Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

10 May 2026
Dangote shifts refinery plans toward Kenya
Speaking to the Financial Times, Dangote says Kenya’s larger port and stronger fuel demand give it an edge over Tanzania.

View: https://m.youtube.com/shorts/s_CQhxV7Gho
Africa's richest man, Dangote, proposes $17B refinery in Kenya despite Ruto's hopes for a regional joint project

  • The refinery would have a production capacity of 650,000 barrels per day and reduce reliance on imported petroleum products.
  • Aliko Dangote plans to build a $17 billion oil refinery in Mombasa, Kenya to address East Africa’s energy needs.
  • Mombasa is favored for its superior port infrastructure and Kenya's larger economy and higher refined product consumption.
  • Dangote's move shifts regional strategy away from a joint Tanzanian project, aiming to strengthen energy security and expand his business empire
The refinery, with a projected capacity of 650,000 barrels per day, aims to reduce the region's dependence on imported refined petroleum products, especially as ongoing geopolitical tensions expose vulnerabilities in the supply chain that currently accounts for most of its energy needs.
In an exclusive interview with The Financial Times, Dangote expressed his preference for Mombasa, Kenya’s coastal city, as the location for the facility, highlighting the port’s superior infrastructure. “I’m leaning more towards Mombasa because Mombasa has a much larger, deeper port,” Dangote said.
He also pointed out Kenya’s larger economy and higher consumption of refined products, further strengthening the case for Mombasa as a strategic location. “Kenyans consume more. It’s a bigger economy,” he added.

A Crucial Investment for East Africa​

The proposed refinery, estimated at $15 billion to $17 billion according to The Financial Times, would be one of the largest industrial investments in East Africa.
It would outshine Uganda's partnership with UAE-based Alpha MBM Investments, which is developing a $4 billion, 60,000-barrel-per-day refinery in Kabaale, Hoima District, aiming for operations between late 2029 and early 2030.
Currently, East and Central Africa has only one operational refinery, a stark contrast to regions such as South Africa, which has seven refineries, North Africa with 21, and West Africa with 14.
While the proposed refinery will not match Dangote’s 650,000-barrel-per-day facility in Lagos, Nigeria, which is expanding to 1.4 million barrels per day, surpassing India’s Jamnagar Refinery; it would still make a significant contribution to addressing the region’s escalating energy needs.

Regional Context: Tanga Proposal and Geopolitical Pressures​

The refinery proposal comes amidst ongoing discussions about a potential joint refinery in Tanga, Tanzania.
Previously, Dangote had committed to supporting the construction of an oil refinery in Tanzania, pledging that his group would take the lead and complete it within four to five years.
This regional refinery would process oil from neighboring countries, including Kenya, South Sudan, and Uganda

President William Ruto of Kenya confirmed these talks at the Africa We Build Summit in Nairobi in April.
“That refinery will process oil from the DRC, Kenya, South Sudan, and Uganda. We will then build a pipeline from Tanga to Mombasa, allowing finished products to move through infrastructure we jointly own with Uganda,” Ruto said.
However, Tanzania's President Samia Suluhu expressed surprise at the announcement, revealing that she had not been consulted about the project before President Ruto made it public.
Ironically, while Ruto had initially hoped for a collaborative, regional project, Dangote’s decision to focus solely on Kenya marks a significant shift in the regional energy strategy.
“The ball is in the hands of President Ruto,” Dangote said. “Whatever President Ruto says is what I’ll do,” he added.

Source : DW
 
10 May 2026
Dangote shifts refinery plans toward Kenya
Speaking to the Financial Times, Dangote says Kenya’s larger port and stronger fuel demand give it an edge over Tanzania
23 April 2026
DHAMBI YA UTAWALA ULIOTOTA DAMU ZA WATANZANIA

TUME YA JAJI CHANDE KUWASILISHA 'TAARIFA' YA UCHUNGUZI KWA RAIS APRILI 23

View: https://m.youtube.com/watch?v=mCZKqgGkiOI
Samia wenzie Museveni na Ruto walizungumzia mambo hayo ya refinery tarehe 23 April 2026 wakati yeye Sqmia anacheza sarakasi za kupokea hotuba ya jaji Chande kuhusu mauaji kabla, wakati na baada ya M029 2025.

