Dangote kishatupiga chenga Tanzania? Sasa kujenga Kenya Kiwanda cha Mafuta cha Trilioni 43. Ni baada ya kauli tata ya Rais Samia

Yes, lakini bado ni muhimu sana kwa raia nmoja mmoja. Imagine bei ya mafuta eneo la Tanga mpaka mikoa ya jirani, fursa za ajira na biashara ya mafuta n.k
Muwekezaji mkubwa haangalii umuhimu wa biashara yake kwa raia bali soko lenye faida kubwa zaidi, upatikanaji malighafi, miondombinu, nishati na sera za kibiashara.

Kuhusu bei za mafuta usiweke matumaini kwamba refinery itashusha bei kwa sababu kwanza hayo mafuta ghafi ya Uganda ni kidogo sana kwa hiyo bado tatendelea kuagiza mafuta mengi nje ya nchi, pia sio ajabu ukakuta hata gharama za uzalishaji na usafirishaji wa mafuta ya Uganda ika sawa au zaidi ya kutoka kwingine tunapoagiza kwa meli sasa hivi.
 
Reactions: Tsh
Hilo linajulikana. Kwa hiyo unataka kusema refinery ikijengwa Tanzania nchi yenye refinery plant haifaidiki na chochote?
Ninachosema Dangote anajua vizuri anapotaka kuwekeza refinery yake ukanda huu, hizi kelele nyingine za wanasiasa na mabishano ni propaganda za kutaka kuonekana relevant tu au janjajanja ya kibiashara ya Dangote kupata favours zaidi za kibiashara.
 
Ilikuwa ni ngumu sana oil refinery kujengwa Tanga....kwa Sababu

Mosi...waagizaji wa mafuta kutoka Uarabuni ni wafanyabiashara wakubwa na wapo watu wa Serikali wanafaidika sana...

Pili ..uarabuni wanalinda maslai yao ya kuuza mafuta...na wapate faida....waarabu wanajua mbinu chafu za kuzuia projects kama hizo

Hivyo ni ngumu sana kwa Serikali yetu kushawishi project hiyo kufanyika Tanga kwakuwa inagusa maslai ya wakubwa
 
Wanapenyeza Fitina Wapi? Ninyi Bandari ya Tanga Mliwauzia waarabu kwa miaka 100. Mwaarabu anataka bandari ya Tanga iwe ya kushusha Mafuta yake biashara yake ikue sio kupakia mafuta.

DP World si mlikuwa mnawatetea? Endeleeni sasa.

Mwarabu Kakataa
Bandari ya Tanga mwarabu Gani kauziwa? Tanzania tunachelewa kwa sababu ya majungu na umbeya usiokuwa na maana.
 
Tajiri ataamua mwenyewe.akajenge kiwanda sehemu ambayo hakuna malighafi au Akajenge sehemu ambayo kiwanda chake kitapata malighafi.
Popote refinery itakapojengwa itapata malighafi. Singapore, India na nchi nyingi za Ulaya wana refineries kubwa kuliko na hawana mafuta. Dangote atakachonufaika nacho zaidi kwa Tanzania labda ni ardhi ya bure.
 
Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika, Aliko Dangote, ametangaza nia yake ya kuwekeza nchini Kenya kwa kujenga kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta (oil refinery) chenye uwezo wa kuchakata mapipa 650,000 kwa siku. Uamuzi huu una
Sababu aliyoitoa dangote ni kina kirefu na ukubwa wa bandari ya Mombasa ukilinganisha na Tanga,muwe mnaacha kuzua Ili kumfanya mtu achukiwe
 
Hivi wanajua Nigeria anakotoka Dangote moja ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani? Ni kipi kiko totfauti kati ya Nigeria na Tanzania kwenye maisha ya watu? Je ni kipi kipo tofauti kati ya Nigeria na Finland nchi isiyozalisha mafuta kama Nigeria? Hoja yangu hapa ni kuwa ajenge, asijenge, hakuna kitakachobadilika. Afrika matatizo yake ni zaidi ya viwanda vya kusindika mafuta.
 
Popote refinery itakapojengwa itapata malighafi. Singapore, India na nchi nyingi za Ulaya wana refineries kubwa kuliko na hawana mafuta. Dangote atakachonufaika nacho zaidi kwa Tanzania labda ni ardhi ya bure.
Mkuu upo sahihi mno. Haya mambo hayatabadilisha maisha yetu na pengine yatafanya kuwa magumu zaidi.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…