DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

DAR: Akram Aziz akamatwa, afikishwa Mahakama ya Kisutu. Ana makosa 75!

Duh, maskini kazi yetu kushangilia kila tajiri anaponyanyaswa, lakini hamkumbuki maisha yetu yameshikwa na huyo tajiri. Tumashangilia ujinga, uonevu na kila aina ya dhulma inayofanyika kwa matajiri. Iko siku nyuma huu mchezo siri iliyojificha itafunuliwa!!
Hii inanifanya nitafakari historia pale Wajerumani walivyokuwa wakishangilia madhila waliyokuwa wakikutana nayo Mayahudi(Jews) dhidi ya utawala wa Adolf Hitler. Exactly the same shit is happening in Tz.
 
Watanzania tuamke!!! Mazingira haya yametengenezwa tu, kama taarifa ya mwanzo ilivyosema kua "askari wamemkamata akiwa na vibali sahihi, ila wakaamua kuondoka navyo vibali vyote original na kukataa kuacha copy ofisini kwake". Hapa kama kawaida, serekali inatuhamisha toka maswala fulani kutupeleka kwengine. Tumeshafanywa kama watoto wa chekechea sasa!!!

Watanzania lini tutapata akili jamani ya kuchanganua mambo na ukweli????? Tulishuhudia YUSUF MANJI alikamatwa na akafikishwa mahakamani kwa kukutwa na NYARA ZA SEREKALI, MIHURI YA JESHI, VITAMBAA VYA SARE ZA JESHI. Case iliishia wapi?????? Nani anaehoji mpaka sasa kuhusu hio tuhuma zake au case alizoshitakiwa nazo?????? Kama kweli angeachiwa huru????

Inasikitisha sana kuona mtu akitetea uonevu unaofanywa na askari kwa raia, na uongo tunaopewa raia na serekali yetu, kama huu na iliopita.

Na inasikitisha zaidi kuona wafanya biashara wakubwa wakionewa mpaka kufikia hatua wanafunga biashara zao na watanzania wenzetu kibao wanakosa ajira.
Rubbish!
 
Screenshot_20181031-193931_1541004059577.jpg

Habari ya Disemba,2012: Trio caught with 78 jumbo tusks after car chase
 
Kwahio unamtetea mtuhumiwa wa ujangili?

Si uachie mahakama iamue kama ni jangili au sio jangili?

Mtu ana makosa 75 wamtetea kweli, unayafahamu hayo makosa?


Mmmhh!!! Sitii neno huu uzi?
 
Kwa wana JF,

Natambua kuwa kuna threads 2 humu; ila taarifa ni kuwa Akram Aziz ambaye ni mdogo wa Mbunge wa zamani wa Igunga, Ndg. Rostam Aziz, ni kweli alikamatwa na Vyombo vya Dola na mchana huu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu.

View attachment 917003

Kwa kuanzia, ana makosa takribani 75 ambayo anahusishwa nayo. Kuna utakatishaji fedha/uhujumu uchumi na kukutwa na nyara za serikali pia katika makosa hayo.

View attachment 917001
View attachment 917002

Kwa Taarifa za awali, Soma => Akram Aziz adaiwa kukamatwa na nyara za Serikali... - JamiiForums
Huyu naye mshamba sana, hakusoma alama za nyakati kama kaka yake.
 
Utahitaji pia kumchukia Mkapa aliyeasisi skandali ya EPA. Kwa maneno mengine usibague kwa misingi ya kabila katika kuchukia ufisadi. Uchukie ufisadi lakini usichukie mtu kwa misingi ya kabila lake.
Umepatia mzee baba, Silipendi kabisa lile lizee.
 
Mimi na wewe hatufahamu hayo.

Huenda ameonyesha stakabadhi ya hivyo vifaa kwamba amenunua nje ya nchi na havikupatikana hapahapa Tanzania, na kisha wakamwachia.

Ndo maana hakufikishwa mahakamani na kumalizana na jeshi na polisi, who knows?

Yaani kwa kifupi sisi raia hatufahamu chochote ila hatuwezi kulaumu polisi kwa kila kitu kwa vile tu imejengwa picha mbaya juu yao.


Duuuuu!!
 
