Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bahati mbaya sana wanatekeleza maagizo kutoka juu na sio kwa mujibu wa sheria.

Inasikitisha sana nchi imekuwa ya namna hii, wenye madaraka wanayatumia kwa namna isiyo sawa.
Shida iliyopo ni Idara ya Usalama kuruhusu hayo mambo kufanyika Kwa kuruhusu hata Green guard ya CCM nao kufanya majukumu ya Kipolisi

Kwahiyo haijulikani hasa wanaoteka watu ni wao ama Polisi ama green guard 🙌
 
Mbona namba za gari ni tofauti? Na zilizopo bandiko la kwanza!
Tukio la Singida taarifa ya Polisi inasema CHADEMA walivamia mkutano wa CCM Magereza wakaingilia kutuliza fujo, ndipo walifyatua risasi iliyomuua marehemu ambaye alikuwa ni mgombea eneo la tukio.
Ukienda palle mtaani kila mtu anajua marehemu aliuawa nyumbani kwake
 
Hivi utaratibu wa kumkamata mtuhumiwa si uko wazi Kwa mujibu wa Sheria?

Huyo Nondo ni Katibu wa Chama, ina maana ana address yake kwamba anaishi wapi

Ndio maana watu wanasema katekwa...

Lakini haya yote lawama ni kwa jeshi la Polisi, haya mautaratibu ya kunyakua watu wameyavumisha wao wenyewe...
 
Mimi sielewi IQ ya kutekana, kama wameshinda kwa 99% na mwakani tunajua watashinda kwa 99% why kutekana si uwaache tu waongee ukifika uchaguzi uibe maisha yaendelee au wapinzani wakiongea ndio watazuia polisi kuiba masanduku?

Umeongea Jambo kubwa mkuu
 
Ila Tanganyika bana. Hivi inakuwaj mtu anatekwa mbele ya watu tena stand, wakati kila siku watu wanahimizwa ulinzi shirikishi. Nadhani muda wa kutembea na sime au serikali kupitisha sheria km ya Marekani kila mtu amiliki silaha kadri ya mapenzi yake umefika.

Ila hawa watekaji hivi hawajui kuna hata wao wanaweza kufa hata bila ya kuguswa na mtu na hata kizigharimu familia zao.

Kuna watu wana dawa za asili za hatari, Yani mtu anarogwa mmoja akishakufa siku ya msiba wake ndugu yake yeyote au mtu yeyote atakaedodosha chozi kumlilia marehemu na yeye anadondoka hapo hapo na kukauka. Hebu fikiria wangapi wataondoka kabla hawajashtukia mchezo. Ebu hao watekaji wajitafakari hawako imara sana kwenye miili yao kuliko binadam wote dunisni, watakuja kuumiza familia na ndugu zao sababu za kibwege.

Kwa vile Nondo ni wa Kigoma, let's wait. Ningefurahi sn km wazee wa huko wangeshusha radi ya karine.
 
Hilo
CCM wanachokiweza ni kuteka kutesa na kuua.

Siasa imewashinda kitambo sana.
liko wazi sana wameshindwa kufanya siasa na mwisho wao hauko mbali. Kuna mtu kaandika mahali fulani kuwa, dola huwa haionjeshwi madaraka mara nyingi ipo siku nao watayatamani, hapo ndo utakuwa mwisho wao. Halahala kidole na jicho
 

