TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

TANZIA Dar: Ali Mohamed Kibao, kiongozi wa CHADEMA auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana

Anita Makirita nilikwambia ukienda haurudi ukirudi ushakua Maiti, Pole sana kwa wafiwa, ndugu, Jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao, inlalilah wa inlalilah rajiuni Bwana katoa Polisibubu wametwaa, marehemu apumzike anapostahiri
Ongezea nyama story yako tufunguwe codes!!
 
Tumekuwa makondoo sana , tunaona mwenzetu anatekwa na sisi tunaona kawaida bila kuchukua hatua , hao wahuni ilibidi wabanwe waonyeshe vitambulisho na warrant ya mahakama ya mtu kukamatwa na waje na sare kamili za polisi na ikiwezekana watu kadhaa wawafuatilie na kuhakikisha huyo aliyekamatwa amepelekwa na kuingizwa kituoni na si vinginevyo ,hii ya wapuuzi tu wanakuja na kuteka watu na kujiongezea kwamba ni polisi au usalama huu ni useng£ kabisa kinyume na hivyo wapigiwe kelele za wezi na wapigwe na kuchomwa moto kama majambazi au wezi wengine mitaani wanavyofanyiwa au mtu anayekamatwa naye ajihami kivyovyote na kuhakikisha hakamatwi , .

Kuna arrest procedures na zinajulikana , aisee watz tuache ukondoo
Wabongo ni waoga sana labda ni kwa sabab uhuru wao waliupata kwa njia za makaratasi
 
Kwa yanayoendelea humu nchini kwa sasa ni obviously hata mimi ninaweza tengeneza kikosi cha kuteka watu huku nijiita polisi au usalama , na hao watu naenda kuwafanyia blackmail , kuwang'oa viungo ,kuwaua au kudai ransom Kwa ndugu na jamaa ili huyo mtu aachiliwe .
Hii ni disaster ,hii tabia ilipamba moto kipindi cha awamu ya tano na huu ni mwendelezo ,subhuman species wanaongoza hili taifa
Kitu ambacho nilishangaa Ni spika wa Bunge kutokubali Kuijadili hii hoja zaidi ya mara Mbili kuna tatizo kubwa sana tunalitengeneza
 
Hii taarifa imeniumiza sana. Polisi waliahidi kufanya uchunguzi kuhusu hili, bahati mbaya majibu hayajifika na Mzee hayupo tena.

20240908_103744.jpg
 
Anaandika Boniyai kutoka Account yake ya X
View attachment 3090046
View attachment 3090047

======


Ali Mohamed Kibao Ameuawa

Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu umekutwa hospitali ya Mkoa wa Kinondoni,Mwananyamala katika chumba cha kuhifadhia maiti mwili wake ukiwa UMEHARIBIWA VIBAYA SANA.

Mwili wa ALI MOHAMED KIBAO ulikutwa umetupwa jana alfajiri maeneo ya UNUNIO (jirani na viwanja vya NSSF) ukiwa na majereha makubwa sehemu za usoni kiasi ndugu zake walipata tabu kuutambua kirahisi.

ALI MOHAMED KIBAO alikamatwa na watu wanao dhaniwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi eneo la TEGETA, mbele ya Jengo la KIBO COMPLEX baada ya gari mbili za Jeshi za Polisi za Landcruiser hardtop nyeupe kuzuia (block) basi la TASHIRIF lenye namba T 343 EES alilokuwa amepanda ALI MOHAMED KIBAO kutoka Dar es saalam kuelekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.

Kwa bahati nzuri wakati wote wa tukio likitendeka ndani ya gari palikuwa na askari wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani (Traffic) ambaye alikuwa kiti cha mbele kama abiria na alishuhudia tukio lote, anatambulika kama MACHIWA anayepatikana kwa namba 0652484802.

Namba ya simu aliyokuwa anatumia ALI MOHAMEDKIBAO ni +255 624 724 247 mpaka wakati anatekwa na kwenda kuuwawa,pia ndiyo namba ambayo mara kadhaa waliomteka walikuwa wakimpigia kuhakiki kama ni yeye.

Kwa mujibu wa wenyeji wa UNUNIO ambao ni walima mchicha, wanasema Jana asubuhi walitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi baada ya Kuona mwili wa Mtu mzima, mweupe mwenye asili ya Kiarabu ambaye baadae Jana jioni ndugu waliutambua kuwa ni mwili ALI MOHAMED KIBAO ukiwa na majeraha.

Kabla ya umauti wake ALI MOHAMED KIBAO aliwahi kuwa afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akastaafu na kujiunga na CCM,baadae akachaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Tanga wakati wa Rais Kikwete,na baadae alijiunga CHADEMA.

Baada ya mauaji haya ya Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA na Msaidizi wa Katibu Mkuu kuwawa idadi ya Viongozi wa CHADEMA wakiotekwa inaongezeka
1. Dioniz Kipanya 2. Kombo Bwana Twaha 3. Godwin Mlay 4. Deusdedith Soka 5. Frank Mbise.


Soma Pia:
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
Huenda Msigwa anatumika(collaborator).
 
TUSALI HII SALAA OMBA REHEMA KWA AJILI YAKO YA FAMILIA YAKOO NA WOTE WALIOHUZUNIKA NA MSIBA HUU OMBA REHEMA KWA AJILI YATAIFA LETU
 

Attachments

  • Screenshot_20240908-121028_Chrome.jpg
    Screenshot_20240908-121028_Chrome.jpg
    397.7 KB · Views: 3
Tunakotaka kufika tutafika tu Hait,Mexico na Colombia nao nafikiri walianza hivi hivi ila wao bora walijua ni makundi ya wauza madawa.Sasa huku hatujui ni kina nani wanahusika.Serikali Jamani tunawalipa mishahara kwa ajiri ya kulinda usalama wetu na tupate huduma hili swala la utekaji fanyeni uchuunguzi tutazalisha magaidi si mda mrefu wote hatutakua salama.Please viongozi hebu tuwaonee huruma watoto wetu hivi tunawaachia Tanzania yenye damu 😭😭😭
 
Sina la kuandika..
Machozi yamenitoka ingawa sikuwahi mfahamu.
MUNGU tunusuru
Mimi mwenyewe sikuwhi kumjua ila kama binadamu nimestushwa mnoo na kiteelndo hiki...
au huyu kamanda alikuwa na kitengo kizito ndani ya chadema kuwadukuwa hawa watekaji?
 
Back
Top Bottom