Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu unakuja baada ya kuwepo kwa mipango ya awali ya kujenga kiwanda hicho hapa nchini Tanzania, hatua ambayo inadaiwa kuibua mvutano wa kidiplomasia kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times (FT) la Uingereza, bilionea huyo ameweka wazi sababu za kubadili gia angani na kugeukia Mombasa badala ya mwambao wetu, jambo ambalo bila shaka litaibua mjadala mzito miongoni mwa wachumi na watunga sera hapa nchini.

Dangote.jpg


Mombasa badala ya Tanga: Nini Kimebadilika?​

Awali, jicho la Dangote lilikuwa katika ukanda wa Tanga, ili kuchukua fursa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalosafirisha mafuta kutoka Uganda. Hata hivyo, mwekezaji huyo raia wa Nigeria ameweka wazi hesabu zake mpya za kibiashara zinazompeleka jirani.

"Ninaamini zaidi upande wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa na yenye kina kirefu zaidi," alisema Dangote alipokuwa akilinganisha bandari ya Kenya na ya Tanga.

Mradi huu unakadiriwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani bilioni 15 hadi 17 (takriban Shilingi trilioni 38 hadi 43 za Kitanzania). Pamoja na uwezo wa bandari, Dangote anaona Kenya ina faida kubwa ya soko. "Wakenya ni watumiaji wakubwa. Ni uchumi mkubwa zaidi," aliongeza.

Dangote pia alibainisha kuwa mafuta ghafi yatatoka soko la wazi na yanaweza kusafirishwa kwa meli hadi kiwandani, hivyo hakuna ulazima wa kiwanda hicho kujengwa karibu na bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 linaloishia rasi ya Chongoleani, Tanga.

Kukerwa kwa Rais Samia kwa Ruto​

Uamuzi huu haujapita hivi hivi. Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kulalamika kwa hisia kali kwa Rais Ruto. Sababu ya msingi ya kukerwa kwa Rais Samia ni kitendo cha kutoshirikishwa kwenye makubaliano hayo mapya, hasa ikizingatiwa mpango wa awali ulikuwa wa kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania.

Masharti ya Dangote kwa Serikali ya Kenya​

"Mpira sasa upo mikononi mwa Rais Ruto," alisema Dangote. "Chochote atakachosema [Ruto] ndicho nitakachofanya."

Hata hivyo, ili mradi huu mkubwa uweze kutua Kenya, Dangote ameweka masharti makuu matatu. Kwanza, anahitaji Serikali ya Kenya itoe ardhi; pili, apatipatiwe ushirikiano wa kifedha kutoka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki; na tatu (ambalo ndilo muhimu zaidi kwake)—ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India.

"Hakuna kiwanda cha kusafisha mafuta duniani kinachoweza kudumu bila ulinzi huo wa kisera," alisisitiza Dangote, huku akiahidi kuwa, "Tukifikia makubaliano, tunaweza kuanza ujenzi mwaka huu."

Rais Ruto, kwa upande wake, amemmwagia sifa tele Dangote, akisema amethibitisha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujenga miradi yao wenyewe mikubwa bila kuwategemea wazungu.

Somo kutoka Nigeria: Mafanikio ya Kiwanda cha Lagos​

Kwa wanaohoji uwezo wa Dangote kutekeleza mradi huu, rekodi zake zinajieleza. Ahadi hii inakuja wakati bilionea huyo akiwa ametoka kukamilisha ujenzi wa kiwanda chake kingine kikubwa cha mafuta mjini Lagos, Nigeria, kilichogharimu Dola bilioni 20.

Kiwanda hicho kilijengwa kwa kipindi cha miaka 10, kikipinga dhana ya wakosoaji waliodhani asingejaribu kutatua changamoto ya nishati ambayo Serikali ya Nigeria ilishindwa kuitatua kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi duniani chenye mtambo mmoja wa uzalishaji (single-train refinery), kikichakata mapipa 650,000 kwa siku na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, hasa wakati huu ambapo usafirishaji wa nishati duniani unakabiliwa na changamoto kutokana na migogoro katika Mlango-bahari wa Hormuz.

Dangote amefanikiwa kuuza mafuta ya ndege (jet fuel) kwa faida kubwa kwa mashirika ya Ulaya, huku akilipa kipaumbele Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), ambalo ndilo kubwa zaidi barani Afrika.

