KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania.

Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba.

IMG_7879.jpeg

Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
 
Tunachokijua
Dan Friedkin alizaliwa 1965, ni mfanyabiashara na bilionea wa Marekani, mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa The Friedkin Group na kampuni yake tanzu ya Gulf States Toyota, ambayo ilianzishwa na baba yake, Thomas H. Friedkin. Pia ni mmiliki na Rais wa klabu ya soka ya A.S. Roma.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hadi kufikia Februari 2023, makadirio ya utajiri wa Dan Friedkin ni dola bilioni 5.7.

Pamoja na hayo, Dan Friedkin ni mwekezaji katika kampuni ya usimamizi wa mahoteli ya kifahari ya Auberge Resorts na mfuko wa uhifadhi, Friedkin Conversation Fund.

Uwepo wao Nchini Tanzania
Friedkin Conservation Fund ni shirika linaloshughulika na masuala ya mazingira, uhifadhi na utalii. Shirika hili limesajiliwa Marekani. The Friedkin Conservation Fund of Tanzania ambayo ni sehemu ya umiliki wao limeanzishwa nchini Tanzania kama shirika lisilotengeneza faida.

Katika tovuti yao rasmi, Shirika hilo limeandika;

"Shughuli zetu Tanzania zimesukumwa na dhamira yetu katika uhifadhi wa mazingira na moyo wa hisani. Tumewekeza mabilioni ya shilingi katika jamii ili kuzisaidia kukuza uchumi na kusaidia nchi hii nzuri tunayoipenda sana"

Aidha, Shirika hilo limeonesha makao yake makuu kuwa Jiji la Arusha limetaja mambo 3 ambayo ni dhamira yake kuwepo nchini ambayo ni;
  1. Kusaidia Serikali ya Tanzania na wananchi wa wake kwa juhudi zao za kuhifadhi mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa.
  2. Kuhirikisha jamii za vijijini katika uhifadhi wa urithi wao wa asili na kuwawezesha kupunguza baadhi ya hali zinazochangia umaskini.
  3. Kufuatilia, kutafiti na kuwezesha mipango katika matumizi endelevu ya maliasili.

Uhifadhi wa Ardhi
Kwa mujibu wa tovuti ya Tanzania Invest, Friedkin Conservation Trust inahifadhi takriban ekari milioni 6.1 zilizoko kaskazini mwa Tanzania. Aidha Ekari 300,000 za hifadhi za Friedkin huruhusu wageni kutembelea na kuona wanyama kwenye mbuga ya Serengeti.

Madai haya yanathibitishwa pia na Blog hii inayohusianishwa na Taasisi hiyo. Aidha, Mwaka 2017, Mtumiaji mmoja wa JamiiForums aliwahi kuweka chapisho ambalo pamoja na mambo mengine lilikuwa linaonesha uwepo wa Taasisi hii kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mwaka 2015, Friedkin Conversation Trust iliipa Tanzania Tsh Bilioni 231.55 ili kulinda mazingira na kukuza utalii.

Kazi zao nchini Tanzania zinatajwa kuanza miaka ya 1989 na Thomas Friedkin, Baba mzazi wa Dan Friedkin aliyefariki Machi 14, 2017 akiwa na umri wa miaka 81.

Hata hivyo, ingawa vyanzo kadhaa, ikiwemo makala katika jarida la Forbes inayosema kwamba taasisi inayomilikiwa na familia Freiedkin – yaani Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org) – imekodisha ekari milioni 6 za pori la Tanzania kwa lengo la kuzilinda, wawakilishi wa bilionea huyo walikanusha madai hayo.

"Friedkin Conservation Fund ni shirika la misaada lisilo la faida ambalo wadhamini wake ni Watanzania, na Dan Friedkin akiwa mfadhili ili kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii," alinukuliwa akisema mwakilishi huyo.

Aidha, Septemba 4, 2023, Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin walitoa taarifa nyingine inayokanusha madai ya kumiliki eneo linalofikia ekari milioni 6 nchini Tanzania.

Sehemu ya taarifa yao iliyotolewa kwa umma ilisema jumla ya eneo lote lililopangishwa kwa kampuni ya Mwiba Holdings Limited wilayani Meatu ni kiasi cha ekari 171,604 - na si ekari milioni 6 kama inavyodaiwa na wale waliowaita kuwa ni wazushi.

Aidha, taarifa hiyo ilibainisha kuwa Kampuni ya Mwiba Holdings haimiliki eneo lolote kwenye maeneo ya hifadhi nchini Tanzania na kuwa haijaingia mkataba wowote (moja kwa moja au kupitia kwa mtu au taasisi nyingine) na Serikali ya Awamu ya Sita.

img_8412-jpeg.2738973

Barua ya ufafanuzi ya Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin
Mikataba yote ya UPANGAJI na UWEKEZAJI imekuwepo kwa muda mrefu na iliongezewa muda mwaka 2018 na 2019 wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Hivyo, madai ya Thomas Dan Friedkin kuwa na hifadhi ya ardhi Tanzania yana ukweli japokuwa sio kwa kiasi cha ekari milioni 6 kama zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Nd'o vile papaa,kuna wadada wa kiKenya wanamiliki mamia ya hekari Ruvuma na Rukwa,wanawezeshwa na KCB,halafu vijana tunawashauri Sumbawanga kuna mapori ya bure,wanajibu eti ni mbali tena kuna wachawi,subirini pakuche mtajuta!!!
 
wapigaji tu hao mwiba holdings....hema moja camp kwa siku tau wanakodisha hadi tzs 10m...hao wanadili na wawindaji matajiri pale makao simiyu...wapigaji kwa kivuli cha ngo
Wanakula na wakubwa hao, serikali wanajua kila kitu na ndiyo maana wanapokea gawio, unadhani mtu anakupa gawio wakati hafanyi biashara kuna nini humo ndani?.

Hii nchi bana, ndiyo maana mlimfukuza aliyekuwa spika ndg Ndugai kwa kusema "kuna siku nchi itauzwa"
 
WhatsApp Image 2023-07-22 at 20.46.01.jpeg


HUYU MZUNGU NI MUWEKEZAJI WA MWIBA GAME RESERVE ANA HEKARI KARIBU 25.000 NDANI YA HIFADHI YA MBUGA ZA WANYAMA.

Na ana mpango wa kuchukuwa karibu Hekari 6 Milioni za Ardhi nchini mwetu Tanzania. Wa-Tanzania amkeni itafika siku nchi yetu yote imeuzwa na wawekezaji tutakuwa Wananchi hatuna ardhi ya kuishi kazi kwenu. Tanzania itakuwa kama nchi ya Zimbabwe siku zijazo ninatabiri hivyo.
 
Back
Top Bottom