Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naona mmeteka Nondo bhana.
Anagalia Sana Zitto sio wa mchezo mtaungua.
nchi hii nani asie mjua nondo kwenye hiyo songombingo?

ananukia pafyumu kali kinyama halafu kapiga raba moja ya maana sana nyeupe,

muungwana mbwa yule aise dah,
alituchezea sana wananchi kipindi cha nyufa za hostel za chuo šŸ’
 
jipige kifua useme sisi ni manyumbu...ataokotwa na kupotezwa mmoja momoja sababu ya ubinafsi wetu...na choyo chetu..tutawaacha wanetu na nani..tutaisha wakishawamaliza hao hatutabaki kwa amani
 
wAAYu9E.jpg
 
Ukiangalia kwa makini utagundua utekwaji na upatikanaji wa Abdul Nondo na Mo Dewji ni kama unafanana tofauti ni Abdul kapatikana haraka zaidi

Allah Akbar
 
Jana siku Nzima Ulikua Bize kweli unasifu kua zitto na Act wako fasta na wanapambana, wambir tunahitaji picha ya Nondo akiwa amejeruiwa vibaya,

Zitto alivujisha picha ya Sativa akiwa wodini vipibya Nondo, ulisema zitto siyo kama Mwamba, mwambie alete picha
 
Nimeota kuwa yale ya 17 March 2021 yatajirudia mapema mwakani. Hifadhini maneno haya.
 
Kwanini Rais Samia Suluhu Hassan ahojiwe matukio ya utekaji na mauaji ya raia ni suala la umuhimu mkubwa katika siasa za Tanzania na usalama wa raia. Katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, kumekuwa na ongezeko la matukio ya ukatili, utekaji na mauaji ya raia katika maeneo mbalimbali nchini. Hali hii imezua wasiwasi miongoni mwa wananchi na imefanya wengi kujiuliza kuhusu jukumu la serikali katika kuhakikisha usalama wa raia.

Kwanza, ni muhimu kuelewa kwamba Rais, kama kiongozi wa nchi, anawajibika moja kwa moja katika kulinda raia. Matukio ya utekaji na mauaji yanapotokea, ni lazima Rais aonyeshe uongozi thabiti kwa kuchukua hatua stahiki, ikiwa ni pamoja na kuanzisha uchunguzi wa kina na kuwawajibisha wahusika. Ikiwa Rais atakaa kimya bila kuchukua hatua, inaweza kutafsiriwa kama kutokujali hali ya usalama wa raia, jambo ambalo linaweza kuathiri imani ya wananchi kwa serikali.

Pili, kuna umuhimu wa kisiasa katika kuhojiwa kwa Rais kuhusu matukio haya. Katika mazingira ya kisiasa, matukio ya utekaji na mauaji yanaweza kufanyika na kushawishi hali ya kisiasa nchini. Wananchi wanahitaji kujua serikali inachukua hatua gani ili kukabiliana na tatizo hili. Kutojibu maswali ya wananchi kunaweza kusababisha kukosekana kwa uwazi wa kisiasa na kuibuka kwa malalamiko ambayo yanaweza kuathiri utawala wa Rais.

Tatu, kuhojiwa kwa Rais kunaweza kusaidia katika kutafuta mifumo bora ya usalama. Rais anaposhiriki katika kujadili masuala haya, anaweza kuhamasisha mabadiliko katika sera za usalama, kuhakikisha kuwa yanatekelezwa kwa ufanisi. Hii ni muhimu ili kuzuia matukio kama haya kutokea tena. Katika baadhi ya matukio, kuna madai kwamba baadhi ya vyombo vya usalama havijatekeleza wajibu wao ipasavyo, na kuhojiwa kwa Rais kunaweza kusaidia kujua viwango vya usalama vilivyopo na hatua zipi zinahitajika kuboresha hali hiyo.

Aidha, ni muhimu kutazama athari za kimataifa zinazoweza kutokea kutokana na matukio haya. Katika ulimwengu wa leo, matukio ya utekaji na mauaji yanaweza kuathiri sifa ya nchi kimataifa. Ikiwa Rais atashindwa kukabiliana na hali hii, kuna uwezekano wa nchi kuathirika katika masuala ya biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa. Hivyo, Rais anapaswa kuhojiwa ili kuonyesha kuwa serikali inachukua hatua za kutosha kulinda raia na kudumisha amani.

