Dar: Ahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua mkewe

unapiga chini unaendelea na maisha, sio unajipa shida ya kwenda jela bure kabisa.

anyway tuchunge hasira zetu sana.
 
View attachment 2763050
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salalam, iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, All Balanda Idofulo, kunyongwa hadi kufa, baada kupatikana na hatia ya kumuua mkewe, aitwaye Selan Kondo kwa kumchoma kisu begani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Septemba 26, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, aliyepewa mamlaka ya nyongeza kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.

"Kwa namna yoyote ile, nimejiridhisha kuwa mshtakiwa ulimuua Kondo kwa kumchoma kisu begeni baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanane akiwemo mtoto wa marehemu mwenye umri wa miaka minane, ambaye aliieleza mahakama kuwa alishuhudia ukimchoma kisu mama yake begani baada ya kutokea msuguano baina yako na marehemu," amesema hakimu Kiswaga na kuongeza

"Kwenye kosa hili la mauaji ya kuua kwa kukusudia, hakuna nafuu iliyotolewa na sheria zaidi ya adhabu ya kunyongwa, hivyo mahakama hii inakuhukumu kifungo cha kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa ipo wazi iwapo hujaridhika na adhabu hii," amesema Hakimu Kiswaga.

Idofulo anadaiwa kumuua Selan Kondo, Mei 6, 2019 eneo la Tabata Liwiti, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alimuita Kondo waonane ili wajadiliane namna ya kurudiana baada ya kutengana kwa muda.

MWANANCHI
Wakili arudishe pesa,kashindwa kazi yake! Nilimsikia ndg wa Mume akisema!!
 
ndio nini sasa unaniita kuja kushuhudia mwanaume mwenzangu akinyongwa... Hapa napunguza stress au ndio unanimalizia nife kabisa... Sawa tuuu uncle...
🤣🤣 Pole uncle
 
Ingekuwa MARA Uzi ungetembea kwa matusi,kejeli na kila aina ya uchafu kwa watu wa mkoa wa mara. Sasa ngoma imekita uswahilini huko kwenye jiji kubwa mko kimya.
Wanaume tambueni kuwa Hawa wanawake ndio chanzo Cha magonjwa ya akili.
#wapuuzen
 
Nyie si huwa mnasifia mume akiua mke? Leo mnaonea huruma watoto.
Shem vipi tena?
Mwanaume anang'ang'ania mwanamke ni bwege... wanawake wako wengi, ukishindwana na mmoja; move to the next one.
 
Huyo Hakimu ni taahira? Watu wakikwaruzana kisha katika ugomvi mmoja akafa si inaitwa ‘Manslaughter’ (kuua bila kukusudia), sasa hiyo kukusudia inatoka wapi?

Hivi ukitaka kuua mtu unamchoma begani au kifuani? , na ukitaka kuua mtu unamuua mbele ya watoto wake au unamvizia akiwa peke yake?
 
View attachment 2763050
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salalam, iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu, All Balanda Idofulo, kunyongwa hadi kufa, baada kupatikana na hatia ya kumuua mkewe, aitwaye Selan Kondo kwa kumchoma kisu begani.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Septemba 26, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, aliyepewa mamlaka ya nyongeza kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.

"Kwa namna yoyote ile, nimejiridhisha kuwa mshtakiwa ulimuua Kondo kwa kumchoma kisu begeni baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wanane akiwemo mtoto wa marehemu mwenye umri wa miaka minane, ambaye aliieleza mahakama kuwa alishuhudia ukimchoma kisu mama yake begani baada ya kutokea msuguano baina yako na marehemu," amesema hakimu Kiswaga na kuongeza

"Kwenye kosa hili la mauaji ya kuua kwa kukusudia, hakuna nafuu iliyotolewa na sheria zaidi ya adhabu ya kunyongwa, hivyo mahakama hii inakuhukumu kifungo cha kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa ipo wazi iwapo hujaridhika na adhabu hii," amesema Hakimu Kiswaga.

Idofulo anadaiwa kumuua Selan Kondo, Mei 6, 2019 eneo la Tabata Liwiti, Wilaya ya Ilala.

Inadaiwa siku hiyo ya tukio, mshtakiwa alimuita Kondo waonane ili wajadiliane namna ya kurudiana baada ya kutengana kwa muda.

MWANANCHI
Mungu atupe hekima na subira ya kudhibiti hasira zetu dhidi ya wenza wetu.

Najiuliza, wale waliouawa kwa mikono ya serikali kama vile Mawazo, Ben Saanane, Azory Gwanda na kadhalika, nani anapaswa kushtakiwa na hukumu yake ipoje
 
Back
Top Bottom