KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania.

Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba.

IMG_7879.jpeg

Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
 
Tunachokijua
Dan Friedkin alizaliwa 1965, ni mfanyabiashara na bilionea wa Marekani, mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa The Friedkin Group na kampuni yake tanzu ya Gulf States Toyota, ambayo ilianzishwa na baba yake, Thomas H. Friedkin. Pia ni mmiliki na Rais wa klabu ya soka ya A.S. Roma.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hadi kufikia Februari 2023, makadirio ya utajiri wa Dan Friedkin ni dola bilioni 5.7.

Pamoja na hayo, Dan Friedkin ni mwekezaji katika kampuni ya usimamizi wa mahoteli ya kifahari ya Auberge Resorts na mfuko wa uhifadhi, Friedkin Conversation Fund.

Uwepo wao Nchini Tanzania
Friedkin Conservation Fund ni shirika linaloshughulika na masuala ya mazingira, uhifadhi na utalii. Shirika hili limesajiliwa Marekani. The Friedkin Conservation Fund of Tanzania ambayo ni sehemu ya umiliki wao limeanzishwa nchini Tanzania kama shirika lisilotengeneza faida.

Katika tovuti yao rasmi, Shirika hilo limeandika;

"Shughuli zetu Tanzania zimesukumwa na dhamira yetu katika uhifadhi wa mazingira na moyo wa hisani. Tumewekeza mabilioni ya shilingi katika jamii ili kuzisaidia kukuza uchumi na kusaidia nchi hii nzuri tunayoipenda sana"

Aidha, Shirika hilo limeonesha makao yake makuu kuwa Jiji la Arusha limetaja mambo 3 ambayo ni dhamira yake kuwepo nchini ambayo ni;
  1. Kusaidia Serikali ya Tanzania na wananchi wa wake kwa juhudi zao za kuhifadhi mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa.
  2. Kuhirikisha jamii za vijijini katika uhifadhi wa urithi wao wa asili na kuwawezesha kupunguza baadhi ya hali zinazochangia umaskini.
  3. Kufuatilia, kutafiti na kuwezesha mipango katika matumizi endelevu ya maliasili.

Uhifadhi wa Ardhi
Kwa mujibu wa tovuti ya Tanzania Invest, Friedkin Conservation Trust inahifadhi takriban ekari milioni 6.1 zilizoko kaskazini mwa Tanzania. Aidha Ekari 300,000 za hifadhi za Friedkin huruhusu wageni kutembelea na kuona wanyama kwenye mbuga ya Serengeti.

Madai haya yanathibitishwa pia na Blog hii inayohusianishwa na Taasisi hiyo. Aidha, Mwaka 2017, Mtumiaji mmoja wa JamiiForums aliwahi kuweka chapisho ambalo pamoja na mambo mengine lilikuwa linaonesha uwepo wa Taasisi hii kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mwaka 2015, Friedkin Conversation Trust iliipa Tanzania Tsh Bilioni 231.55 ili kulinda mazingira na kukuza utalii.

Kazi zao nchini Tanzania zinatajwa kuanza miaka ya 1989 na Thomas Friedkin, Baba mzazi wa Dan Friedkin aliyefariki Machi 14, 2017 akiwa na umri wa miaka 81.

Hata hivyo, ingawa vyanzo kadhaa, ikiwemo makala katika jarida la Forbes inayosema kwamba taasisi inayomilikiwa na familia Freiedkin – yaani Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org) – imekodisha ekari milioni 6 za pori la Tanzania kwa lengo la kuzilinda, wawakilishi wa bilionea huyo walikanusha madai hayo.

"Friedkin Conservation Fund ni shirika la misaada lisilo la faida ambalo wadhamini wake ni Watanzania, na Dan Friedkin akiwa mfadhili ili kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii," alinukuliwa akisema mwakilishi huyo.

Aidha, Septemba 4, 2023, Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin walitoa taarifa nyingine inayokanusha madai ya kumiliki eneo linalofikia ekari milioni 6 nchini Tanzania.

Sehemu ya taarifa yao iliyotolewa kwa umma ilisema jumla ya eneo lote lililopangishwa kwa kampuni ya Mwiba Holdings Limited wilayani Meatu ni kiasi cha ekari 171,604 - na si ekari milioni 6 kama inavyodaiwa na wale waliowaita kuwa ni wazushi.