Dhambi ya damu za watu zitamgaragaza Samia kiasi ya kushindwa kupata muda wa kushughulikia masuala ya nchi tofauti kama angepata ushindi wa kuingia Ikulu kupitia mchakato sahihi ulio wa haki, kidemokrasia na kikatiba wa kupata madaraka
 
Neno kuvuka mipaka ya nchi kupiga Watu Mikwaju lina maana pana na ni hatari kwa Wawekezaji, Wanaharakati na Jumuiya ya Kimataifa

View: https://m.youtube.com/watch?v=sYN-FCrYapU

Watoa waraka mzito kulaani matamshi ya hivi karibuni kuhusu kuwashughulikia raia wa Afrika ya Mashariki watakaotumia uhuru wao kupinga tawala

Hii inakuja baada ya Samia Hassan kuchagiza kuwa lazima kuwepo na mikono ya sheria ya serikali haramu inayoweza kuvuka mipaka ya nchi ili kuwashughulikia wale wanaotoa maoni, na akatumia neno kupiga mikwaju ambalo lina maana pana na ni hatari kwa uhuru, maisha na haki ya kuishi wamesema Wanaharakati Wa Afrika Mashariki wakisoma waraka wao mzito
 
Wapumbavu wazanzibar wanauchungu sana na NYERERE kwa sababu wanatamani kuongozwa na muarabu na mna abudu muarabu
Hizo ndizo fikra alizowatia Babu yenu mkristo Laanatullahi Nyerere na CCM yake , hulaumiki
 
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu unakuja baada ya kuwepo kwa mipango ya awali ya kujenga kiwanda hicho hapa nchini Tanzania, hatua ambayo inadaiwa kuibua mvutano wa kidiplomasia kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times (FT) la Uingereza, bilionea huyo ameweka wazi sababu za kubadili gia angani na kugeukia Mombasa badala ya mwambao wetu, jambo ambalo bila shaka litaibua mjadala mzito miongoni mwa wachumi na watunga sera hapa nchini.

View attachment 3586367

Mombasa badala ya Tanga: Nini Kimebadilika?​

Awali, jicho la Dangote lilikuwa katika ukanda wa Tanga, ili kuchukua fursa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalosafirisha mafuta kutoka Uganda. Hata hivyo, mwekezaji huyo raia wa Nigeria ameweka wazi hesabu zake mpya za kibiashara zinazompeleka jirani.

"Ninaamini zaidi upande wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa na yenye kina kirefu zaidi," alisema Dangote alipokuwa akilinganisha bandari ya Kenya na ya Tanga.

Mradi huu unakadiriwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani bilioni 15 hadi 17 (takriban Shilingi trilioni 38 hadi 43 za Kitanzania). Pamoja na uwezo wa bandari, Dangote anaona Kenya ina faida kubwa ya soko. "Wakenya ni watumiaji wakubwa. Ni uchumi mkubwa zaidi," aliongeza.

Dangote pia alibainisha kuwa mafuta ghafi yatatoka soko la wazi na yanaweza kusafirishwa kwa meli hadi kiwandani, hivyo hakuna ulazima wa kiwanda hicho kujengwa karibu na bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 linaloishia rasi ya Chongoleani, Tanga.

Kukerwa kwa Rais Samia kwa Ruto​

Uamuzi huu haujapita hivi hivi. Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kulalamika kwa hisia kali kwa Rais Ruto. Sababu ya msingi ya kukerwa kwa Rais Samia ni kitendo cha kutoshirikishwa kwenye makubaliano hayo mapya, hasa ikizingatiwa mpango wa awali ulikuwa wa kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania.

Masharti ya Dangote kwa Serikali ya Kenya​

"Mpira sasa upo mikononi mwa Rais Ruto," alisema Dangote. "Chochote atakachosema [Ruto] ndicho nitakachofanya."

Hata hivyo, ili mradi huu mkubwa uweze kutua Kenya, Dangote ameweka masharti makuu matatu. Kwanza, anahitaji Serikali ya Kenya itoe ardhi; pili, apatipatiwe ushirikiano wa kifedha kutoka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki; na tatu (ambalo ndilo muhimu zaidi kwake)—ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India.

"Hakuna kiwanda cha kusafisha mafuta duniani kinachoweza kudumu bila ulinzi huo wa kisera," alisisitiza Dangote, huku akiahidi kuwa, "Tukifikia makubaliano, tunaweza kuanza ujenzi mwaka huu."

