Mtu anaoa anamuweka ndani mke mwenye kila kitakiwacho, wanafurahia mahusiano ghafla mwanaume anajiona kidume.
Anaanza kuchepuka anarudi alfajiri bila maelezo, akiulizwa anageuza kibao eti, eti mke hana utii, ana mdomo, ana kelele ndio anakuwa amepata sababu ya kuhalalisha alilolianza....
Eti mwanamke hakasiriki, hana hasira, haumii, haathiriki kisaikolojia yaani aendelee kumfurahia mume anayetaka utii kwa kunukuu vitabu vitakatifu bila yeye kutimiza aliyotakiwa na kitabu hichohicho....
Hongera zao wanaoishi bila kuumizana hisia...Mungu awalinde. Awaepushe na wala msije kuwa kama haya mengine yanayodhani yakioa mke hawezi kuondoka, mke akiondoka anamtafuta amuue eti amkomoe na kukomoa wampendao....STUPID