Aidha, taarifa hiyo ilibainisha kuwa Kampuni ya Mwiba Holdings haimiliki eneo lolote kwenye maeneo ya hifadhi nchini Tanzania na kuwa haijaingia mkataba wowote (moja kwa moja au kupitia kwa mtu au taasisi nyingine) na Serikali ya Awamu ya Sita.

img_8412-jpeg.2738973

Barua ya ufafanuzi ya Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin
Mikataba yote ya UPANGAJI na UWEKEZAJI imekuwepo kwa muda mrefu na iliongezewa muda mwaka 2018 na 2019 wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Hivyo, madai ya Thomas Dan Friedkin kuwa na hifadhi ya ardhi Tanzania yana ukweli japokuwa sio kwa kiasi cha ekari milioni 6 kama zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Hakuna kitu kama hicho, hunting block zinatolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa makampuni kwa kukodishwa na wanalipa fee kila mwaka.

Umeingia kwenye eneo ambalo nimefanyakazi kwa muda mrefu.

Mzungu aliyewahi kuwa na vitalu vingi hasa Selous game reserve ni Gerald Pasanisi tu wa Nice France na ameshafariki, na vitalu vingi amevirudisha serikalini baada ya Magufuli kuvamia hiyo sector without know how
 
View attachment 2696387
HUYU MZUNGU NI MUWEKEZAJI WA MWIBA GAME RESERVE ANA HEKARI KARIBU 25.000 NDANI YA HIFADHI YA MBUGA ZA WANYAMA.
Na ana mpango wa kuchukuwa karibu Hekari 6 Milioni za Ardhi nchini mwetu Tanzania. Wa-Tanzania amkeni itafika siku nchi yetu yote imeuzwa na wawekezaji tutakuwa Wananchi hatuna ardhi ya kuishi kazi kwenu. Tanzania itakuwa kama nchi ya Zimbabwe siku zijazo ninatabiri hivyo.

Watanzania watajakuwa walinzi na vibarua wa mali walizoziuza wenyewe.
 
Na nyie tafuteni fursa mkachukue maeneo huko

Ova
Siyo kweli, uongo mtupu, hata Dr Rick Abdallah mchambuzi wa mpira ana vitalu na ana kampuni ya hunting.

Rostam Aziz kampuni yake inaitwa Miombo safari ipo Masaki anaendesha Mdogo wake yupo na mzungu mmoja wa kunduchi anaitwa Michelle wana vitalu vya uwindaji.
 
Hakuna kitu kama hicho, hunting block zinatolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa makampuni kwa kukodishwa na wanalipa fee kila mwaka.

Umeingia kwenye eneo ambalo nimefanyakazi kwa muda mrefu.

Mzungu aliyewahi kuwa na vitalu vingi hasa Selous game reserve ni Gerald Pasanisi tu wa Nice France na ameshafariki, na vitalu vingi amevirudisha serikalini baada ya Magufuli kuvamia hiyo sector without know how
American billionaire Dan Friedkin, Chairman of Friedkin Group,owns Italian football club AS Roma, and owns Gulf States Toyota is the owner of the 25 000 acres Mwiba Game Reserve in Tanzania. He also leases up to 6 million acres of Tanzanian wilderness he plans to privatise. source.
 
Huyu Mzungu alikimbia Tanzania kipindi cha Magufuli akaenda nunua timu ya mpira Italy As Roma akamuajiri Mourinho....

Huyu bilionea nchi kibao zinatamni akawekeze kwao ..Sisi Magufuli alimtibua Sana akatukimbia..

Tuache malalamiko ya kimasikini...
Mzungu abembelezwe arudi kuwekeza sehemu mbalimbali...
Hamtaki waarabu na Wazungu pia ?
 
Hakuna kitu kama hicho, hunting block zinatolewa na wizara ya maliasili na utalii kwa makampuni kwa kukodishwa na wanalipa fee kila mwaka.

Umeingia kwenye eneo ambalo nimefanyakazi kwa muda mrefu.

