TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Tabia ya viongozi kuchukulia wepesi mambo magumu kama haya ya utekaji,utesaji na uuaji si nzuri hata kidogo.Intelijensia mara zote ni wakinzani tu kwamba wataleta fujo.Lakini,hayo ya utekaji na uuaji intelijensia haina macho iyaone kabla?Nchi inaenda kuwa kiroja kabisa.
 
Mluu nimestushwa sana na member mwenzetu kujijasirisha na akafungua uzi kuwatuhumu CHADEMA kuwa wanahusika na hivi vifo.

Huu ujasiri na intention ya kuspin imelindwa na online mods.

Tupo kwenye hatari kubwa sana sana. Na watu wanaleta dhihaka na mabezo.

Umenena kweli
 
Hii kitu inamchafua sana Mh. Rasi Mama Samia, asipofanya maamuzi mazito kukemea haya yanayoendelea hii nchi itamfia mikononi mwake.

Very sad new indeed.
Naona kashtuka katoa pole kwa familia, muhimu aache kuwa muoga yeye kama amri jeshi mkuu avunje kikosi kazi husika na ikiwezekana wajulikane na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ili haki itendeke.
 
Hizi ni ndoto. Amkeni mfanye jambo
Kwa taarifa yako, kilichompata Jiwe nilionya 2015 wakati wanamkejeli Lowassa kuwa Ikulu sio wodi ya wagonjwa.

Nakumbuka niliandika kwa mafumbo nikawaonya CCM na mgombea wao na miaka 6 baadae yalitokea.

Ni bahati mbaya, baada ya muda mchache, ule uzi sikuuona tena hapa Jukwaani, nahisi mods waliufuta.
 
Usijekujaribu kuandamana, Hawa watu wamejipanga, Dola ni zao, watawamaliza, ziko njia mbadala za kushughulika nao.
Hakuna nguvu ya dola iliyowahi ishinda nguvu ya umma.

Kumalizwa hatabila kuandamana watakumaliza tu kwani hao waliouawa na kumalizwa waliandamana?

Leo mzee wetu, hatujui kesho ni nani? Inaweza kuwa wewe au mimi. Bila kupiga kelele, tutakuwa kama kondoo mbele ya Fisi mkuu.

Tanzania ni yetu sote.
 
Another sad sad day kwa Watanzania. Haitoshi kwa IGP au Mkuu wa Usalama kuujiuzulu. Waziri wa Mambo ya Ndani ni lazima awe wa kwanza kujiuzulu. Vyombo vya usalama haviwezi kujichunguza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…