KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Aprili 27, 2023, akaunti ya Mtandao wa Twitter inayotumia jina la MainLandAfrica iliweka chapisho linalodai kuwa Bilionea wa Marekani Dan Friedkin amekodisha takriban Ekari 6,000,000 za ardhi nchini Tanzania.

Chapisho hilo lilienda mbali zaidi kwa kudai kuwa Friedkin ni mmiliki wa Ekari zingine 25,000 za ardhi zinazounda pori la Akiba la Mwiba.

IMG_7879.jpeg

Wanaojua kuhusu huyu jamaa watupe details anafanya biashara gani na ardhi kubwa kiasi hicho?
 
Tunachokijua
Dan Friedkin alizaliwa 1965, ni mfanyabiashara na bilionea wa Marekani, mmiliki na Mkurugenzi Mtendaji wa The Friedkin Group na kampuni yake tanzu ya Gulf States Toyota, ambayo ilianzishwa na baba yake, Thomas H. Friedkin. Pia ni mmiliki na Rais wa klabu ya soka ya A.S. Roma.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, hadi kufikia Februari 2023, makadirio ya utajiri wa Dan Friedkin ni dola bilioni 5.7.

Pamoja na hayo, Dan Friedkin ni mwekezaji katika kampuni ya usimamizi wa mahoteli ya kifahari ya Auberge Resorts na mfuko wa uhifadhi, Friedkin Conversation Fund.

Uwepo wao Nchini Tanzania
Friedkin Conservation Fund ni shirika linaloshughulika na masuala ya mazingira, uhifadhi na utalii. Shirika hili limesajiliwa Marekani. The Friedkin Conservation Fund of Tanzania ambayo ni sehemu ya umiliki wao limeanzishwa nchini Tanzania kama shirika lisilotengeneza faida.

Katika tovuti yao rasmi, Shirika hilo limeandika;

"Shughuli zetu Tanzania zimesukumwa na dhamira yetu katika uhifadhi wa mazingira na moyo wa hisani. Tumewekeza mabilioni ya shilingi katika jamii ili kuzisaidia kukuza uchumi na kusaidia nchi hii nzuri tunayoipenda sana"

Aidha, Shirika hilo limeonesha makao yake makuu kuwa Jiji la Arusha limetaja mambo 3 ambayo ni dhamira yake kuwepo nchini ambayo ni;
  1. Kusaidia Serikali ya Tanzania na wananchi wa wake kwa juhudi zao za kuhifadhi mtandao wa maeneo yaliyohifadhiwa.
  2. Kuhirikisha jamii za vijijini katika uhifadhi wa urithi wao wa asili na kuwawezesha kupunguza baadhi ya hali zinazochangia umaskini.
  3. Kufuatilia, kutafiti na kuwezesha mipango katika matumizi endelevu ya maliasili.

Uhifadhi wa Ardhi
Kwa mujibu wa tovuti ya Tanzania Invest, Friedkin Conservation Trust inahifadhi takriban ekari milioni 6.1 zilizoko kaskazini mwa Tanzania. Aidha Ekari 300,000 za hifadhi za Friedkin huruhusu wageni kutembelea na kuona wanyama kwenye mbuga ya Serengeti.

Madai haya yanathibitishwa pia na Blog hii inayohusianishwa na Taasisi hiyo. Aidha, Mwaka 2017, Mtumiaji mmoja wa JamiiForums aliwahi kuweka chapisho ambalo pamoja na mambo mengine lilikuwa linaonesha uwepo wa Taasisi hii kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mwaka 2015, Friedkin Conversation Trust iliipa Tanzania Tsh Bilioni 231.55 ili kulinda mazingira na kukuza utalii.

Kazi zao nchini Tanzania zinatajwa kuanza miaka ya 1989 na Thomas Friedkin, Baba mzazi wa Dan Friedkin aliyefariki Machi 14, 2017 akiwa na umri wa miaka 81.

Hata hivyo, ingawa vyanzo kadhaa, ikiwemo makala katika jarida la Forbes inayosema kwamba taasisi inayomilikiwa na familia Freiedkin – yaani Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org) – imekodisha ekari milioni 6 za pori la Tanzania kwa lengo la kuzilinda, wawakilishi wa bilionea huyo walikanusha madai hayo.

"Friedkin Conservation Fund ni shirika la misaada lisilo la faida ambalo wadhamini wake ni Watanzania, na Dan Friedkin akiwa mfadhili ili kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya jamii," alinukuliwa akisema mwakilishi huyo.

Aidha, Septemba 4, 2023, Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin walitoa taarifa nyingine inayokanusha madai ya kumiliki eneo linalofikia ekari milioni 6 nchini Tanzania.

Sehemu ya taarifa yao iliyotolewa kwa umma ilisema jumla ya eneo lote lililopangishwa kwa kampuni ya Mwiba Holdings Limited wilayani Meatu ni kiasi cha ekari 171,604 - na si ekari milioni 6 kama inavyodaiwa na wale waliowaita kuwa ni wazushi.

Aidha, taarifa hiyo ilibainisha kuwa Kampuni ya Mwiba Holdings haimiliki eneo lolote kwenye maeneo ya hifadhi nchini Tanzania na kuwa haijaingia mkataba wowote (moja kwa moja au kupitia kwa mtu au taasisi nyingine) na Serikali ya Awamu ya Sita.

img_8412-jpeg.2738973

Barua ya ufafanuzi ya Mwiba Holdings Limited na Thomas Dan Friedkin
Mikataba yote ya UPANGAJI na UWEKEZAJI imekuwepo kwa muda mrefu na iliongezewa muda mwaka 2018 na 2019 wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Hivyo, madai ya Thomas Dan Friedkin kuwa na hifadhi ya ardhi Tanzania yana ukweli japokuwa sio kwa kiasi cha ekari milioni 6 kama zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Siyo kweli, uongo mtupu, hata Dr Rick Abdallah mchambuzi wa mpira ana vitalu na ana kampuni ya hunting.

Rostam Aziz kampuni yake inaitwa Miombo safari ipo Masaki anaendesha Mdogo wake yupo na mzungu mmoja wa kunduchi anaitwa Michelle wana vitalu vya uwindaji.

Hapo umenena kweli leaky Abdallah ana mdogo wake yuko kibondo huko mabamba anaitwa Jamal nilikua nikienda kwake kumtembelea muda wa kwenda burundi nilikua nakula nyama za pori sana. Ndio nimejua sasa
 
Lakini huyu Mmarekani si ni mkristo na sio mwarabu?...
Shida iko wapi???


Halafu Lissu anajitia Saba aibu kudandia taarifa za mitandaoni
Friedkin yupo Tanzania toka wakati wa Mkapa...
Kuja kusema Samia kampa ardhi ni upumbavu kabisa
Kwa hiyo mkristo aibe tu raslimali zetu?

Ukiambiwa wewe ni punguani utakataa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini huyu Mmarekani si ni mkristo na sio mwarabu?...
Shida iko wapi???


Halafu Lissu anajitia Saba aibu kudandia taarifa za mitandaoni
Friedkin yupo Tanzania toka wakati wa Mkapa...
Kuja kusema Samia kampa ardhi ni upumbavu kabisa
Usipanic 😂😂🔥🔥

Lisu hajasema Thomas kapewa ardhi na nani bwashee

Marekani ndio wanaimiliki Saudi Arabia 😄 kwahiyo ni kweli ni Wagalatia wale
 
Naye anaruhusiwa kumiliki afuate tu sheria na tararibu,na mchanganuo anataka kufanyia nini?,atapatiwa bila shaka,na atapewa kwa vipindi,33yrs, 66yrs,99yrs.
HUYU MWEHU ANAJARIBU KUTUMIA KILA NJIA KUCHONGANISHA SEREKALI NA WANANCHI, (INFLICTION AND TROUBLE MAKER)
•~APUUZWE BURE KABISA~•
JK: Ukiwa Mwanasiasa Lazima uwe na ngozi ngumu
 
Lakini huyu Mmarekani si ni mkristo na sio mwarabu?...
Shida iko wapi???


Halafu Lissu anajitia Saba aibu kudandia taarifa za mitandaoni
Friedkin yupo Tanzania toka wakati wa Mkapa...
Kuja kusema Samia kampa ardhi ni upumbavu kabisa
Kamtaja samia? We punga nini? Na unapoleta hoja ya huyu mkristo na yule sjui nani, Tundu lissu alimkemea Magufuli mkatoliki, mkapa mkatoliki, hiyo ya udini mnajua nyinyi na akili zenu ndogo
 
Lakini huyu Mmarekani si ni mkristo na sio mwarabu?...
Shida iko wapi???


Halafu Lissu anajitia Saba aibu kudandia taarifa za mitandaoni
Friedkin yupo Tanzania toka wakati wa Mkapa...
Kuja kusema Samia kampa ardhi ni upumbavu kabisa

Sasa Ukristo na Uislam unakujaje? Huwezi jadili topic? Kuna watu gamboot kabisa
 

"Mwiba Holdings Ltd operates the ranch and has been paying annual land rental and servicing the lease agreement for the 48,548 acres for the Mwiba Ranch, 10,872 acres for Mwangundo, and 112,183 acres for the Makao WMA," says the representative.

Picture1.jpg
 
• Huyu jamaa ndiye anayetajwa na Tundu Lissu kwenye mikutano ya CHADEMA inayoendelea nchi nzima kuwa anamiliki ekari million 6 kwenye hifadhi zetu..

• Huyu jamaa na familia yake huko Houston - Texas - USA ndiyo waliolipia gharama za utengenezaji wa filamu ya "Royal Tour" ambayo sterling wake alikuwa "nani kama mama" Rais Samia Suluhu Hassan

• Endeleeni kuunganisha dots mpaka tupate kitu kamili.

Twendeni tu mdogo mdogo mpaka kitaaeleweka tu..!!
================================================
aee3e9d1-4143-4ad7-904b-8453e3e7d39c.jpg

===================================================
Mwiba: A Tanzanian wildlife ranch under lease to American billionaire’s company

In summary:
Dar es Salaam. Tanzania is home to one of the best wildlife reserves in Africa, making it a revered safari destination for many across the world, but not much is known about Mwiba Wildlife Ranch, a property leased to Mwiba Holdings Limited, owned by American billionaire Dan Friedkin.

The Texas-based businessman, who is also the chairman of Gulf States Toyota, is the beneficial owner of Mwiba Holdings Ltd.

According to their local representatives, the area was acquired in 2008 on a 30-year lease after an agreement was reached between Makao Village Council and Meatu District Council.

"Mwiba Holdings Ltd operates the ranch and has been paying annual land rental and servicing the lease agreement for the 48,548 acres for the Mwiba Ranch, 10,872 acres for Mwangundo, and 112,183 acres for the Makao WMA," says the representative.

Spread over thousands of acres, Mwiba borders the Ngorongoro Conservation Area’s western boundary and the southern part of Serengeti National Park.

Serengeti’s wildebeest migration passes through Mwiba between December and April. Characterized by rolling hills, kopjes, thickets, waterholes, and (dry) rivers where pools form, its permanent water attracts wildlife all year round.

Visitors who have been there say it is an animal magnet when the southern Serengeti and the Ngorongoro Conservation Areas dry out between July and November each year.

The Mwiba Lodge, an eye-catching beauty that complements the area, costs $1,800 per person and was built with a near-stealth presence in the landscape.

Though an article in Forbes says the billionaire’s family trust, the Friedkin Conservation Fund (friedkinfund.org), has leased an astonishing 6 million acres of Tanzania's wilderness with an eye towards protecting it, his representatives have refuted the claims.

"Friedkin Conservation Fund is a charity organization whose trustees are Tanzanians, with Dan Friedkin as the sponsor of the trust to support wildlife conservation and community development," he says.

He named the trustees as Abdulkadir Luta Mohammed, Asela Msando, and Naib Sykes and further clarified that Mwiba Holdings is a wildlife ranch that belongs to Makao Village Council as the owner.
==================================================

Source: Gazeti la The Citizen la August 2, 2023
 
Naye anaruhusiwa kumiliki afuate tu sheria na tararibu,na mchanganuo anataka kufanyia nini?,atapatiwa bila shaka,na atapewa kwa vipindi,33yrs, 66yrs,99yrs.
HUYU MWEHU ANAJARIBU KUTUMIA KILA NJIA KUCHONGANISHA SEREKALI NA WANANCHI, (INFLICTION AND TROUBLE MAKER)
•~APUUZWE BURE KABISA~•

Nilisema hili kipindi mnaishambulia serikali kuhusu bandari
Hawa jamaa wanataka kuleta mpasuko nchini
 
Back
Top Bottom