) dhidi ya Samuya na maafisa wake wa juu kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu.