KWELI Dan Friedkin ana hifadhi ya ardhi kubwa Tanzania

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Huwa ninasema kila siku haijawahi kutokea mzungu kumpenda mwafrika hata siku moja. Huu tunaoita uhisani ni njia ya kupita tu kuchukua wanachokitaka katika ardhi ya Afrika.

Hakuna msaada anaopata mwafrika kwa mzungu zaidi ya maumivu.

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kila siku mnasema tuna mapori yapo yapo tu kumbe yamenunuliwa
Ni sawa tu kama mtu mweusi anamkatalia mweusi mwenzake kujenga kanyumba kwao kisa aliukana uraia ila mzungu anapewa ardhi yote hiyo kisa eti anawasaidia kuweka mazingira Safi

Kweli tuna akili za matope
Leo mzungu anakuambia naipenda Tanzania unachekelea
 
Umeambiwa amekodisha (lease) sijui unaelewa..?
 
Wote hao wanaomiliki mapori sijui ya akiba,sijui vitalu vya uwindaji,sijui misitu sijui Nini,sijui mashamba makubwa.Sijui mahotel makubwa mbugani au beach
Hawa wanufaika na mambo mengine kabisa tofaut na hayo waliyosajiliwa nayo ambayo ni kiini macho.
Kwa sababu sisi tumelala hatuna macho.
Hawa wanafanya
1.Wanachimba madini kwa Siri maporini huko madini mengi yapo mbugani.
2.Wanadili na hazina za kale zikiwemo sites na ishu za mercury ya miamba.
3.Madawa ya kulevya
4.Silaha za magendo,
Mizigo inatoroshewa kwenye airport hizo za porini kwa private charter au wanatumiaa submarine ndogo usiku zinaibukia kwenye meli zilizopo deep sea.
Eti mzungu anatoka ulaya anakuja kulima nyanya,sijui parachichi Morogoro.
Hizo hotel za mbugani au beach nyingi ni meeting place za kufanyia wao biashara.
Zipo hotel mswahili uingii au Bei kubwa asiyomudu mswahili.Hizo Bei ni geresha tu ili kulimits watu hasa watz wasiyagundue wayafanyayo.
 
aisee na tupo tu
 
Wazungu siyo washamba wakija huwa wanachunguza maeneo huwenda waligundua eneo hilo lina utajiri hapo chini
Kwa hiyo baadae utasikia ile mikataba ya nchi kupata asilimia 0.4 ya faida itakayopatikana

Aliye tuloga
 
Ahsante kwa taarifa. mnajitahidi kuuzima mjadala wa bandari...
Mjadala wa bandari umekaa vibaya sana hauzimiki kirahisi kwasababu hata hao wanao usifia mchana usiku ndio wanao chochea kuni.

Meki ma wodi.
 
Mwiba Holdings Company ya American Billionaire aitwaye Dan Friedkin anamiliki 6 milion acres (24,281 km square) katika Hifadhi za Taifa Magharibi mwa Ngorongoro na Kusini mwa Manyaroa National park ambako ni njia na wanyama wa kuhama yaani pofo, punda milia etc.

Ukubwa wa Tanzania in 945,000 km square.
Piga hesabu, 24,281/945,087X100 = 3% approx.

Kwa hivyo, Mr. Dan Friedkin anamiliki 3% ya ardhi bora ya Tanzania. Huyu ni mtu mmoja tu, je hao wengine na makampuni yao ni vipi.....

Ifike mahali Tanzanians tuhoji accountability ya ARDHI yetu. Ni kiasi gani ardhi yetu SALAMA, iko leased, sold na kwa mpango upi na faida gani.

Tunamtaka Controller and Auditor General (CAG) atupatie audited data za ardhi yetu kwa ripoti itakayotoka next time. CAG asiishie tu kukagua ofisi za serikali kwa mambo madogomadogo wakati ardhi imekwishauzwa na kuna siku tutakuja kutimuliwa na wenye ardhi.

Wamasai walikwishafukuzwa, huu ni mfano bora na wa uhakika.

NAWASILISHA.
 
Ulikuwa hujui?
 
Hatuna viongozi tunamadalali
 
hivi ni kweli huyu mzungu kapewa hii ardhi wakati sisi wengine hapa hapa tunaitafuta hiyo ardhi hatupewi? mwezetu amewapa nini au ametumia njia zipi? na anawekeza kitu gani na kwa masharti yepi?
 
Nilikuwa namsikia Lissu anazungumzia hii issue, kumbe kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…