Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Katiba chakavu ndio chanzo cha haya yote.....ni sawa na kuvaa shati lililopauka wakati uwezo wa kununua shati jipya unao
 
Gullible East Africans kupenda kujadili mambo kiwepesi. All there is at best kwenye hii refinery saga is politics. Ruto inaonekana anatafuta political mileage Kenya; na mafuta labda ni sensitive issue kwa sasa ndio msingi wa hii suddenly refinery project.

Sidhani kama project kama hiyo inatoka kuwa concept week mbili nyuma na kuwa investment decisions leo (it takes a lot of planning). Wakati hii refinery ya EAC hata huyo mwenyeji (Tanzania) hakuwa na habari ingeenda jengwa Tanga na yeye kaona tu kama wengine mitandaoni.

On the initial discussion day lilipoibuka swala la refinery; moja ya concern za Dangote ilikuwa source of stock feed; nchi zinazotajwa DRC, South Sudan na Uganda. DRC hata thoroughly exploration aijafanyika bado let kuanza kuuza crude, South Sudan uwezo wao wa kump mafuta kwa siku ni chini 80,000 kwa siku. Uganda uwezo wake ni 225000 barrels.

Sasa muulize huyo Dangote mwenyewe huko kwao kama anapata stock feed yote kutoka Nigeria? Jibu hapana kwao wana pump almost 1.4 million barrel kwa siku na wamiliki wa vitalu kwa umoja wao can only give him 250,000 crude per day. Wachimbaji wana masoko yao ya kupeleka crude pia nje ya Nigeria. Matokeo yake Dangote almost 60% ya stock feed ya refinery yake anaagiza nje ya nchi.

He is not stupid (Dangote) keshajifunza changamoto za kupata inventory ya mafuta. Kweli we unaamini Total hawana soko lao na mafuta ya Uganda, South Sudan hawana soko lao (achilia mbali political instability), DRC hakuna hata investments za kutoa mafuta from ground nor clear understanding of the reserves amount. Bado East Congo kwenye mafuta kuna political instability halafu mtu anakwambia anajenga refinery inventory itatoka huko.

Ni hivi seriousness ya EAC refinery haiwezi fanyika jukwaani kirahisi vile; Ruto anauchaguzi karibu Kenya ndio msingi wa hizi hadithi za refinery it’s all politics.
Dangote ni mfanyi biashara hajishukuliki na siasa...amejenga refinery kwao na ameona faida kubwa sana katokana na huo refinery. Amefanya hesabu zake na ameona kunafaidi kubwa akijenga afrika mashariki
 
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu unakuja baada ya kuwepo kwa mipango ya awali ya kujenga kiwanda hicho hapa nchini Tanzania, hatua ambayo inadaiwa kuibua mvutano wa kidiplomasia kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times (FT) la Uingereza, bilionea huyo ameweka wazi sababu za kubadili gia angani na kugeukia Mombasa badala ya mwambao wetu, jambo ambalo bila shaka litaibua mjadala mzito miongoni mwa wachumi na watunga sera hapa nchini.

View attachment 3586367

Mombasa badala ya Tanga: Nini Kimebadilika?​

Awali, jicho la Dangote lilikuwa katika ukanda wa Tanga, ili kuchukua fursa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalosafirisha mafuta kutoka Uganda. Hata hivyo, mwekezaji huyo raia wa Nigeria ameweka wazi hesabu zake mpya za kibiashara zinazompeleka jirani.

"Ninaamini zaidi upande wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa na yenye kina kirefu zaidi," alisema Dangote alipokuwa akilinganisha bandari ya Kenya na ya Tanga.

Mradi huu unakadiriwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani bilioni 15 hadi 17 (takriban Shilingi trilioni 38 hadi 43 za Kitanzania). Pamoja na uwezo wa bandari, Dangote anaona Kenya ina faida kubwa ya soko. "Wakenya ni watumiaji wakubwa. Ni uchumi mkubwa zaidi," aliongeza.

Dangote pia alibainisha kuwa mafuta ghafi yatatoka soko la wazi na yanaweza kusafirishwa kwa meli hadi kiwandani, hivyo hakuna ulazima wa kiwanda hicho kujengwa karibu na bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 linaloishia rasi ya Chongoleani, Tanga.

Kukerwa kwa Rais Samia kwa Ruto​

Uamuzi huu haujapita hivi hivi. Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kulalamika kwa hisia kali kwa Rais Ruto. Sababu ya msingi ya kukerwa kwa Rais Samia ni kitendo cha kutoshirikishwa kwenye makubaliano hayo mapya, hasa ikizingatiwa mpango wa awali ulikuwa wa kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania.

