TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Kwa hiyo maRais wapo nje ya mfumo na mauji yanayotendeka hawayajui na hawajawahi kuyasikia?
 
Mtu kaenda kutekwa na watu wana bunduki, Pingu, na magari ambayo bila kuhoji ni yale yanayotumiwa na Serikali.

Kama hujui Mbowe angekua anaongoza magenge ya uhalifu, Serikali ingefurahi sana maana miaka yote wamekuwa wakitafuta kona ya kumbana wamuweke ndani.

Matukio ya utekaji yanaendeshwa na watu waliopo Serikalini. Nyenzo zote za utekaji ni mali za serikalini na zinakua accessed na watu waliopo serikalini

Edgar Mwakabela alipotekwa alipelekwa karakana ya Kituo cha polisi Oysterbay. Muda wote aliokua hapo, suala la chakula alihudumiwa na maaskari wa jeshi la Polisi.

Je Mbowe anaweza kufanya yote haya? Msijigeuze wajinga japo mmeshauvaa upumbavu.
 
Tlaatlaah haya ndiyo yanaendelea nchini sio bla bla. Sasa hakuna atakaye shikwa kwasababu tu huyu mzee alikuwa Chadema. Haya ndiyo mnaunga mkono iko siku watakuwa ndugu zenu ndiyo mtaelewa
kwanini haya yote yanafanyika kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani wa chadema tu?

na kwanini wahusika wa songombingo ya kabokamchizi ni kwa watu wa chadema pekee?

nafasi ya mtoa taarifa hizi wa Chadema ni ipi hasa hata aonekane kama vile alikuepo wakati wa utekaji, lakini pia yupo kama vile alikua akishuhudia mwisho wa tukio na matokeo ya utekaji?

na mbona matukio haya yanaongezeka zaidi wakati wa uchaguzi wa ngazi ya juu chadema?πŸ’

Kwa hali hii,
kuna anaempinga mwezake chadema alie salama kweli?

nadhani kuna haja ya uchunguzi yakinifu chadema πŸ’
 
Ni kweli inaumiza. Hii yote ni kwa ajili ya nini? Nipo tayari kwa ajili ya kuunga mkono maandamano yoyote yanayopinga mauaji ya namna hii.
Usijekujaribu kuandamana, Hawa watu wamejipanga, Dola ni zao, watawamaliza, ziko njia mbadala za kushughulika nao.
 
Huna adabu kna yanayoendelea usishangae wewe ukafuata!!kemea
 
NI jambo la kulaaniwa vikali!
 
Kuna msingi mzuri wa hoja hapa umejaribu kuujenga japo unaweza kupingwa vikali na watu fulani....kwanini iwe hiki kipindi na kwanini iwe kwa wafuasi wa Chama fulani tu?
 
Sio kila jambo la kuleta mzaha. Kuna masuala ya utani wa kivyama lakini kwenye suala hili jitajidi kuwa serious basi
 
Inasikitisha sana.............haki ya kuishi haiwezi kuthamanishwa na kitu chochote

Chanzo cha taarifa ya utekaji niliona twita kwa Bonny x-mayor,msiba pia nimeona kwa Bonny x-mayor......hata jamii forums ndiyo walitumia kama source......... binafsi inanipa mixed feelings
 
Kuna msingi mzuri wa hoja hapa umejaribu kuujenga japo unaweza kupingwa vikali na watu fulani....kwanini iwe hiki kipindi na kwanini iwe kwa wafuasi wa Chama fulani tu?
πŸ‘ŠπŸ’ͺtupo pamoja gentleman,

nakubali kupingwa kwa hoja, but why all this at a time of chadema elections?πŸ’
 
Katika hali yoyote ile, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi kuendelea kuwa ofisini hadi muda huu ni dharau na kejeli kubwa kwa Watanzania.

Mkuu wa Polisi pia afanye maamuzi magumu japo sioni kama ni magumu, yeye kuendelea kuwa katika nafasi hiyo pia ni aibu kwake na mzigo mzito.

Tunaelekea wapi kama taifa? Sijui!
 
This is Terrorism, targeted killings.

Mazee tuwaachie Nchi yao watatumaliza.

Mwenyezi Mungu akawalaani Wana wa Seruya na kusema Na Damu Yake Abneli iwe juu ya mikono yenu na uzao wenu woote.

Ktk ukoo wao paskose mtu mlemavu, ukoma njaa na tabu za hapa na pale.

Amina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…