Rais Ruto, kwa upande wake, amemmwagia sifa tele Dangote, akisema amethibitisha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujenga miradi yao wenyewe mikubwa bila kuwategemea wazungu.

Somo kutoka Nigeria: Mafanikio ya Kiwanda cha Lagos​

Kwa wanaohoji uwezo wa Dangote kutekeleza mradi huu, rekodi zake zinajieleza. Ahadi hii inakuja wakati bilionea huyo akiwa ametoka kukamilisha ujenzi wa kiwanda chake kingine kikubwa cha mafuta mjini Lagos, Nigeria, kilichogharimu Dola bilioni 20.

Kiwanda hicho kilijengwa kwa kipindi cha miaka 10, kikipinga dhana ya wakosoaji waliodhani asingejaribu kutatua changamoto ya nishati ambayo Serikali ya Nigeria ilishindwa kuitatua kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi duniani chenye mtambo mmoja wa uzalishaji (single-train refinery), kikichakata mapipa 650,000 kwa siku na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, hasa wakati huu ambapo usafirishaji wa nishati duniani unakabiliwa na changamoto kutokana na migogoro katika Mlango-bahari wa Hormuz.

Dangote amefanikiwa kuuza mafuta ya ndege (jet fuel) kwa faida kubwa kwa mashirika ya Ulaya, huku akilipa kipaumbele Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), ambalo ndilo kubwa zaidi barani Afrika.

Nini maana yake kwetu Tanzania?​

Utajiri wa Dangote—kutoka kwenye biashara ya chumvi, sukari, unga, saruji hadi sasa mafuta—umechangiwa pia na uwezo wake wa kushawishi serikali kumpa misamaha ya kodi, kipaumbele katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na kulinda biashara zake dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje. Sasa anapanga kuongeza uzalishaji maradufu Lagos kufikia mapipa milioni 1.4 kwa siku ndani ya miezi 30 ijayo, akijiweka bega kwa bega na kampuni kubwa duniani kama Reliance Industries ya bilionea wa India, Mukesh Ambani.

Kwa sisi Watanzania, hatua hii ni kengele ya kuamka (wake-up call). "Ni jukumu la Waafrika kuwekeza katika bara lao wenyewe. Kama hatutafanya sisi, nani mwingine atafanya?" alihoji Dangote.

Kwa upande wetu Wadau:
Je, Tanzania tumekosa fursa hii adhimu kutokana na mapungufu ya miundombinu yetu ya Tanga kama inavyodaiwa, urasimu wetu wa ndani, au ni janja za kidiplomasia ambazo wenzetu wa Kenya wamezicheza vyema zaidi kibiashara?

Karibuni kwa mjadala.
Ieleweke kwamba Toka Mwanzo Dangote alitaka kujenga Tanga na ndio maana kina Ruto walijua Hilo mapema Hadi wanafanya kutngaza Kwa shingi upande Ili wapate sifa za Kisiasa.

Sasa baada ya kuzodolewa walitumua Kila hila na juhudi kumshawishi bwana Dangote aende Mombasa na ndio kimetokea bila shaka kapewa incentives za kutosha.

Ieleweke kwamba Kenya ndio adui namba Moja wa Tanzania achana na porojo za mdomoni mwao.

Mwisho hatuna sababu ya kumlazimisha Mwekezaji yeyote Bali atakuja mwenyewe akiona inafaa.

Muelekeo wa Tzn ni matumizi ya gesi so in long ran Mafuta sio dili sana ila Mafuta tutanunua popote yatakapokuwa bei rahisi hata kama ni Kenya.
 
Kazi kwenu Tanzania na Uganda mtakubaliana na Dangote, Kenya ipewe shavu kwenye refinery?

Taifa ambalo halina hisa kwenye mradi wa EACOP na mlikataa bomba lisipite Mombasa bali Tanga
Hapo anaua soko la kiwanda la Uganda.
 
NAAMINI BADO REFINARY ITAJENGWA TANZANIA.

SABABU

1. UWEPO WA EACOP.
2. UPATIKANAJI RAISI WA ARTHI.
3.BANDARI YA TANGA.

IKIJENGWA MOMBASA.

CRUDE ITATOTOKA WAPI?
JE LITAJENGWA BOMBA JIPYA KUTOKA UGANDA?

