Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Wakenya wanapenyeza fitina.ila bado sisi tunayo karata . Hapa ndo pa kuchangamka sasa
Unafiki wako fitina gani wakati rais kwa kinywa chake alitamka kukerwa na akamtaka rais wa kenya ajieleze hadharan, wenzetu wako busy kuimarisha uchumi wao sisi huku tu awaza uchawa wa kumsifia mama muda wote, bure kabisa
 
Wakenya wanapenyeza fitina.ila bado sisi tunayo karata . Hapa ndo pa kuchangamka sasa
Biashara haziendeshwi kwa majungu na porojo. Dangote anaangalia nani mwenye soko la ndani kubwa zaidi ili apate wateja wa kuanzia, na nani ana bandari yenye kina kirefu zaidi na yenye uwezo mkubwa wa kushusha na kupakia.
 
Viongozi wapumbavu waislamu ndiyo tatizo ..japo kwenye ili nadhani ujenzi ni tanga kwa sababu ya bomba la mafuta ya Uganda
Upumbavu ulianzishwa na Baba yenu mkristo Laanatullahi Nyerere, haya ni matunda ya mti alioupanda CCM
 
Mkenya ana taka bomba lingine liingia kenya Tanga to mombasa sio
 
Hakuna mtu hasa mgeni mwenye akili timamu anaweza wekeza trillions kwenye nchi ambayo, mahakama inaweza tuu kupelekewa kimemo haki isipatikane.
Mahakama za kibiashara bongo, ubabaishaji, arbitration mbovu sana.
Bongo kupoteza mtaji kwa kudhulimiwa au utapeli ni dakika sifuri tuu.
 
Popote refinery itakapojengwa itapata malighafi. Singapore, India na nchi nyingi za Ulaya wana refineries kubwa kuliko na hawana mafuta. Dangote atakachonufaika nacho zaidi kwa Tanzania labda ni ardhi ya bure.
Hata upatikanaji wa karibu wa malighafi ni faida kwake.
 
Tanzania Petroleum Professionals Board (TPPB)

Pamoja na hoja zinazotolewa kuhusu Port of Mombasa na ukubwa wa soko la Kenya, bado zipo sababu nyingi za msingi zinazoweza kuifanya Tanzania kuwa strategically attractive zaidi kwa refinery na petrochemical investments za muda mrefu.

Kwanza, East African Crude Oil Pipeline ni infrastructure kubwa sana ambayo tayari inaifanya Tanzania kuwa official crude oil export corridor ya Afrika Mashariki. Hii ni strategic advantage ambayo si rahisi kuipuuza katika long-term refinery na petrochemical planning. Uwepo wa crude export infrastructure karibu na Tanga unaweza kupunguza baadhi ya logistics complexities zinazoweza kujitokeza kwenye crude sourcing na storage integration hapo baadaye.

Pili, Tanzania ina eneo kubwa zaidi la maendeleo ya viwanda na industrial expansion ukilinganisha na pressure kubwa ya urban congestion inayoongezeka Mombasa. Kwa miradi mikubwa ya refinery na petrochemicals, availability ya large industrial land ni jambo muhimu sana kwa sababu miradi hiyo huhitaji:
  • storage farms,
  • petrochemical complexes,
  • pipelines,
  • export terminals,
  • power systems,
  • pamoja na future expansion corridors.
Ukanda wa Tanga bado una nafasi kubwa sana ya kujengwa integrated energy-industrial ecosystem kwa muda mrefu.

Tatu, Tanzania ina natural gas reserves kubwa sana ambazo zinaweza kuwa major competitive advantage kwenye future integrated refinery-petrochemical-gas industrial system. Dunia ya energy industry sasa inaelekea zaidi kwenye integration kati ya:
  • refinery,
  • gas processing,
  • petrochemicals,
  • LNG,
  • fertilizers,
  • methanol,
  • na hydrogen-related industries.
Katika eneo hilo, Tanzania ina strategic energy resources ambazo zinaweza kuongeza long-term competitiveness zaidi kuliko kutegemea refinery pekee.

Nne, Tanzania kijiografia ipo kwenye nafasi nzuri sana kwa regional exports kwenda:
  • Zambia,
  • DRC,
  • Rwanda,
  • Burundi,
  • Malawi,
  • Uganda,
  • pamoja na Southern Africa kupitia Indian Ocean corridor.
Kwa hiyo refinery au petrochemical hub ya Tanzania inaweza kutengeneza faida kubwa kupitia regional energy trade na transit logistics kwa muda mrefu.