Pia, kuna umuhimu wa kuzingatia hali ya kiuchumi. Utekaji na mauaji yanaweza kuathiri shughuli za kiuchumi, hususan katika maeneo ambayo matukio haya hutokea mara kwa mara. Wananchi wanahitaji kuhisi kuwa wana usalama ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi. Serikali inapaswa kuhakikisha kuwa raia wanajihisi salama ili kukuza uchumi wa nchi.

Kuhusiana na haki za binadamu, Rais Samia anapaswa kuhojiwa kuhusu jinsi serikali inavyoshughulikia matukio haya katika muktadha wa haki za binadamu. Utekaji wa raia na mauaji ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, na serikali inawajibika kulinda haki hizo. Ikiwa serikali itashindwa kuchukua hatua, inaweza kujikuta ikikabiliwa na malalamiko kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na jamii ya kimataifa.

Kwa kumalizia, kuhojiwa kwa Rais Samia kuhusu matukio ya utekaji na mauaji ya raia ni muhimu kwa sababu inahusiana na usalama wa raia, uwazi wa kisiasa, ushawishi wa kimataifa, hali ya kiuchumi, na haki za binadamu. Ni jukumu la Rais kuhakikisha kuwa raia wanapata usalama na kwamba serikali inachukua hatua stahiki kukabiliana na tatizo hili. Wananchi wanahitaji kujua kwamba wana kiongozi anayewajali na anachukua hatua za kuhakikisha usalama wao. Hivyo, ni muhimu kwa Rais kujiweka wazi na kujibu maswali yanayohusiana na matukio haya ili kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
 
1. Milishindwa kupiga picha wahusika?
2. Mlishindwa kupiga picha gari lao?
3. Hakuna alie weza hata kuchukua video ya tukio?
4. Walikua na silaha za moto?
5. Walikua wangapi?
6. Mlishindwa kuwahoji?
7. Mlishimdwa kuwazuwia wasimchukue?
Hivi unachouliza hiki uko serious kweli?

Ukiwapiga picha ukawajua, au ukapiga picha gari ukalijua, utafanya nini?

Unaweza kuwazuia watu wana bunduki?

Hao siyo majambazi, hiyo ni special task force. Hata ukiita polisi hawawezi kuwazuia.
 
Tangu atekwe Nondo wa ACT Wazalendo, hakuna gazeti lolote la serikali, chama dola au vigazeti vinavyofadhiliwa na serikali lililoandika kuhusu habari hiyo. Kwa vyovyote vile ile ni habari kubwa iliyostahili kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti. Hata habari za utekaji mwingine uliofanyika huko nyuma haikupewa kabisa nafasi katika magazeti na media zote cha serikali, chama dola na vibaraka wao. Kwa wale wenye uwezo wa kusoma nyakati, Chronos, Kairos na Eschaton, hatuhitaji ushahidi zaidi ya huo wa wazi
 
Tangu atekwe Nondo wa ACT Wazalendo, hakuna gazeti lolote la serikali, chama dola au vigazeti vinavyofadhiliwa na serikali lililoandika kuhusu habari hiyo. Kwa vyovyote vile ile ni habari kubwa iliyostahili kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti. Kwa wale wenye uwezo wa kusoma nyakati, chronos, Kairos na Eschaton, hatuhitaji ushahidi zaidi ya huo wa wazi
Hii mbona iko obvious, umeshawahi kusikia viongozi wa CCM au wa serikali au wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakikemea matukio haya ya utekaji? Haihitaji magazeti kutokuandika eti ndiyo uamini uhusika wao au direct orders kutoka kwao au wao kujua kinachoendelea ni kitu gani, kwa sababu zipi, kwa malengo gani na kwa faida ya nani.
Kama pictures za wahusika huwa zipo kwenye CCTV cameras servers mpaka mitandaoni lakini haijawahi kutokea wakakamatwa what more proof do you need kujua kuwa hawa watu wako protected na dola?
Utekaji ni direct orders 'from above' (chama na serikali).
 
Tangu atekwe Nondo wa ACT Wazalendo, hakuna gazeti lolote la serikali, chama dola au vigazeti vinavyofadhiliwa na serikali lililoandika kuhusu habari hiyo. Kwa vyovyote vile ile ni habari kubwa iliyostahili kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti. Hata habari za utekaji mwingine uliofanyika huko nyuma haikupewa kabisa nafasi katika magazeti na media zote cha serikali, chama dola na vibaraka wao. Kwa wale wenye uwezo wa kusoma nyakati, Chronos, Kairos na Eschaton, hatuhitaji ushahidi zaidi ya huo wa wazi
Asante sana. Kila mtu anajua wauaji ni serikali na huyo mama mkwe wa Mcherengwa. Kuna mtu hajui hadi leo?
 