NAAMNINI HAPA WANACHEZA MCHEZO ILI WAPATE MASHARTI NAFUU...

Dangote Group hawafanyi uamuzi kwa kuegemea Imani au uamuzi wa tamko la rais dikteta uchwara , bali sera endelevu sahihi zisizoathiriwa nani yupo ikulu zinazozingatia utawala wa sheria unaothibitisha kwa vitendo kulinda uwekezaji na pale kukiwepo changamoto mhimili wa mahakama huru unaweza kutoa maamuzi ya haki na kutoa usawa kwa wote bila kujali ni mwenyeji mzawa au mgeni
 
Mkuu vipi umeamini Mombasa kuna kina kirefu kudhidi Tanga !!!!

TANGA na Mombasa ni mkondo m1.✅️
jiwe moja ✅️

vipi kule Kuwe na kina kirefu!!

Chunguza kwanza T14 Armata

kutunza heshima yako.

Siasa za uchumi hakuna kina kirefu Mombasa changa la kisiasa kwenye uchumi!

Yani lengo kujenga hoja kwamba kuwekeza Mombasa kuna kilee kizuri kwenu hakipo!!

Inaitwa Siasa ya kabla kuwekeza!! Dangote ataenda Uganda kumuomba mu7 baada ya Ruto kushindwa.

Mu7 atajidai kamuomba Dangote na kamwelewa. kuwekeza Tanga badala ya Mombasa!!! Mungu atupe punzi
nimekaaa pale!!!!

Tanzania tunatafutwa kwanjia ndevu tujae!!!

Bahari ya Mombasa ipo kwenye mgogoro na Somalia ✅️
Mkuu hapo nimeandika mambo mawili, bandari ya kina kirefu na pili bandari yenye uwezo wa kupakia na kushusha mizigo haraka kwenye meli.
Bandari ya Tanga ni ndogo kwa Mombasa ambayo ni kubwa hata kuizidi ya Dar hivyo hata kama ingekuwa kina ni sawa au kirefu zaidi haina maana kuliko uwezo wa mizigo.

Hata hivyo Mombasa ina kina kikubwa kuliko ya Dar. Bandari ya Bagamoyo ndio ingekuwa na kina kirefu na bila entrance channel nyembamba kama ilivyo Dar.

Tukiachana na hoja nyingine, hii ni kweli sasa iwe inaathiri au lah nisijue kwa hapo juu ya wapi refinery ijengwe. Lakini bado ukija hoja nyingine ya matumizi, Kenya wanatumia mafuta zaidi yetu.
 
Ngote kashashtuka hawa waarabu nduguze mama wamewekeza sana watakuja mgeuka huko mbeleni
 
Kwenye Mkataba wa Hoima-Tanga imeandikwa itajengwa refinery Tanga sijui hiyo refinery ya Dangote itachakata mafuta kutoka wapi?
 
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu unakuja baada ya kuwepo kwa mipango ya awali ya kujenga kiwanda hicho hapa nchini Tanzania, hatua ambayo inadaiwa kuibua mvutano wa kidiplomasia kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Kenya, William Ruto.

Katika mahojiano maalum na gazeti la Financial Times (FT) la Uingereza, bilionea huyo ameweka wazi sababu za kubadili gia angani na kugeukia Mombasa badala ya mwambao wetu, jambo ambalo bila shaka litaibua mjadala mzito miongoni mwa wachumi na watunga sera hapa nchini.

View attachment 3586367

Mombasa badala ya Tanga: Nini Kimebadilika?​

Awali, jicho la Dangote lilikuwa katika ukanda wa Tanga, ili kuchukua fursa ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) linalosafirisha mafuta kutoka Uganda. Hata hivyo, mwekezaji huyo raia wa Nigeria ameweka wazi hesabu zake mpya za kibiashara zinazompeleka jirani.

"Ninaamini zaidi upande wa Mombasa kwa sababu Mombasa ina bandari kubwa na yenye kina kirefu zaidi," alisema Dangote alipokuwa akilinganisha bandari ya Kenya na ya Tanga.

Mradi huu unakadiriwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani bilioni 15 hadi 17 (takriban Shilingi trilioni 38 hadi 43 za Kitanzania). Pamoja na uwezo wa bandari, Dangote anaona Kenya ina faida kubwa ya soko. "Wakenya ni watumiaji wakubwa. Ni uchumi mkubwa zaidi," aliongeza.