Tano, bandari ya Tanga bado ina nafasi kubwa ya kupanuliwa zaidi kwa future energy infrastructure development tofauti na baadhi ya mature ports ambazo tayari zina congestion kubwa na operational pressure. Katika mega energy projects, uwezo wa future expansion ni jambo muhimu sana kwa investors wanaofikiria miaka 30 hadi 50 ijayo.

Muhimu zaidi, investors wengi wa energy industry huangalia stability ya muda mrefu kuliko excitement ya muda mfupi wa soko. Tanzania bado inaonekana kuwa moja ya nchi zenye:
  • strategic geographic positioning,
  • growing energy demand,
  • na large-scale industrial potential ndani ya Afrika Mashariki.
Kwa hiyo, hata kama Kenya inaweza kuwa na baadhi ya short-term commercial advantages kwenye marine petroleum trading ecosystem, bado Tanzania ina strong long-term strategic advantages ambazo zinaweza kuifanya kuwa attractive zaidi kwa refinery, petrochemical, LNG, na integrated industrial investments za baadaye.
 
Wakenya wanapenyeza fitina.ila bado sisi tunayo karata . Hapa ndo pa kuchangamka sasa
Kenyans are business oriented, ujamaa umewafanya kuwa bongolala. Biashara ni vita, mikakati, aggressiveness na fitna pia. Magufuli na uzezeta wake vita alivyopigana bomba la mafuta kupita TZ hadi bandarini Tanga angekuwa ni Samia(Mwajuma nchokonoe) hata bomba lingepita Kenya, akili(kama anazo) ameshikiwa na Waomani.
 
Kenya hawatuzidi diplomasia ya uchumi bali kilichotumika ni kilekile kinachofanywa kwenye makoloni ya magharibi.

Dangote ni mtu wao, Kenya ni koloni lao lisilofurukuta hivyo Tanzania tunawekwa pembeni kwa mtindo huo hapo mwelekeo wa dunia kwa sasa huu ujinga utakoma
Nyie chura wenu anatembelewa na rais badala ya aelezee changamoto za kiuchumi zinazowakabili na jinsi ya kuzitatua yeye anaongelea kupiga watu
 
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu unakuja baada ya kuwepo kwa mipango ya awali ya kujenga kiwanda hicho hapa nchini Tanzania, hatua ambayo inadaiwa kuibua mvutano wa kidiplomasia kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times (FT) la Uingereza, bilionea huyo ameweka wazi sababu za kubadili gia angani na kugeukia Mombasa badala ya mwambao wetu, jambo ambalo bila shaka litaibua mjadala mzito miongoni mwa wachumi na watunga sera hapa nchini.

View attachment 3586367

Mombasa badala ya Tanga: Nini Kimebadilika?​

Awali, jicho la Dangote lilikuwa katika ukanda wa Tanga, ili kuchukua fursa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalosafirisha mafuta kutoka Uganda. Hata hivyo, mwekezaji huyo raia wa Nigeria ameweka wazi hesabu zake mpya za kibiashara zinazompeleka jirani.

"Ninaamini zaidi upande wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa na yenye kina kirefu zaidi," alisema Dangote alipokuwa akilinganisha bandari ya Kenya na ya Tanga.

Mradi huu unakadiriwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani bilioni 15 hadi 17 (takriban Shilingi trilioni 38 hadi 43 za Kitanzania). Pamoja na uwezo wa bandari, Dangote anaona Kenya ina faida kubwa ya soko. "Wakenya ni watumiaji wakubwa. Ni uchumi mkubwa zaidi," aliongeza.

Dangote pia alibainisha kuwa mafuta ghafi yatatoka soko la wazi na yanaweza kusafirishwa kwa meli hadi kiwandani, hivyo hakuna ulazima wa kiwanda hicho kujengwa karibu na bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 linaloishia rasi ya Chongoleani, Tanga.

Kukerwa kwa Rais Samia kwa Ruto​

Uamuzi huu haujapita hivi hivi. Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kulalamika kwa hisia kali kwa Rais Ruto. Sababu ya msingi ya kukerwa kwa Rais Samia ni kitendo cha kutoshirikishwa kwenye makubaliano hayo mapya, hasa ikizingatiwa mpango wa awali ulikuwa wa kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania.