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
Unajua wakati sheria ya usala wa Taifa kuruhusiwa kukamata watu watu wengi waliipigia kelele sheria hii na mtu wavkwanza kuikemea nakumbuka alikuwa Shekh Ponda watu wakamchukulia kuwa kwakuwa ni mwanaharakati wa kidini akaja tundulisi watu wakamuona kwakuwa ni mwanaharakati wa kisiasa lakini tangu sheria hii ipitishwe tumeona watu wengi wakitekwa na kuuwa pasipo POLISI kuchukua hatua yoyote kama vile wanasema si wabunge wenu wenyewe wamepitisha sheria ya hovyo sasa mnalia na Nani. Kuna Targeted group ambolo lipo Targrted na hawa watu ni siku zote utasia ni Landcrusser nyeupe hata yule kija wa kule tukuyu aliye chana picha ya Rais alichukuliwa na watu hao hao wenye Landcrusser nyeupe, Aly kibao gari lililo zuia basi la Tasshrifu mbele na nyuma ni hizo hizo landcrusser nyeupe, Mwenyekiti wa Bawacha kule kibiti anasema alitekwa na watu walikuwa na Landcrusser nyeupe. Haya kama ndiyo staili yakutulinda hiyo sawa, lakini kwa upande wangu naona mambo siyo shwari, mkidhani mtaweza kuwanyamazisha wananchi kwakuwatisha na kuwatesa mjue na wao watatafuta njia za kujihami sasa ikifikia hapo itakuwa mtafutamno mkimchukua kwao mmoja kwenu wanachukua kumi hivyo hivyo mpaka kila upande utakapo kubali suruhu ila itakuwa damu imemwagika nyingi sana kwani nakumbuka ya kibiti, mkuranga na Rufiji mpaka sasa ni vilio kwa familia nyingi tu Azori gwanda alijaribu kufuatilia aliishia kwenye shimo la tewa.
 
Ukifuatilia harakati za Abdul nondo na wote wa namna yake watakuambia wanawapigania watanzania!
Ukweli mchungu hizo harakati ni sehemu ya kazi zao za kuwapatia riziki kama alivyo fundi mjenzi dereva mwalimu na askari nk, sasa kila kutafuta riziki kuna changamoto zake ambazo mtu huzikabili na kusonga mbele.
Fundi umeme kuna wakati ana pigwa shoti na fundi bomba kuna wakati analowana maji na hakuna anaye jali kwa vile ni wajibu wake!
Sasa hao wasiasa na wanaharakati wanataka kila wanapo pata changamoto watanzania wote wasimame nao hali ni wajibu wao kuzikabili.
Mawazo ya kijinga kama haya ndo maana hii nchi mpaka leo ni maskini
Na mtu kama huyu utashangaa ni baba na anafamilia
Tanzania hatuna wapambanaji bali ubinafsi unaitafuna hii nchi
 
Swala
Ila Tanganyika bana. Hivi inakuwaj mtu anatekwa mbele ya watu tena stand, wakati kila siku watu wanahimizwa ulinzi shirikishi. Nadhani muda wa kutembea na sime au serikali kupitisha sheria km ya Marekani kila mtu amiliki silaha kadri ya mapenzi yake umefika.

Ila hawa watekaji hivi hawajui kuna hata wao wanaweza kufa hata bila ya kuguswa na mtu na hata kizigharimu familia zao.

Kuna watu wana dawa za asili za hatari, Yani mtu anarogwa mmoja akishakufa siku ya msiba wake ndugu yake yeyote au mtu yeyote atakaedodosha chozi kumlilia marehemu na yeye anadondoka hapo hapo na kukauka. Hebu fikiria wangapi wataondoka kabla hawajashtukia mchezo. Ebu hao watekaji wajitafakari hawako imara sana kwenye miili yao kuliko binadam wote dunisni, watakuja kuumiza familia na ndugu zao sababu za kibwege.

Kwa vile Nondo ni wa Kigoma, let's wait. Ningefurahi sn km wazee wa huko wangeshusha radi ya karine.
la kumiliki silaha halina Shida. Sema sasa sisi wenyewe hatuko tayari. Mtu utakuta anamiliki mamilioni lakini hana hata bastola, hebu tubadilike. Kama watanzania wengi tungekuwa na tabia ya kumiliki silaha ninaamini haya matukio yasingefanyika kiboya namna huu, kuna namna hao watekaji wangekuwa na tahadhari sana
 
Hivi hawa wasiojulikana huwa wanatumwa na nani, au wanaowatuma nao hawajulikani, kwani pingu wamiliki wake ni nani, au pingu yeyote anaweza kuzimiliki?
Watumwe na na nani wakati wao ndiyo kazi yao hiyo kulenga watu wote wenyevidomo domo yaani wewe ukishindwa kuuzuia tu mdomo wako unashtukia hao. Wanaondoka na wewe kama mwewe. Hapo nadhani wana list tusubiri nani anafuata.
 
Back
Top Bottom