Dangote pia alibainisha kuwa mafuta ghafi yatatoka soko la wazi na yanaweza kusafirishwa kwa meli hadi kiwandani, hivyo hakuna ulazima wa kiwanda hicho kujengwa karibu na bomba la EACOP lenye urefu wa kilomita 1,500 linaloishia rasi ya Chongoleani, Tanga.

Kukerwa kwa Rais Samia kwa Ruto​

Uamuzi huu haujapita hivi hivi. Wiki iliyopita, Rais Samia Suluhu Hassan alionekana kulalamika kwa hisia kali kwa Rais Ruto. Sababu ya msingi ya kukerwa kwa Rais Samia ni kitendo cha kutoshirikishwa kwenye makubaliano hayo mapya, hasa ikizingatiwa mpango wa awali ulikuwa wa kujenga kiwanda hicho nchini Tanzania.

Masharti ya Dangote kwa Serikali ya Kenya​

"Mpira sasa upo mikononi mwa Rais Ruto," alisema Dangote. "Chochote atakachosema [Ruto] ndicho nitakachofanya."

Hata hivyo, ili mradi huu mkubwa uweze kutua Kenya, Dangote ameweka masharti makuu matatu. Kwanza, anahitaji Serikali ya Kenya itoe ardhi; pili, apatipatiwe ushirikiano wa kifedha kutoka ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki; na tatu (ambalo ndilo muhimu zaidi kwake)—ulinzi wa soko lake dhidi ya uingizwaji holela wa nishati ya bei rahisi (dumping) kutoka mataifa kama Urusi na India.

"Hakuna kiwanda cha kusafisha mafuta duniani kinachoweza kudumu bila ulinzi huo wa kisera," alisisitiza Dangote, huku akiahidi kuwa, "Tukifikia makubaliano, tunaweza kuanza ujenzi mwaka huu."

Rais Ruto, kwa upande wake, amemmwagia sifa tele Dangote, akisema amethibitisha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujenga miradi yao wenyewe mikubwa bila kuwategemea wazungu.

Somo kutoka Nigeria: Mafanikio ya Kiwanda cha Lagos​

Kwa wanaohoji uwezo wa Dangote kutekeleza mradi huu, rekodi zake zinajieleza. Ahadi hii inakuja wakati bilionea huyo akiwa ametoka kukamilisha ujenzi wa kiwanda chake kingine kikubwa cha mafuta mjini Lagos, Nigeria, kilichogharimu Dola bilioni 20.

Kiwanda hicho kilijengwa kwa kipindi cha miaka 10, kikipinga dhana ya wakosoaji waliodhani asingejaribu kutatua changamoto ya nishati ambayo Serikali ya Nigeria ilishindwa kuitatua kwa miongo kadhaa. Hivi sasa, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi duniani chenye mtambo mmoja wa uzalishaji (single-train refinery), kikichakata mapipa 650,000 kwa siku na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana, hasa wakati huu ambapo usafirishaji wa nishati duniani unakabiliwa na changamoto kutokana na migogoro katika Mlango-bahari wa Hormuz.

Dangote amefanikiwa kuuza mafuta ya ndege (jet fuel) kwa faida kubwa kwa mashirika ya Ulaya, huku akilipa kipaumbele Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines), ambalo ndilo kubwa zaidi barani Afrika.

Nini maana yake kwetu Tanzania?​

Utajiri wa Dangote—kutoka kwenye biashara ya chumvi, sukari, unga, saruji hadi sasa mafuta—umechangiwa pia na uwezo wake wa kushawishi serikali kumpa misamaha ya kodi, kipaumbele katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na kulinda biashara zake dhidi ya ushindani wa bidhaa kutoka nje. Sasa anapanga kuongeza uzalishaji maradufu Lagos kufikia mapipa milioni 1.4 kwa siku ndani ya miezi 30 ijayo, akijiweka bega kwa bega na kampuni kubwa duniani kama Reliance Industries ya bilionea wa India, Mukesh Ambani.

Kwa sisi Watanzania, hatua hii ni kengele ya kuamka (wake-up call). "Ni jukumu la Waafrika kuwekeza katika bara lao wenyewe. Kama hatutafanya sisi, nani mwingine atafanya?" alihoji Dangote.

