DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Ni kweli siwapendi, walituibia vya kutosha Tanzania na adhabu pekee walipata ni kuachia Ubunge na kujivua nyadhifa zao kwenye chama chake.
Mtaani huku vijana wanaiba kuku na chakula tunawapiga mawe hadi kufa.
Ni sawa usemavyo lakini usisahau katika wizi huo hata wasio wahindi walihusika kikamilifu, hivyo sio vizuri kubagua.
 
kwani nani mlimpa? sasa mbona unaidhalilisha serikali maana inaonekana sasa serikali haifanyi lolote inasubiri iambiwe nini cha kufanya. halafu wewe unaifanyia kazi humu JF? maana huna mbele wala nyuma ... zaidi ya kushabikia hata usiyoyajua. serikali iwakamate wale mafisadi niliotaja wakiongozwa na kiongozi wao. aliyefisadi pesa nyingi sana.

Rudisheni ile list of Shame tuifanyie kazi
 
halafu hawa watu wanachwaje kwenye tuhuma za ufisadi?
1. kikwete
2. andrew chenge
3. lowassa
4. gsm
5. karamagi n.k?
Usimsahau mshauri Mkuu wa Raisi Magufuli na mwasisi wa magenge ya ufisadi nchini.
Mzee Benjamini William Mkapa ambaye aliuza nchi bure na kujilimbikizia mali kinyume na maadili.
Hawa wafanyabiashara walianza kukua kipindi cha utawala wake au umesahau Tume ya Warioba 1997 ??
 
Waambie hao wenye kampuni na wanasheria wke kuwa ule wakati wa kuchezea mali za watanzania kwa kuwa unajua kucheza na sheria za nchi umekwisha! mtatoa matamko sana.
ni kweli muda wa watu kuuza nyumba za serikali na kununua kivuko kibovu haupo, ila upo wa kufisadi 1.5 trilioni
 
Kwa wana JF,

Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi na kukutwa na nyara za serikali pia katika makosa hayo.

Taarifa zaidi zinakuja.

Kwa Taarifa za awali, Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums
Ngoja tuone mwisho utakuwaje cos wengi wamefikishwa mwisho hadi leo haieleweki
 
kwani nani mlimpa? sasa mbona unaidhalilisha serikali maana inaonekana sasa serikali haifanyi lolote inasubiri iambiwe nini cha kufanya. halafu wewe unaifanyia kazi humu JF? maana huna mbele wala nyuma ... zaidi ya kushabikia hata usiyoyajua. serikali iwakamate wale mafisadi niliotaja wakiongozwa na kiongozi wao. aliyefisadi pesa nyingi sana.

Mkuu hawa wafia vyama wanajua kila mtu ana upande kumbe wengi ndugu yetu ni Tanzania na tuko kuiona Tanzania inasonga mbele na sio kushabikia unafiki, Hawajui kama ufisadi na mafisadi watanzania walio wengi wanawajua lakini wanajifanya kama watanzania hatujui nini kinaendelea, JK, Mkapa, Chenge, Karamagi, Ngeleja, Lowassa, na wengine wengi ndio miziz ya ufisadi na ndio chanzo cha ufisadi maana kupitia hawa watu hao tunaowakamata ndio walipata access ya kupenya kwenye mifumo na kwenye hizo mali za hao matajiri pia kuna mikono ya hawa wanasiasa na bila shaka Serikali hilo inalijua.
 
Back
Top Bottom