Mzungu aliyewahi kuwa na vitalu vingi hasa Selous game reserve ni Gerald Pasanisi tu wa Nice France na ameshafariki, na vitalu vingi amevirudisha serikalini baada ya Magufuli kuvamia hiyo sector without know how
Namkumbuka huyu Pasanisi na magari yAke kama maroli ya jeshi
 
Siyo kweli, uongo mtupu, hata Dr Rick Abdallah mchambuzi wa mpira ana vitalu na ana kampuni ya hunting.

Rostam Aziz kampuni yake inaitwa Miombo safari ipo Masaki anaendesha Mdogo wake yupo na mzungu mmoja wa kunduchi anaitwa Michelle wana vitalu vya uwindaji.
Wanavyo mpaka nchi za kusini mwa africa! Miombo sio mchezo
 
Kama sio mwarabu acha achukue tu. Jamaa wanaojifanya wapinzani hawana mpango nae🤣🤣🤣🤣
Msichanganye mada, hunting block ziko wazi kuombwa na makampuni yote, Tena Kigwangwalla alileta mfumo wa kuomba kwa njia ya mnada.

Na kwa wawindaji local kwa ajili ya kitoweo zipo open area vibali vinatoka halmashauri husika.
 
Huyu Mzungu alikimbia Tanzania kipindi cha Magufuli akaenda nunua timu ya mpira Italy As Roma akamuajiri Mourinho....

Huyu bilionea nchi kibao zinatamni akawekeze kwao ..Sisi Magufuli alimtibua Sana akatukimbia..

Tuache malalamiko ya kimasikini...
Mzungu abembelezwe arudi kuwekeza sehemu mbalimbali...
Hamtaki waarabu na Wazungu pia ?
Mkuu wawekezaji tunawahitaji wawe ni Wazungu au waarabu au watu weusi lakini katika kuwekeza kuwepo na makubaliano maalum yenye kunufaisha Taifa kwa ujumla. Siyo aje muwekezaji afanye mpango wa kuwekeza kwa maslahi yake mwenyewe, awape baadhi ya Viongozi wetu waliopo Serikalini Rushwa ya Pesa ili wapate kumpitishia Mkataba wa uwekezaji wake anavyotaka yeye mwenyewe aka awekeze kwa mfano miaka 100 au zaidi ya hapo. Na aje kufanya anavyotaka katika nchi yetu eti kwa sababu amewekeza sisi wananchi masikini ndio tutakuwa watumwa wake katika kuendeleza uwekezaji wake, hivyo hatutaji mambo ya ubwanyenye aka ukoloni mambo leo. Hatutaki Mambo ya mikataba feki au mikataba hewa ya kutuumiza sisi wenyewe katika nchi yetu.
 
Namkumbuka huyu Pasanisi na magari yAke kama maroli ya jeshi
Yes, yeye ndio aliyemshawishi Nyerere aruhusu uwindaji na Nyerere aliporuhusu Pasanisi alianza kuwinda kama PH kupitia Tawico ya serikali na baadaye yeye ndio akiwa mtu wa kwanza kuanzisha private company ya uwindaji ya Tanganyika wildlife Safari.

Kenya mpaka leo hawaruhusu uwindaji, huyu Pasanisi alikuwa lobbyists hasa kumshawishi Nyerere mpaka akalegea siyo mchezo.
 
Msichanganye mada, hunting block ziko wazi kuombwa na makampuni yote, Tena Kigwangwalla alileta mfumo wa kuomba kwa njia ya mnada.

Na kwa wawindaji local kwa ajili ya kitoweo zipo open area vibali vinatoka halmashauri husika.
Mbona umeanza kuona maluweluwe; Dr wa PhD ya mchongo?🤣
 
Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
Huyu jamaa ni Patner wa Nyaga Mawalla wa Mwiba Holdings, baada ya Nyaga kufariki yeye ndiye anaimiliki Mwiba.

Huyu jamaa ni mtu poa sana, na kampuni yake inafanya mambo makubwa mazuri ya hifadhi na kulisaidia taifa.

Nimemfanyia baadhi ya kazi zake za Publicity, he is a good man and the deal is a good deal.

Msiwe na wasiwasi nae, yuko legit kabisa!.
P
 
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania.

Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba.

Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
Ok
 
Back
Top Bottom