Azimio la Arusha lingali hai, ukitaka kuliona ni huuu mwendelezo wa sera ya UJAMAA. chama Cha mapinduzi ambacho ni mtekerezaji mkuu wa ujamaa, kingali Bado kinafanya KAZI Kwa mjibu wa sera ya UJAMAA.
YAFUATAYO ni matendo yanayo fanyika dhahiri Kwa mjibu wa ujamaa,
Sera ya UJAMAA na kujitegemea inaaamini hasa katika mgawanyo sawa wa maendeleo Kwa wote. Mfano, Leo hiii ukiona barabara inajengwa Moshi basi utakuta barabara hiyohiyo inajengwa sumbawanga ambapo yanakuwa nimatokeo ya makusanyo bajeti yaliyotokana na wananchi wenyewee. Pia huduma zote za jamii husambazwa Kila pahala ambapo Pana raia wa kitanzania kwani naye Kwa mjibu wa ujamaa, anastahiri huduma hiyooo. Kama sio ujamaa, huenda ungekuta maendeleo yanakuwa na ubaguzi wa hali ya juuu.
Hivyo basi sera ya UJAMAA ni MUHIMU Kwa sababu kunakuwa na mgawanyo sawa wa maendeleo Kwa wote bila ubaguziiii.
Tuwapuuze watu wanaohuniri sera za majimbo na kusema Kila mkoa ujitegemee kutoka a na rasilimali zao, wakisahau yakwamba Kuna baadhi ya mikoa hata ukipanda mahindi hayaotii. Sasa hao wataishije kama tukiacha UJAMAA?? Hivyo tuipongeze CCM Kwa kuwa na sera nzuri ya UJAMAA.