Tuacheni kutetea maovu , mtu anakamtwa na meno ya Tembo tena vizibiti vipo tunasema ameonewa eti kwa kuwa ni tajiri au kwa kuwa anapingana na serikali iliyopo madarkani, watanzania mbona tuko down sana kiasi hiki? kweli mtu kakamatwa na uwindaji haramu tuna sema serikali inanyanyasa matajiri? wangapi wamekamatwa Tanzania hii kwa uwindaji haramu na wako huko wanasubiri kesi zao? kama ameonewa mahakama ipo itatoa hukumu, lakini sio tuache kuchukua hatua pindi watu wanapokuwa na hatia, tunataka kujenga taifa la ajabu sana kisa eti tunataka huyo tajiri aliyekamatwa tumtetete hapa tumchonganishe na serikali ili akitoka basi aungane nasi katika vyama vyetu kisa tupate misaada ya ufadhili, siasa ni mbaya sana tukiicha iwe katika akiri zetu muda wote maana kila kitakachokuwa kinatokea hapa nchini baada ya kujadili in a facts way tunalichukulia ni suala lakutafutia wafuasi, lets the government do the work, kuna mahakama zitaamua, ndio maana mimi nasem serikali iliyopo itakuwa ngumu sana kuyatoa, maana yanazidi kupata uungwaji mkubwa wa watu na kujiweka katika mazingira mazuri kwa kipindi kijacho,wanacheza na agenda zao vizuri, rushwa, ujangili,madawa ya kulevya na kadhalika, sisi tunadharau lakini wenzetu ndo wanakimbia hivyo.
Mkuu achana nao, Nyumbu atabaki kuwa nyumbu,usihangaike sana kama unajua tabia za nyumbu!
 
Habari Mpasuko: Mtandao Ndugu wa Rostam, Zitto Wanaswa

Kuna habari huenda ikaripuka wakati wowote ya kukamatwa ndugu wa Rostam aitwae Ikram kwa kuhusika na ujangiri.

Huyu jamaa amekuwa akimiliki silaha na kuendeleza ujangiri nchini kwa manufaa ya wakubwa wengine walioko nyuma yake wa wenye maslahi flani.

Tetesi zinasema Mbunge Zitto Kabwe naye huenda yumo katika mtandao wa kunufaika na nyara hizo.

Taarifa kamili itawajia punde. Chini ni baadhi ya silaha na nyara hizo haramu.
 

Attachments

  • IMG-20181031-WA0018.jpg
    IMG-20181031-WA0018.jpg
    72.4 KB · Views: 35
  • IMG-20181031-WA0019.jpg
    IMG-20181031-WA0019.jpg
    70.4 KB · Views: 39
  • IMG-20181031-WA0026.jpg
    IMG-20181031-WA0026.jpg
    65.1 KB · Views: 38
Hahahaa!! Hivi thamani ya Vodacom Tanzania kwa sasa ni shilingi bilioni mia ngapi?! The question is: Mmiliki wa takribani 26% ya hayo mabilioni atakuwa tayari kumuona kaka yake anaozea jela kwa kesi ay tumilioni kadhaa?! Kaka ambae kwa namna moja au nyingine huwa anamtumia kwenye biashara zake kama ile ya kummilikisha tone la kampuni inayomiliki 26% ya Vocadom Tanzania!

Btw, yupo ndani au yupo nje kwa dhamana? Manake kwa hizo tuhuma anatakiwa kuwa ndani kwa sababu, mathalni kesi ya uhujumu uchumi nadhani haina dhamana!!!
 
Ni Tanzania pekee ambapo Mtu baada ya Kuikosoa Serikali anaaonekana anayo hatia, Sioni ajabu ata MAKONDA siku atakapoanza kumkosoa Baba yake atapelekwa kisutu na kupewa kesi ya vyeti Fake..
 
Jumatano siku ya kuzini, akili hua zinanirudia Alhamisi.
 
Ni Tanzania pekee ambapo Mtu baada ya Kuikosoa Serikali anaaonekana anayo hatia, Sioni ajabu ata MAKONDA siku atakapoanza kumkosoa Baba yake atapelekwa kisutu na kupewa kesi ya vyeti Fake..
kwa hiyo anayeikosoa Serikali hawezi kufanya uhalifu?
 
Back
Top Bottom