KERO Dar: Abiria wateseka kwenye foleni kusubiri mabasi ya mwendokasi Kituo cha Mbezi Mwisho

KERO Dar: Abiria wateseka kwenye foleni kusubiri mabasi ya mwendokasi Kituo cha Mbezi Mwisho

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kuna siku nilipanda daladala asubuhi hapo Mbezi kwenda Kariakoo! Aisee nilijuta kuzaliwa. Maana nilitumia karibia masaa 3-4 kufika Kariakoo. Ile route ilikuwa ni ndefu mpaka basi.

Halafu cha kushangaza kila kituo abiria waliokuwa wanapanda walikuwa ni wengi kuliko wale waliokuwa wanashuka!!! Hivi watu wa Dar mnawezaje kuvumilia hayo mateso aisee
 
Tatizo ni majizi sana hata hela za uendeshaji tu hawana wanakomba zote
Mabasi yanakufa na kuzima kisa oil au filter
Nchi inaenda tu, kweli ni kazi isiyo ngumu kuendesha biashara hii ila nani muadilifu wa kuisimamia?
Kuna jamaa yangu anamiliki coaster za g'mboto -simu 2000,foleni,kugombea abiria usumbufu wa trafiki na bado faida anaiona kubwa tu,mwendokasi wao ndio wanawaringia abiria,wana barabara yao maalum ambayo haina foleni,awapati usumbufu wowote wa polisi trafic na bado wanashindwa kutoa huduma bora na wanalalamika wanapata hasara halafu sekta kama hizo wakipewa watu kutoka nje wanaojielewa waziendeshe tunaanza kulalamika!
 
Aisee kweli hawa jamaa mishipa ya aibu ilishakatika
Ukiona chuma inachomoka pale Kimara terminal au Mbezi zile ndefu ndani mna abiria siyo chini ya 230/40 zile kipisi zinabeba 150/55 na route zote kwa muda wa asubuhi kutoka Kimara/Mbezi to town hakuna gari zinavuka Ubungo milango ikiwa inafunguka normally kwa sababu ya kujaza sana.

Jioni vivyo hivyo hakuna gari inatoka mjini (Gerezani ,Kivukoni) ikapita fire bila kujaza sana abiria,hapo hatujaweka zile route za Kibaha-Kimara,Kimara-Mloganzila,Kimara-Magufuli Terminal,Kimara-Mbezi Terminal na Muhimbili-Gerezani.
 
Mwendokasi zimekua kama daladala,haiji kituoni mpaka ihakikishe abiria wamejazana vya kutosha,ili mkiingia mshonane kwelikweli.
 
Usafiri huo ni wa malofa na sisi malofa

Usafiri huo ni wa waduanzi kabisa

Ova
We si ndio unasemaga watu waache kuendesha magari yao kisa bei ya mafuta imepanda.


Anyways mwendokasi/daladala ni laana

 
We si ndio unasemaga watu waache kuendesha magari yao kisa bei ya mafuta imepanda.


Anyways mwendokasi/daladala ni laana

[emoji1]

Ova
 
Kila mtu awe na gari lake huko barabarani itakuaje?
Barabara zitapanuliwa kuendana na wingi magari..maana magari yakiwa mengi hata kodi itakua kubwa kuanzia Ku import, mafuta, vipuri bila kusahau fine za barabarani.
 
Sisemi
 

Attachments

  • IMG_1068.jpeg
    IMG_1068.jpeg
    1.3 MB · Views: 5
  • IMG_1069.jpeg
    IMG_1069.jpeg
    1.3 MB · Views: 5
Hali ya usafiri wa katika Kituo cha Daladala cha Mbezi Mwisho ilivyo asubuhi ya leo Septemba 25, 2023, Mdau anasema hakuna gari za Mwendokasi, foleni ya abiria imefika zaidi ya watu 9,600


Pia soma:

DART: Sababu ya uhaba wa mabasi ya Mwendokasi Vituoni, ni hakuna mfumo rasmi wa kuongozea mabasi, Pia mabasi ni machache

Tanzania hatuna viongozi
 
Maboresho yanayotakiwa kufanyika katika mradi wa mabasi yaendayo haraka Bus rapid transit (BRT) jijini Dar es Salaam.


Nimebaini changamoto kadhaa zinazotakiwa kutatuliwa katika mradi huu.


Hivyo nimemshauri juu ya maboresho yanayotakiwa kufanywa katika mradi huu. Pitia katika link hii kusoma ushauri wote: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….


Pia michango mbalimbali imetolewa na wadau wengine na wameshauri jinsi ambavyo mfumo wa uendeshaji wa haya mabasi unapaswa kuwa ili kwendana na ukuaji wa teknolojia:


Ushauri wote tumeuandika hapa: Kwako Mkurugenzi mpya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART): Katatue changamoto zifuatazo….
 
Back
Top Bottom