Nini maana yake kwetu Tanzania?​

Utajiri wa Dangote—kutoka kwenye biashara ya chumvi, sukari, unga, saruji hadi sasa mafuta—umechangiwa pia na uwezo wake wa kushawishi serikali kumpa misamaha ya kodi, kipaumbele katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na kulinda biashara zake dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje. Sasa anapanga kuongeza uzalishaji maradufu Lagos kufikia mapipa milioni 1.4 kwa siku ndani ya miezi 30 ijayo, akijiweka bega kwa bega na kampuni kubwa duniani kama Reliance Industries ya bilionea wa India, Mukesh Ambani.

Kwa sisi Watanzania, hatua hii ni kengele ya kuamka (wake-up call). "Ni jukumu la Waafrika kuwekeza katika bara lao wenyewe. Kama hatutafanya sisi, nani mwingine atafanya?" alihoji Dangote.

Kwa upande wetu Wadau:
Je, Tanzania tumekosa fursa hii adhimu kutokana na mapungufu ya miundombinu yetu ya Tanga kama inavyodaiwa, urasimu wetu wa ndani, au ni janja za kidiplomasia ambazo wenzetu wa Kenya wamezicheza vyema zaidi kibiashara?

Karibuni kwa mjadala.
 
Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote anapanga kutazama Kenya kama eneo la kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta chenye uwezo wa kubeba mapipa 650,000 kwa siku katika Afrika Mashariki

Gazeti la Financial Times liliripoti Jumapili, likinukuu mahojiano naye. Katika mahojiano hayo Dangote alilinganisha bandari ya Mombasa na bandari ya Tanga ya Tanzania akisema
:
​
“Ninazidi kuelekeza zaidi Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa zaidi na yenye kina kirefu."
–
Aliko Dangote

​
Ripoti hiyo inakuja baada ya Rais wa Kenya William Ruto kusema mwezi uliopita kwamba nchi za Afrika Mashariki zilikuwa zikijadili mipango ya kujenga kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta katika bandari ya Tanga nchini Tanzania, mradi ambao unafanana na ule wa Nigeria wa Dangote.
​
“Wakenya wanatumia zaidi mafuta. Uchumi wake ni mkubwa zaidi. Mpira uko mikononi mwa Rais Ruto, Chochote ambacho Rais Ruto atasema, ndicho nitakachofanya."
—
Aliko Dangote
​

Dangote alikadiria kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu kati ya dola bilioni 15 hadi 17, kulingana na ripoti ya FT.

Nilisema kuwa Kenya wanatuzidi kwenye diplomasia ya uchumi wengi wakakataa.​
 
Ingekuwa ni mimi chap kwa haraka, ningekutana na Dr Rutto ili tuyaweke sawa na kuwa na msimamo mmoja. Ujue Dr Rutto ndiye ameshika kwenye mpini.....

Namuelewa Dangote kwani ni kweli kuwa, Kenya ipo mbali kiuchumi kulinganisha na sisi kwani hata makusanyo yake ya kodi yametupita mbali sana pamoja na kuwa na kiwango cha chini cha kodi ya VAT kuliko sisi (Kenya ni 16%)

Kenya hata shule zao za umma za Msingi na Sekondari wameshikilia ubora ule ule wa miaka ya 90, hivyo wanafunzi/wazazi wanaona fahari watoto wao kupangiwa shule ya umma......OGOPA NCHI ILIYOWEKEZA KWENYE ELIMU.....
 
Kama kujengwa ni Tanzania tu kwasasa katazama kina tu !!

lkn Makampuni makubwa yanatabia za bint bint sitaki nataka nyingi !!

kwaiyo Dangote yupo kwenye Siasa ya uchumi!!

lkn lengo lake kuja Tanzania sasa izm kwanza ajidai Mombasa kuna kile sijui kile!!

ili Serikali yetu ifanye kama kumvutia kwake kumbe nayeye ndio mpango wake!!

Serikali yetu inajua mpango wake!!

Ruto anatumika na Dangote Eneo la uwekazaji ni kubwa sana!
lazima Dangote aje yeye kama yeye sio kujidai kumtumia Ruto na Mombasa na kulipia media kudanganya watu.

Tanzania tunaweza kumvutia China kuwekeza kwenye Refinery

Mwacheni tu.
 
Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote anapanga kutazama Kenya kama eneo la kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta chenye uwezo wa kubeba mapipa 650,000 kwa siku katika Afrika Mashariki

Gazeti la Financial Times liliripoti Jumapili, likinukuu mahojiano naye. Katika mahojiano hayo Dangote alilinganisha bandari ya Mombasa na bandari ya Tanga ya Tanzania akisema
:
​
“Ninazidi kuelekeza zaidi Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa zaidi na yenye kina kirefu
–
Aliko Dangote

​
Ripoti hiyo inakuja baada ya Rais wa Kenya William Ruto kusema mwezi uliopita kwamba nchi za Afrika Mashariki zilikuwa zikijadili mipango ya kujenga kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta katika bandari ya Tanga nchini Tanzania, mradi ambao unafanana na ule wa Nigeria wa Dangote.
​
“Wakenya wanatumia zaidi mafuta. Uchumi wake ni mkubwa zaidi. Mpira uko mikononi mwa Rais Ruto, Chochote ambacho Rais Ruto atasema, ndicho nitakachofanya."
—
Aliko Dangote
​

Dangote alikadiria kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu kati ya dola bilioni 15 hadi 17, kulingana na ripoti ya FT.

Nilisema kuwa Kenya wanatuzidi kwenye diplomasia ya uchumi wengi wakakataa.​
Viongozi wapumbavu waislamu ndiyo tatizo ..japo kwenye ili nadhani ujenzi ni tanga kwa sababu ya bomba la mafuta ya Uganda
 
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga k

Karibuni kwa mjadala.

Ukiona hivyo basi Mu7 akachomoa betri...Mzee wa watu kaona hataki kuwauza waganda kimya kimya, anataka hiyo refinery ijengwe Uganda
 
Kenya hawatuzidi diplomasia ya uchumi bali kilichotumika ni kilekile kinachofanywa kwenye makoloni ya magharibi.

Dangote ni mtu wao, Kenya ni koloni lao lisilofurukuta hivyo Tanzania tunawekwa pembeni kwa mtindo huo hapo mwelekeo wa dunia kwa sasa huu ujinga utakoma
 
Tanzania tunaweza kumvutia China kuwekeza kwenye Refinery
Sahihi, Tanzania na Uganda wamtetemeshe kwa kutafuta mwekezaji mwingine. Hata refinery yake ya Nigeria mkandarasi mkuu alikuwa ni kampuni ya China, CNCEC

Na walimtumia Mchina kwa sababu mataifa ya Magharibi hayakuwa tayari kuona Afrika inamiliki refinery kubwa.

Wao Magharibi walikuwa wanataka mafuta ghafi yatoke Nigeria yaende kwao yasafishwe yarudi kuuzwa tena Nigeria/Afrika

Nchi kadhaa za Afrika kwa sasa zimeamua kutumia makampuni ya Kichina inapohusu masuala ya nishati kupunguza bureaucracy za Magharibi na mashirika yao ya kifedha kama IMF na WB

Na yeye tumfanyie kama alichowafanyia Wazungu kule Nigeria. The game is brutal but still fair
​
 
Wakenya wanapenyeza fitina.ila bado sisi tunayo karata . Hapa ndo pa kuchangamka sasa
Wanapenyeza Fitina Wapi? Ninyi Bandari ya Tanga Mliwauzia waarabu kwa miaka 100. Mwaarabu anataka bandari ya Tanga iwe ya kushusha Mafuta yake biashara yake ikue sio kupakia mafuta.

DP World si mlikuwa mnawatetea? Endeleeni sasa.

Mwarabu Kakataa
 
Ingekuwa ni mimi chap kwa haraka, ningekutana na Dr Rutto ili tuyaweke sawa na kuwa na msimamo mmoja. Ujue Dr Rutto ndiye ameshika kwenye mpini.....

Namuelewa Dangote kwani ni kweli kuwa, Kenya ipo mbali kiuchumi kulinganisha na sisi kwani hata makusanyo yake ya kodi yametupita mbali sana pamoja na kuwa na kiwango cha chini cha kodi ya VAT kuliko sisi (Kenya ni 16%)

Kenya hata shule zao za umma za Msingi na Sekondari, wameshikilia ubora ule ule wa miaka ya 90, hivyo wanafunzi/wazazi wanaona fahari watoto wao kupangiwa shule ya umma.... Kwenda private ni kwa wale waliokosa nafasi....
Unadhalilidha SHYTON.

Punguza kukaa porini, upate akili.
 
Tanzania too much talking,action zero,alisumbuliwa sana kupata gesi kule kusini
 
Back
Top Bottom