Masharti ya Dangote kwa Serikali ya Kenya​

"Mpira sasa upo mikononi mwa Rais Ruto," alisema Dangote. "Chochote atakachosema [Ruto] ndicho nitakachofanya."

Hata hivyo, ili mradi huu mkubwa uweze kutua Kenya, Dangote ameweka masharti makuu matatu. Kwanza, anahitaji Serikali ya Kenya itoe ardhi; pili, apatipatiwe ushirikiano wa kifedha kutoka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki; na tatu (ambalo ndilo muhimu zaidi kwake)—ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India.

"Hakuna kiwanda cha kusafisha mafuta duniani kinachoweza kudumu bila ulinzi huo wa kisera," alisisitiza Dangote, huku akiahidi kuwa, "Tukifikia makubaliano, tunaweza kuanza ujenzi mwaka huu."

Rais Ruto, kwa upande wake, amemmwagia sifa tele Dangote, akisema amethibitisha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujenga miradi yao wenyewe mikubwa bila kuwategemea wazungu.

Somo kutoka Nigeria: Mafanikio ya Kiwanda cha Lagos​

Kwa wanaohoji uwezo wa Dangote kutekeleza mradi huu, rekodi zake zinajieleza. Ahadi hii inakuja wakati bilionea huyo akiwa ametoka kukamilisha ujenzi wa kiwanda chake kingine kikubwa cha mafuta mjini Lagos, Nigeria, kilichogharimu Dola bilioni 20.

Kiwanda hicho kilijengwa kwa kipindi cha miaka 10, kikipinga dhana ya wakosoaji waliodhani asingejaribu kutatua changamoto ya nishati ambayo Serikali ya Nigeria ilishindwa kuitatua kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi duniani chenye mtambo mmoja wa uzalishaji (single-train refinery), kikichakata mapipa 650,000 kwa siku na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, hasa wakati huu ambapo usafirishaji wa nishati duniani unakabiliwa na changamoto kutokana na migogoro katika Mlango-bahari wa Hormuz.

Dangote amefanikiwa kuuza mafuta ya ndege (jet fuel) kwa faida kubwa kwa mashirika ya Ulaya, huku akilipa kipaumbele Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), ambalo ndilo kubwa zaidi barani Afrika.

Nini maana yake kwetu Tanzania?​

Utajiri wa Dangote—kutoka kwenye biashara ya chumvi, sukari, unga, saruji hadi sasa mafuta—umechangiwa pia na uwezo wake wa kushawishi serikali kumpa misamaha ya kodi, kipaumbele katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na kulinda biashara zake dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje. Sasa anapanga kuongeza uzalishaji maradufu Lagos kufikia mapipa milioni 1.4 kwa siku ndani ya miezi 30 ijayo, akijiweka bega kwa bega na kampuni kubwa duniani kama Reliance Industries ya bilionea wa India, Mukesh Ambani.

Kwa sisi Watanzania, hatua hii ni kengele ya kuamka (wake-up call). "Ni jukumu la Waafrika kuwekeza katika bara lao wenyewe. Kama hatutafanya sisi, nani mwingine atafanya?" alihoji Dangote.

Kwa upande wetu Wadau:
Je, Tanzania tumekosa fursa hii adhimu kutokana na mapungufu ya miundombinu yetu ya Tanga kama inavyodaiwa, urasimu wetu wa ndani, au ni janja za kidiplomasia ambazo wenzetu wa Kenya wamezicheza vyema zaidi kibiashara?

Karibuni kwa mjadala.
Mimi naombeni kuuliza tu mwenye hilo bomba ni total sasa wao ndio wawekeza hapo je watakubali kuwekewa hizo refinery sijui za kusafisha mafuta?
 
Kujengwa kwa refinery Mombasa hainamaanishi mafuta lazima itoke Uganda bali itanunuliwa kutoka soko ya dunia mahali bei iko chini. Mafuta ya Uganda kusafirishwa kw bomba la EACOP hadi Tanga itagharimu $12 kwa pipa na kutoka ughaibuni hadi mombasa ni $2. Tayari kuna shida kwa bei
 
Kwani Tanzania haiwezi kujenga kama nchi, tulikuwa na refinery kigamboni Tipper sio lazima kumtegemea Dangote.
Anataka ulinzi wa nini huu ni wakati wa soko huria.
 
Refinery ya Lagos inatoa mafuta yake kwa wingi kutoka US....
Nigeria ni Oil producer hawajampa mzawa? Kweli aisee nigeria ina extract 1.4million-18m barrels per day na refinery yake ina capacity ya kuchakata 650,000 barrels per day bado anachukua US and other suppliers!
IMG_2196.jpeg
 
Back
Top Bottom