Tangu atekwe Nondo wa ACT Wazalendo, hakuna gazeti lolote la serikali, chama dola au vigazeti vinavyofadhiliwa na serikali lililoandika kuhusu habari hiyo.
Kila media inayo editorial policy yake na editorial independence yake ambayo haipaswi kuingiliwa!
Kwa vyovyote vile ile ni habari kubwa iliyostahili kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti. Hata habari za utekaji mwingine uliofanyika huko nyuma haikupewa kabisa nafasi katika magazeti na media zote cha serikali, chama dola na vibaraka wao.
Kuna habari inaweza kuwa ni kubwa kwako kustahili front page, lakini kwa mwingine isiwe habari kabisa!. Huu ndio Uhuru wa habari.
Kwa wale wenye uwezo wa kusoma nyakati, Chronos, Kairos na Eschaton, hatuhitaji ushahidi zaidi ya huo wa wazi
Mkuu Gulwa , ushahidi huu hauukidhi viwango vya ushahidi.
P
 
Hakuna gazeti hata moja lenye mrengo wa serikali au chama cha Mapinduzi iliyoandika habari za Abdul Nondo, hata gazeti la Global Publishers ambao ni vibaraka wa CCM hawajaandika. Kweli huu ni u-bias wa aina yake.
 
Kila media inayo editorial policy yake na editorial independence yake ambayo haipaswi kuingiliwa!

Kuna habari inaweza kuwa ni kubwa kwako kustahili front page, lakini kwa mwingine isiwe habari kabisa!. Huu ndio Uhuru wa habari.

Mkuu Gulwa , ushahidi huu hauukidhi viwango vya ushahidi.
P
Kwa hiyo Kwa CCM na vyombo vyske vya habari maisha ya watu siyo Sera Yao kuandika yanapokuwa hatarini? Utetezi mwingine Bora muwe mnakaa kimya tu. Mbona waliandika Kada wao alipopigwa risasi Iringa? Au tukubaliane CCM ni wabaguzi ndugu Mtetezi?
 
Tangu atekwe Nondo wa ACT Wazalendo, hakuna gazeti lolote la serikali, chama dola au vigazeti vinavyofadhiliwa na serikali lililoandika kuhusu habari hiyo. Kwa vyovyote vile ile ni habari kubwa iliyostahili kuwekwa kwenye kurasa za mbele za magazeti. Hata habari za utekaji mwingine uliofanyika huko nyuma haikupewa kabisa nafasi katika magazeti na media zote cha serikali, chama dola na vibaraka wao. Kwa wale wenye uwezo wa kusoma nyakati, Chronos, Kairos na Eschaton, hatuhitaji ushahidi zaidi ya huo wa wazi
IMG_20240922_035102.jpg
IMG_20240922_035041.jpg
 
Kila media inayo editorial policy yake na editorial independence yake ambayo haipaswi kuingiliwa!

Kuna habari inaweza kuwa ni kubwa kwako kustahili front page, lakini kwa mwingine isiwe habari kabisa!. Huu ndio Uhuru wa habari.

Mkuu Gulwa , ushahidi huu hauukidhi viwango vya ushahidi.
P
Pascal Mayalla U FM ya Bakhressa huwa inajiunga na DW Kiswahili saa saba mchana, sasa siku mbili DW wakizungumzia utekaji wa Nondo na wengine hukata matangazo hayo na kucheza muziki wa hovyo hovyo mpaka habari hiyo ipite.
Hata wakisoma magazeti habari za utekaji hawasomi hii Afadhali hata kwenye Uhuru media kwa uchawa.
 
Kwa hiyo Kwa CCM na vyombo vyske vya habari maisha ya watu siyo Sera Yao kuandika yanapokuwa hatarini? Utetezi mwingine Bora muwe mnakaa kimya tu. Mbona waliandika Kada wao alipopigwa risasi Iringa? Au tukubaliane CCM ni wabaguzi ndugu Mtetezi?
Kwanza tuwekane sawa, hakuna chombo chochote cha habari kinachomilikiwa na chama cha siasa. Media zote zinamilikiwa na makampuni tanzu yake.

Editorial independence ni uhuru wa media kutoa contents kwa uhuru kabisa
bila kuingiliwa, tusiwaingilie kwa kuwapangia nini watoe!.

Madam media ziko nyingi, usipotoa wewe, mwingine ametoa, umma umehabarika itoshe.

P
 
Back
Top Bottom