Dar: Aliyedai kuporwa Tsh. Milioni 60 aonesha alipozificha

Dar: Aliyedai kuporwa Tsh. Milioni 60 aonesha alipozificha

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Deodatus Thadei Luhela, Mhasibu wa Kampuni ya ‘Your Home Choice’’ amekamatwa kwa kutoa taarifa za uongo akidai Majambazi walimjeruhi na kumpora fedha za Mwajiri wake.

Mtuhumiwa alifungua kesi ya unyang'anyi kituo cha Polisi Chang’ombe, baada kubanwa kwa maswali ya Askari, aliwapeleka Chanika Kitunguu na kuonesha fedha hizo.

Jeshi la Polisi limewatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani.

=====================

“Tukio limetokea November 14,2022 eneo la Chang’ombe Temeke ambapo Mtuhumiwa huyo alidai tarehe hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi alikamatwa na Majambazi wawili waliokuwa na gari nyeusi baada ya kumtishia kwa silaha baadae akaingizwa kwenye gari ambapo walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni, na kumpora fedha alizokuwa nazo na baadae kumtupa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi alijikongoja hadi kituo cha Polisi kidogo cha Gongo la Mboto ambako alipewa PF. 3 kwaajili ya matibabu.

“Baada ya tukio hilo majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa huyo alifungua kesi kituo cha Polisi Chang’ombe ya unyang’anyi na kuporwa tsh 60,000,000, Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam walimuhoji kwa kina na kubaini kuwa taarifa hizo zilikuwa ni za uongo na ilipofika tarehe 15/11/2022 majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa aliwaongoza Askri hadi Chanika Kitunguu alipokuwa amezificha pesa hizo”

“Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa Maafisa wa Serikali kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani”

POLISI KANDA MAALUM DAR
 
Hakukua na namna yoyote ya kupanga zaidi ya kuchukua fedha na kuzipeleka kunakohusika na kusubiri mshahara mwisho mwezi.

Huwezi kuwa salama uwadanganye polisi swala lililohusu silaha.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hiyo ndo hasara ya tamaa!! Kwa Nini usitosheke na mshahara wako???
1 Timotheo 6:6
Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.

1 Timotheo 6:7
Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;

1 Timotheo 6:8
ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.

1 Timotheo 6:9
Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.

1 Timotheo 6:10
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
 
Jamaa alikosea kuchora mchoro. Nasisitiza unapotaka kufanya tukio la janja janja au kama ilo nenda kajikabidhi kwa polisi kwanza. Wao ndio watakusaidia namna ya kuishi kimaster.

Pia jamaa anaonekana anamkono mfupi alitaka kula million 60 peke yake
 
Back
Top Bottom