Masharti ya Dangote kwa Serikali ya Kenya​

"Mpira sasa upo mikononi mwa Rais Ruto," alisema Dangote. "Chochote atakachosema [Ruto] ndicho nitakachofanya."

Hata hivyo, ili mradi huu mkubwa uweze kutua Kenya, Dangote ameweka masharti makuu matatu. Kwanza, anahitaji Serikali ya Kenya itoe ardhi; pili, apatipatiwe ushirikiano wa kifedha kutoka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki; na tatu (ambalo ndilo muhimu zaidi kwake)—ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India.

"Hakuna kiwanda cha kusafisha mafuta duniani kinachoweza kudumu bila ulinzi huo wa kisera," alisisitiza Dangote, huku akiahidi kuwa, "Tukifikia makubaliano, tunaweza kuanza ujenzi mwaka huu."

Rais Ruto, kwa upande wake, amemmwagia sifa tele Dangote, akisema amethibitisha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujenga miradi yao wenyewe mikubwa bila kuwategemea wazungu.

Somo kutoka Nigeria: Mafanikio ya Kiwanda cha Lagos​

Kwa wanaohoji uwezo wa Dangote kutekeleza mradi huu, rekodi zake zinajieleza. Ahadi hii inakuja wakati bilionea huyo akiwa ametoka kukamilisha ujenzi wa kiwanda chake kingine kikubwa cha mafuta mjini Lagos, Nigeria, kilichogharimu Dola bilioni 20.

Kiwanda hicho kilijengwa kwa kipindi cha miaka 10, kikipinga dhana ya wakosoaji waliodhani asingejaribu kutatua changamoto ya nishati ambayo Serikali ya Nigeria ilishindwa kuitatua kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi duniani chenye mtambo mmoja wa uzalishaji (single-train refinery), kikichakata mapipa 650,000 kwa siku na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, hasa wakati huu ambapo usafirishaji wa nishati duniani unakabiliwa na changamoto kutokana na migogoro katika Mlango-bahari wa Hormuz.

Dangote amefanikiwa kuuza mafuta ya ndege (jet fuel) kwa faida kubwa kwa mashirika ya Ulaya, huku akilipa kipaumbele Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), ambalo ndilo kubwa zaidi barani Afrika.

Nini maana yake kwetu Tanzania?​

Utajiri wa Dangote—kutoka kwenye biashara ya chumvi, sukari, unga, saruji hadi sasa mafuta—umechangiwa pia na uwezo wake wa kushawishi serikali kumpa misamaha ya kodi, kipaumbele katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na kulinda biashara zake dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje. Sasa anapanga kuongeza uzalishaji maradufu Lagos kufikia mapipa milioni 1.4 kwa siku ndani ya miezi 30 ijayo, akijiweka bega kwa bega na kampuni kubwa duniani kama Reliance Industries ya bilionea wa India, Mukesh Ambani.

Kwa sisi Watanzania, hatua hii ni kengele ya kuamka (wake-up call). "Ni jukumu la Waafrika kuwekeza katika bara lao wenyewe. Kama hatutafanya sisi, nani mwingine atafanya?" alihoji Dangote.

Kwa upande wetu Wadau:
Je, Tanzania tumekosa fursa hii adhimu kutokana na mapungufu ya miundombinu yetu ya Tanga kama inavyodaiwa, urasimu wetu wa ndani, au ni janja za kidiplomasia ambazo wenzetu wa Kenya wamezicheza vyema zaidi kibiashara?

Karibuni kwa mjadala.
Ruto ni akili kubwa na ana PhD ya darasani na siyo
Ya sagura sagura.
1. alijua kwamba bibi hakushirikishwa kwenye wazo la ujenzi wa hiyo refinery Tanga na
2. alijua kwamba akisema hivyo mbele ya bibi, bibi ataanza kubwabwaja, na
3. Na kweli, Ruto aliposema tu, bibi akajaa kwenye mfumo: Mara ooh mimi Sina taarifa, who are you na BLA BLA kibao
4. Ruto akachekelea akijua: game over!
5. Leo Financial times wameandika: Dangote kaamua kujenga kiwanda hicho Mombasa.
6. Somo la leo: mdomo uliponza kichwa
 
"ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India".

