Daniel Chongolo: Hotuba za viongozi wa CHADEMA hazina tija kwa wananchi

Daniel Chongolo: Hotuba za viongozi wa CHADEMA hazina tija kwa wananchi

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,891
Reaction score
8,448
Katibu mkuu wa CCM bwana Chongolo amesema anateswa na hotuba za viongozi wa Chadema kwenye majukwaa kwani hazina tija yoyote kwa wananchi.

Bwana Chongolo amesema ukiwasikiliza viongozi wa Chadema kwenye hotuba zao kuanzia mwanzo mpaka mwisho hawataji mahitaji muhimu kwa wananchi kama hospital, barabara, maji, umeme, shule, kilimo, utalii, viwanda etc wao huwa ni kuhubiri matumaini hewa na kutukana viongozi waliopita ambao wamelifanyia makubwa taifa hili, mbaya zaidi wanatukana hadi wananchi waliojiajiri kihalali kabisa.

Bwana Chongolo amewataka wananchi kuwapuuza Chadema duniani na mbinguni kwani ni wapuuzi wasiojielewa kabisa.
 
Hukumbuki hata kumiliki hiyo simu na kutuma ujumbe hapa kama hayo yoyote na mafanikio ya CCM Kwa miaka 60. Kwanza umedanganyaaa, hakuna watu wanaokunywa topeee
Mimi situmii simu iliyotengenezwa wala kulipiwa na CCM? simu imetengenezwa korea kule hakuna ccm. nilinunua kwa pesa yangu toka mfukoni wala siyo CCM ilinunua. Watu wanakunywa tope nenda kwenye jimbo la January Makamba kule bumbuli au kule Bahi kisha uje uongee upuuzi hapa. uanfikiria Tz ni Dar tu. Hata hapa Dar kule tandika watu wanakunywa maji ya visima vya wapemba chunvi tupu
 
Hivi hapa Kipanya alimaanisha nini?
IMG_20230309_101109.jpg
 
Mama akiwa Kilimanjaro siku ya wanawake, amesema hata ndani ya ccm kuna wahafidhina ambao hawakutaka maridhiano Kati ya ccm na chadema. Matamshi ya Chongolo ni mfano hai. Anapashwa kujitafakari na kuchukua hatua. Tuna imani yuko JF na Id ya uficho. Anapashwa kuwa mwangalifu na matakwa mapana ya nchi hii.
Kweli mama amewaelekeza viongozi wa ccm wajibu mapigo ya upinzani, lakini siyo kutumia misemo ya awamu ya tano.
 
Ni kweli Chongolo hotuba za CDM ni kumtukana JPM mwanzo mwisho ndiyo sera yao,wacha wajimalize.
 
Hukumbuki ata kumiliki hiyo simu na kutuma ujumbe hapa kama hayo yoyote na mafanikio ya CCM Kwa miaka 60. Kwanza umedanganyaaa, hakuna watu wanaokunywa topeee
Kwamba CCM ndiyo wamiliki wa makampuni ya kutengeneza simu na hata wanaotuma/tunaotuma hizi jumbe kutoka mataifa mengine ni mafanikio ya CCM, nchi zote duniani ziishukuru CCM kwa kumiliki simu. Kweli CCM ni simu na simu ni CCM.

Sukuma gang wanamtindio wa ubongo, labda kwa kuwa bado wanaomboleza maana kuomboleza kwa muda mrefu huwa kunasababisha hitilafu kwenye afya ya akili.
 
Wapuuzi ni Mapaka ambayo yamelitawala Taifa hili kwa miaka sitini lakini bado maji na matundu ya vyoo ni mahitaji muhimu kwa wananchi.
 
Amesema akiwa wapi maana bwana jalala ni mzushi
 
Hukumbuki ata kumiliki hiyo simu na kutuma ujumbe hapa kama hayo yoyote na mafanikio ya CCM Kwa miaka 60. Kwanza umedanganyaaa, hakuna watu wanaokunywa topeee
Mkuu una umri gani? Kwani wakati hatuna hizo simu, mtawala alikuwa wa nani? Haya masuala ya simu na mengineyo ni utandawazi na technology kwa dunia mzima. Hata wewe ungekuwa rais vingekuwepo.
 
Ruzuku ya CCM? Hivi Mwendawazimu alifanikiwa kuwa-brainwash kiasi hicho? No wonder ndiyo maana kuliibuka uzuzu wa mara barabara za Jiwe, meli za Jiwe, miradi ya Jiwe sasa je kipindi cha Mchonga kuanzia nchi ilipopata uhuru angekuwa ni Jiwe si hata nchi angeiita Jina lake na mikoa akipa majina ya watoto wake na hata mlima Kilimanjaro angeuita mlima Chato.
Eti ruzuku za CCM.
Mkuu una-imagination kali namna hii.
 
Mkuu una umri gani? Kwani wakati hatuna hizo simu, mtawala alikuwa wa nani? Haya masuala ya simu na mengineyo ni utandawazi na technology kwa dunia mzima. Hata wewe ungekuwa rais vingekuwepo.
Unaposema CCM hajafanya chochote, inaonesha hujui historian ya hiii nchi
 
Kwamba CCM ndiyo wamiliki wa makampuni ya kutengeneza simu na hata wanaotuma/tunaotuma hizi jumbe kutoka mataifa mengine ni mafanikio ya CCM, nchi zote duniani ziishukuru CCM kwa kumiliki simu. Kweli CCM ni simu na simu ni CCM.

Sukuma gang wanamtindio wa ubongo, labda kwa kuwa bado wanaomboleza maana kuomboleza kwa muda mrefu huwa kunasababisha hitilafu kwenye afya ya akili.
Mbona CCM imeweezesha maendeleo ya kiteknologia Kwa kiwango Cha juu?? CCM imeitoa nchii Toka mbaliiii, fikiriaa hivyo ulivyo na unavyochati hapa, haya yote ni mafanikio ya CCM. Angalia majengo ya kisasa ya watu binafsi yanavyojengwaa. Mawasiliano yameboresheka parefuuu, saaana. Ibu ipongezeni CCM Kwa kuikomboa Tanzania yetu. Acheni kubezaa
 
Mimi situmii simu iliyotengenezwa wala kulipiwa na CCM? simu imetengenezwa korea kule hakuna ccm. nilinunua kwa pesa yangu toka mfukoni wala siyo CCM ilinunua. Watu wanakunywa tope nenda kwenye jimbo la January Makamba kule bumbuli au kule Bahi kisha uje uongee upuuzi hapa. uanfikiria Tz ni Dar tu. Hata hapa Dar kule tandika watu wanakunywa maji ya visima vya wapemba chunvi tupu
Sawa lakini mawasiliano haya yakimtandao yamewezeshwa na nani kama sio CCM. Simu umenunulia huko, lakini mtandao unaoutumia ni juhudi za CCM. Ebu ipongezee CCM basiiii.
 
Back
Top Bottom