Naam, ninaelewa kiswahili kina changmoto zake.
Weka neno lako hapa, ili tujifunze zaidi.
"Kisheria, tunasema kila mkataba ni makubaliano, lakini sio kila makubaliano ni mkataba. Iko hivi, mkataba unakidhi matakwa yote ya kisheria, kama vile kuwa na maandishi, kuwa na pande mbili au zaidi zenye nia ya kisheria, kuwa na lengo halali na kuwa na ubadilishaji wa thamani.
Nikupe mfano, mimi na wewe tukikubaliana tuingie ubia wa kuuza magari, huu utaitwa mkataba kwasababu kuuza magari ni biashara halali, ili mradi tu tuzingatie sheria za nchi.
Lakini, makubaliano ni mikataba ambayo sheria na kanuni zake zinatawaliwa nje ya mfumo wa sheria mara nyingi, kwa sababu kuna makubaliano ya tabia nzuri ambayo yanaweza kuchukuliwa na umuhimu au uzito wa mkataba. Makubaliano hayo yanaweza kuzingatiwa kila siku, kwani watu kawaida huyatumia kufafanua masharti kuhusu shughuli ambayo inahitaji juhudi za pamoja kuzitimiza.
Kwa mfano, mimi na wewe tukikubaliana tuingie ubia wa kuuza madawa ya kulevya, huu hauwezi kuwa mkataba kwasababu kuuza madawa ya kulevya ni kosa kisheria, kwahiyo katika muktadha huu tutakuwa tumekubaliana tu lakini hatujaingia mkataba.
Kwa hiyo, tofauti ni kwamba mkataba una nguvu ya kisheria na unaweza kutumika katika mahakama ikiwa pande moja itavunja masharti yake, lakini makubaliano hayana nguvu hiyo na yanategemea imani na uaminifu wa pande zinazohusika."