Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Pre GE2025 Dar: Abdul Nondo atekwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watumwe na na nani wakati wao ndiyo kazi yao hiyo kulenga watu wote wenyevidomo domo yaani wewe ukishindwa kuuzuia tu mdomo wako unashtukia hao. Wanaondoka na wewe kama mwewe. Hapo nadhani wana list tusubiri nani anafuata.
Wenye matonge yao
 
Kama mmekabizi pingu na simu kwa police Sina Cha kuwasaidia hiyo pingu ingewafukuzisha kazi Wengi na simu tungeitumia kufuatilia waarifu hapo MMEFANYA USHENZI FUTENI LIUZI LENU
Sasa wakabidhi wapi mkuu?? Polisi ndo wenye mandate ya kufanya uchunguzi kama huo... yaani ubaki na lisimu la watekaji halafu kesho jamaa kaokotwa kafa, na wewe raia umedakwa na hilo lisimu, jiulize utakuwa kwenye hali gani?

Suala la kwamba polisi watafanyia kazi au kutofanyia, hiyo ni juu yao, ila raia wema wametimiza wajibu wao
 
Haya mambo ya utekaji si mageni hapa jijini labda kwa wageni jijini
 
Huu ni ujinga uliopitiliza sasa, mtu maarufu kama Abdul Nondo unashida naye unashindwa kumpa wito afike kituoni central polisi Dar, unamhoji na kama kumpeleka mahakamani unampeleka.
Kumfuata kituo cha basi na kumchukua billa taratibu tayari ni utekaji huo SIO SAWA.

Tusipokuwa makini tutajikuta pabaya.
 

Mwanasiasa Abdull Nondo wa Chama Cha ACT Wazalendo amechukuliwa asubuhi ya Leo na wati waliomvamia akiwa kituo Cha basi Mbezi.

Katika purukushani hiyo wahusika walidondosha pingu na sasa hatma yake haijulikani mpaka wakati huu

====

UPDATE

JamiiForums imewasiliana na Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT Wazalendo Shangwe Ayo ambapo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza Nondo alikuwa ametokea Kigoma baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kumalizika, ambapo wakati anashuka kwenye basi Stendi ya Magufuli watu wasiyojulikana watatu walimfuata kukawa na purukushani Nondo akijitahidi kujinasua lakini walifanikiwa kumchukua na kuangusha pingu walizokuwa wameenda nazo pamoja na begi alilokuwanalo Nondo

Matukio mengine ya utekaji kuwahi kufanyika nchini haya hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Shangwe ameeleza pia gari lililomteka Nondo ni Land Cruiser nyeupe yenye namba za usajili T 249 EMV. Taarifa za awali walizitoa kwa mashuhuda ambao walikuwa wanamfagamu Nondo, baada ya kufungua begi lake kulikuwa na note book ambayo nayo ilithibisha kumilikiwa na Abdul Nondo

Pia shuhuda aliyekuwa eneo la tukio amesema gari hilo lililokuja kumteka Abdul Nondo lilikuwa na watu 4, wawili wakiwa na bunduki na wawili wakiwa mikono mitupu, watu walipoenda kuangalia kuna nini na kujaribu kuhoji waliwanyooshea bastola na hivyo watu kubaki wanaangalia tukio hilo likitokea na Abdul Nondo akawa ametekwa! Katika purukushani hizo kwa maelezo ya shuhuda mbali na pingu na bengi la Nondo, ilianguka pia inadaiwa simu ya moja ya watekaji ambavyo vyote vilikabidhiwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Magufuli.
Ndiye yule aliyekutwa kwa mwanamke ?
 
Pole sana ndugu yetu Abdul, mwenyezi Mungu akupiganie wakuachilie salama.

Lakini Abdul kwa level aliyofikia, alitakiwa awe hata na ka vitz jamani, sass watu wanakuja kukutekea stand, tena stendi ya mbezi shamba.
Nimeshindwa kukutofautisha na nguruwe. Sio lazma kwenye mijadala ya msingi uongee pumba kuna forums nyingi humu.
 
Simba mmoja anavamia kundi kuuuuubwa la nyumbu takribani nyumbu 600 anajichagulia mmoja wengine 559 wanasimama pembeni na kushuhudia mwenzao akitafunwa.
Hujui hesabu na wewe ni nyumbu tu kama nyumbu wenzio 40 ambao hamjulikani mmeelekea wapi bora wenzako 559 wanaangalia + 1 kachukuliwa = 560 + 40 msiojielewa ndio inakua nyumbu 600
Swali nyingi nyumbu 40 mmeenda wapi😂
 
Watumwe na na nani wakati wao ndiyo kazi yao hiyo kulenga watu wote wenyevidomo domo yaani wewe ukishindwa kuuzuia tu mdomo wako unashtukia hao. Wanaondoka na wewe kama mwewe. Hapo nadhani wana list tusubiri nani anafuata.
labda tuulize, wanateka wenye kidomodomo, kidomodomo kwa mambo yapi, na wanateka kwa maslahi ya nani au maslahi ya kitu gani?
 
Amechukuliwa na police au watu wasiojulikana???
Kuna watu hawajulikani dunia hii??
Hawajulikani hawana ndugu???
Hawajulikani hawajazaliwa na mama???
Nani anawalipa mishahara ilihali hawajulikani????
sikila wewe, 'wasiojulikana' ni dhana tu ya uficho inayotumiwa na wahusika wenye mamlaka ya kutoa taarifa. Ukweli ni kwamba 'wasiojulikana' wanajulikana vema tu, tena huwa wanaacha nyayo kwenye uharamia wao. Kuna siku wataumbuka mchana kweupe
 
Askari wanasema wanafuatilia jambo hilo 🤣🤣 sasa sijui wanamtafutia wapi wakati waliomchukua wamedondosha pingu 🤣🤣
Haya mambo aliyazungumzia askofu mwamakula baada ya tukio la kariakoo ila watu hapa walijaa hisia ila kama utani usikute huyu dogo nae anapotea anakuja kuonekana akiwa mwili umeharibika
 
Watumwe na na nani wakati wao ndiyo kazi yao hiyo kulenga watu wote wenyevidomo domo yaani wewe ukishindwa kuuzuia tu mdomo wako unashtukia hao. Wanaondoka na wewe kama mwewe. Hapo nadhani wana list tusubiri nani anafuata.
Kwa hiyo uhuru wa maoni na wajibu wa kushiriki mijadala ya kitaifa ni kuwa na vidomo domo?
Hivi kwanini wanataka kulazimisha malkia asifiwe kwa kila kitu??
 
Back
Top Bottom