Hili sharti la kipumbavu sana. Dangote anapenda apate yeye tu hataki ushindani. Monopoly ndo sera yake. Hata huko Nigeria anasumbuana sana na serikali. Pia kusema anataka usaidizi wa kifedha ni sharti la kishenzi. Atafutwe mwekezaji mwingine asiye na masharti ya kijinga.

Pale Nigeria kiwanda chake kidogo kifungwe analeta uzawa uzawa mwingi kwenye mambo ya msingi kuna mengine yanaangukia kwenye Usalama wa nchi!!

Serikali yetu inajua Dangote ni m'Nigeria mjanja mjanja..

muhimu aje mwenyewe mezani yajengwe!

Serikali imeshajifunza kupitia kwao Nigeria!

Narudia Serikali ya Nigeria kidogo ikifunge kiwanda cha Dangote ❗️❗️

Dangote alitaka kilakitu adhibiti yeye!!!!
Wakamdhibiti yeye Hakuna kuagizo kitu!!!

Dangote akaanza kupiga kelele kupitia MEDIA za kimataifa!!

Janja janja hatutaki!!!
 
Tanzania Petroleum Professionals Board (TPPB)

Pamoja na hoja zinazotolewa kuhusu Port of Mombasa na ukubwa wa soko la Kenya, bado zipo sababu nyingi za msingi zinazoweza kuifanya Tanzania kuwa strategically attractive zaidi kwa refinery na petrochemical investments za muda mrefu.

Kwanza, East African Crude Oil Pipeline ni infrastructure kubwa sana ambayo tayari inaifanya Tanzania kuwa official crude oil export corridor ya Afrika Mashariki. Hii ni strategic advantage ambayo si rahisi kuipuuza katika long-term refinery na petrochemical planning. Uwepo wa crude export infrastructure karibu na Tanga unaweza kupunguza baadhi ya logistics complexities zinazoweza kujitokeza kwenye crude sourcing na storage integration hapo baadaye.

Pili, Tanzania ina eneo kubwa zaidi la maendeleo ya viwanda na industrial expansion ukilinganisha na pressure kubwa ya urban congestion inayoongezeka Mombasa. Kwa miradi mikubwa ya refinery na petrochemicals, availability ya large industrial land ni jambo muhimu sana kwa sababu miradi hiyo huhitaji:
  • storage farms,
  • petrochemical complexes,
  • pipelines,
  • export terminals,
  • power systems,
  • pamoja na future expansion corridors.
Ukanda wa Tanga bado una nafasi kubwa sana ya kujengwa integrated energy-industrial ecosystem kwa muda mrefu.

Tatu, Tanzania ina natural gas reserves kubwa sana ambazo zinaweza kuwa major competitive advantage kwenye future integrated refinery-petrochemical-gas industrial system. Dunia ya energy industry sasa inaelekea zaidi kwenye integration kati ya:
  • refinery,
  • gas processing,
  • petrochemicals,
  • LNG,
  • fertilizers,
  • methanol,
  • na hydrogen-related industries.
Katika eneo hilo, Tanzania ina strategic energy resources ambazo zinaweza kuongeza long-term competitiveness zaidi kuliko kutegemea refinery pekee.

Nne, Tanzania kijiografia ipo kwenye nafasi nzuri sana kwa regional exports kwenda:
  • Zambia,
  • DRC,
  • Rwanda,
  • Burundi,
  • Malawi,
  • Uganda,
  • pamoja na Southern Africa kupitia Indian Ocean corridor.
Kwa hiyo refinery au petrochemical hub ya Tanzania inaweza kutengeneza faida kubwa kupitia regional energy trade na transit logistics kwa muda mrefu.

Tano, bandari ya Tanga bado ina nafasi kubwa ya kupanuliwa zaidi kwa future energy infrastructure development tofauti na baadhi ya mature ports ambazo tayari zina congestion kubwa na operational pressure. Katika mega energy projects, uwezo wa future expansion ni jambo muhimu sana kwa investors wanaofikiria miaka 30 hadi 50 ijayo.

