Dancing ingelipa kiasi hiki basi Moze Iyobo na Angel Nyigu wangekuwa mabilionea

Dancing ingelipa kiasi hiki basi Moze Iyobo na Angel Nyigu wangekuwa mabilionea

kuna mtu hapa duniani anahitaji hela kidogo tu awaonyeshe watu maajabu.

chino kapata hio fursa mtashangaa sana Kwani hafanyi vile mlivyo zoea

kuna mtu anahitaji elfu hamsini tu afanye makubwa na bado inamsumbua kuipata wakati wewe unayo na hujui uifanyie nini

umeelewa wewe kiazi?
Kiazi sijaelewa 😀 Kina dully, makomando, msami, belle9 walikosa elfu 50 tu mpaka leo?
 
Hatukatai ni ndogo, ila ni ndogo kwa mtu gani? Kwa mwanasiasa kama Msukuma ni ndogo sana, kwa wafanyabiashara kina vunjabei, Davidsports wear, Jose madini, au wachezaji kina Mayele, Aziz ki n.k ambao shughuli zao zinajulikana, mbona kuna dancers wamepiga show kama kina Msami, makomandoo, sijui Fm acadèmia?au wasanii wanaoimba na kupiga show kama kina Zuchu, maua samma,mrisho mpoto n.k ? Au show za chino anapiga huko mambele super bowl, BET, grammy n.k?? Kama milioni 200 ndogo hao kina kontawa wa dungamawe wangekuwa n pesa sana😀
acheni upuuzi million 200 hata kwa nani ni kubwa
 
Kweli unayosema, Lakini mbona wapo wengi waliopambana wakatoboa wanajulikana na wanapongezwa, kina Diamond, Harmonize, Rayvanny,Zuchu, au waigizaji na watangazaji kama kina Masanja (analima sana mpunga) Mpoki, Joti n.k Lakini kuna baadhi ya mafanikio yana ukakasi kidogo, mfano hao kina Chief Godlove (hajulikani anafanya shughuli gani) Chino nk.
Kila mwenye mafanikio yeye ndio anajua anakotoa hela. Wewe elewa ni dancer mengine muachie mwenyewe.
 
Nafikiri huyu kijana amepata hela nyingi kwa kina tulia ackson na viongozi wengine wa serikali kwenye shughuli zao alizotumbuiza.

Japo kiuwezo jamaa anauwezo mdogo sana wa dance na muziki sema bahati tu inamng'arisha zaidi, sikuizimziki sio kujua kuimba sana au kujua kucheza sana ni inategemea yani Kwahiyo kijana apiga mamillion kwa wakubwa wanchi ndio kama hivyo yani katoboa
Kwamba akina kukata mauno lwenye ziara ya tulia hapa Mbeya anapewa pesa nyingi hivyo?

Acha uzwazwa dogo Nifahamuvyo, usiamini sana picha za watu wanazoweka nitandaoni. Nyingi wanaenda kupigia kwa watu ili wajidanganye na kuwadanganya maboya kama nyie.

Hana pesa yoyote huyo dogo, ni maskini mwenzako tu sawa na mimi muuza madafu na maisha hayapo hivyo.
 
Umezunguka sana, ila kinachokusumbua ni :

wivu

mtu asiyependa mwingine apate mafanikio; mtu mwenye kijicho

Hali iliyokufanya uwe na:

chuki

tabia ya kutopenda, hasa watu au ya kuwa na roho mbaya


Nb: Nipe uhusiano wa kufanya kazi muda mrefu na mafanikio. Mfano kuna mchezaji alicheza yanga miaka kumi iliyopita, halafu kuna mchezaji anacheza yanga mwaka wa tatu sasa.

Nb: Bado unaamini kuwa na umri mkubwa ndiyo mafanikio?? Linganisha dunia yako na dunia ya sasa, unaona ipi ina fursa zaidi?

Nb: Kuna nyakati huamua nini kifanyike coz ndiyo kinahitajika kwa wakati huo. Mfano Elon Musk na Mark Zuckerberg utajiri wao umepaa haraka sana kulingana na nyakati!
Kitu ambacho hata Mzee kikwete aliwahi hoji...."Ni pale watanzania wanapoona Kiongozi wa kawaida tu ila Mara baada ya kupata uongozi, anaanza kujikusanyia Mali ".

Hapa lazima wahoji.

Ukweli ni kua, Nyuma ya huyu Msanii Kuna utakatishaji mkubwa wa Pesa na Huenda nitakua sijakosea kua anajihusisha na biashara haramu.

Kwa aina ya muziki na dance ya hapa Bongo , HUWEZI KUA NA UKWASI MKUBWA NAMNA HIYO NDANI YA MUDA MFUPI HIVO

Sasa watu wanapohoji, msiwapige , Maisha unayoishi yanaonekana na yanapimika.
 
Tuache masikhara na maisha, watu wamecheza sana kiasi kwamba huyu anayejiita Chino kid hafiki hata nusu, hata akisema anaimba, watu wameimba sana, kina Jay melody, Ray vanny mwenyewe mpaka kufikia hapo ameshasota sana na hajapata mafanikio ya ghafla na haraka, amefanya mziki tukiwa tunamuona.

Sasa huyu chino hata ukiniuliza hit song yake hata moja sijui, hizo dancing labda anafanya huko background, sijui lakini najua kuna dancers wakali mno kumzidi yeye.Labxa anafanya biashara? Mbona hazijulikani?

Huu utajiri, Pesa, Mali, Majumba na magari ya kifahari na hana hata miaka mitano kwenye industry au hata akiwa nayo bado hajawa na impact yoyote ya kushtua, INATIA MASHAKA SANA 🤔🤔🤔
View attachment 3126070View attachment 3126072View attachment 3126073View attachment 3126074View attachment 3126075
Una uhakika izo mali anamiliki au kakodisha Mzee.
 
Back
Top Bottom