Kwa upande wetu Wadau:
Je, Tanzania tumekosa fursa hii adhimu kutokana na mapungufu ya miundombinu yetu ya Tanga kama inavyodaiwa, urasimu wetu wa ndani, au ni janja za kidiplomasia ambazo wenzetu wa Kenya wamezicheza vyema zaidi kibiashara?

Karibuni kwa mjadala.
Samia huwa anataka waarabu. Wajenzi wa kiwanda hicho angesikia wanatoka Oman wala asingesema kwa hisia kwamba kwanini Ruto hakumshirikisha.
 
Tanzania walikuwa na refinery pale Kigamboni wakaiua wenyewe kwa tamaa ili waagize mafuta yaliyokwisha safishwa wapige pesa sasa leo wanahitaji tena refinery ya nini wanafiki wakubwa.

Pia Tanzania sio nchi ya kibiashara kwani toka Nyerere alivyokuja na siasa ya ujamaa na kujitegemea ndipo alipoua ujasiriamali lkn Kenya hawakuwa na ujinga kama huo.
 
Ingekuwa ni mimi chap kwa haraka, ningekutana na Dr Rutto ili tuyaweke sawa na kuwa na msimamo mmoja. Ujue Dr Rutto ndiye ameshika kwenye mpini.....

Namuelewa Dangote kwani ni kweli kuwa, Kenya ipo mbali kiuchumi kulinganisha na sisi kwani hata makusanyo yake ya kodi yametupita mbali sana pamoja na kuwa na kiwango cha chini cha kodi ya VAT kuliko sisi (Kenya ni 16%)

Kenya hata shule zao za umma za Msingi na Sekondari wameshikilia ubora ule ule wa miaka ya 90, hivyo wanafunzi/wazazi wanaona fahari watoto wao kupangiwa shule ya umma......OGOPA NCHI ILIYOWEKEZA KWENYE ELIMU.....
Kwani lazima hiyo refinery ijengwe na Dangote tu?
Atafutwe tycoon mwingine kama akina Moh ibrahim na wengineo ndio wapewe hiyo dili ya Tanga huku Ruto na Dangote wake wakijenga ya kwao Mombasa
 
Kama kujengwa ni Tanzania tu kwasasa katazama kina tu !!

lkn Makampuni makubwa yanatabia za bint bint sitaki nataka nyingi !!

kwaiyo Dangote yupo kwenye Siasa ya uchumi!!

lkn lengo lake kuja Tanzania sasa izm kwanza ajidai Mombasa kuna kile sijui kile!!

ili Serikali yetu ifanye kama kumvutia kwake kumbe nayeye ndio mpango wake!!

Serikali yetu inajua mpango wake!!

Ruto anatumika na Dangote Eneo la uwekazaji ni kubwa sana!
lazima Dangote aje yeye kama yeye sio kujidai kumtumia Ruto na Mombasa na kulipia media kudanganya watu.

Tanzania tunaweza kumvutia China kuwekeza kwenye Refinery

Mwacheni tu.
Wachina wahuni hao sitaki hata kuvisikia
 
Kenya Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote amesema anafikiria kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta chenye uwezo wa kusafisha hadi mapipa 650,000 kwa siku nchini Kenya.Mradi unaokadiriwa kugharimu kati ya dola bilioni 15 hadi 17 za Kimarekani.

Kauli hiyo imeripotiwa na gazeti la Financial Times baada ya kufanya mahojiano na mfanyabiashara huyo tajiri barani Afrika, ambaye amesema kiwanda hicho kinaweza kujengwa mjini Mombasa kutokana na uwepo wa bandari kubwa na yenye kina kirefu.

Kauli ya Dangote imekuja siku chache baada ya Rais wa Kenya William Ruto kusema kuwa nchi za Afrika Mashariki zilikuwa zikijadili uwezekano wa kujenga kiwanda cha pamoja cha kusafisha mafuta katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Hata hivyo, Dangote alilinganisha bandari za Mombasa na Tanga akisema Kenya ina uchumi mkubwa na soko pana la walaji, huku akisisitiza kuwa uamuzi wa mwisho uko mikononi mwa Rais Ruto, na yeye yupo tayari kufuata mwelekeo ambao serikali ya Kenya itaamua.#dwkiswahili
 
Tume jipiga chenga wenyewe sio bure kuna mtu pale juu kakataa kisijengwe tanga
 
Back
Top Bottom