Muhimu zaidi, investors wengi wa energy industry huangalia stability ya muda mrefu kuliko excitement ya muda mfupi wa soko. Tanzania bado inaonekana kuwa moja ya nchi zenye:
  • strategic geographic positioning,
  • growing energy demand,
  • na large-scale industrial potential ndani ya Afrika Mashariki.
Kwa hiyo, hata kama Kenya inaweza kuwa na baadhi ya short-term commercial advantages kwenye marine petroleum trading ecosystem, bado Tanzania ina strong long-term strategic advantages ambazo zinaweza kuifanya kuwa attractive zaidi kwa refinery, petrochemical, LNG, na integrated industrial investments za baadaye.
Ok , kwanini mnatumia VPN.?
 
Ni kweli DP world wapo, lakini hawa waliokuja hapa ni affiliation ya majizi ya huku kwetu. Ndio maana mkataba ule huku kasaini rais, lakini kule sio mtawala wa UAE. Yaani serekali ya Dubai haijui lolote kuhusu huu mikataba, bali ni wa wafanya biashara wezi na viongozi wetu hasa Samia, Kikwete, Rostam nk. Huu utapeli ni kama ule mkataba wa Richmond.

Kama unaweza kuongea vizuri na Tulia Akson muulize alisimamia kitu gani kipitishwe bungeni. Maana ana hasira atafunguka mchezo wote wa nyuma ya pazia.
Hebu weka hizo Saini za muwekezaji kwenye mkataba tuone,muwe mnaacha uwongo walau mara moja moja, habari ya dp kuwekeza dar es salaam ilikua global,useme wenyewe hawajui?
Kabla ya DP palikua na kampuni gani hapo bandari na kwa miaka mingapi?
 
Biashara haziendeshwi kwa majungu na porojo. Dangote anaangalia nani mwenye soko la ndani kubwa zaidi ili apate wateja wa kuanzia, na nani ana bandari yenye kina kirefu zaidi na yenye uwezo mkubwa wa kushusha na kupakia.
Mkuu vipi umeamini Mombasa kuna kina kirefu kudhidi Tanga !!!!

TANGA na Mombasa ni mkondo m1.✅️
jiwe moja ✅️

vipi kule Kuwe na kina kirefu!!

Chunguza kwanza T14 Armata

kutunza heshima yako.


Siasa za uchumi hakuna kina kirefu Mombasa changa la kisiasa kwenye uchumi!

Yani lengo kujenga hoja kwamba kuwekeza Mombasa kuna kilee kizuri kwenu hakipo!!

Inaitwa Siasa ya kabla kuwekeza!! Dangote ataenda Uganda kumuomba mu7 baada ya Ruto kushindwa.

Mu7 atajidai kamuomba Dangote na kamwelewa. kuwekeza Tanga badala ya Mombasa!!! Mungu atupe punzi
nimekaaa pale!!!!

Tanzania tunatafutwa kwanjia ndevu tujae!!!

Bahari ya Mombasa ipo kwenye mgogoro na Somalia ✅️
 
Wakenya wanapenyeza fitina.ila bado sisi tunayo karata . Hapa ndo pa kuchangamka sasa
Kuchangamka na nani? Tunachojua ni kumnyanyasa Lissu, kuteka na kuua. Tulichopanda ndio hicho hicho tutakachovuna kumamakeh..
 
Kuna mengi ya kufikirika na kisha yakaleta dhana kadhaa, mfano...

1. Yamkini ameona ujanja/tamaa/rushwa kutoka kwa utawala wa Tanzania. Kuanzia yeye kupewa eneo, kibali cha ujenzi, percent n.k mfano labda wana mtandao na wao walitaka waweke pesa hapo watakatishe.

2. Political instability kwa miaka kadhaa ijayo ndani ya Tanzania. Ni dhahiri kuwa upepo wa kisiasa Tanzania haujakaa sawa.

3. William Ruto alipokuja Tz, Samia alimwambia kuwa awashughulikie ipasavyo upinzani. Yamkini mashirika makubwa ya kutetea haki za binadamu yameona hii ni taswira mbaya kwa Tanzania, so inapaswa kutengwa.

4. Hapa kuna dhana ya kiroho, huu utawala wa sasa Tanzania una mikono iliyojaa damu, sio rahisi kila wanachokishika kikaenda vyema.
Kweli kabisa. Yan wewe unaona kabisa Kuna deal la kunufaisha nchi kiuchumi, ajira, n.k,,matamshi unayotoa "chapa mikwaju" ...hata Mimi siwez kuja sehem kama hio kuwekeeza...dangote alichotumia ni chenga ya mwili hajaenda direct
 
Back
Top Bottom