Dar: Aliyedai kuporwa Tsh. Milioni 60 aonesha alipozificha

Dar: Aliyedai kuporwa Tsh. Milioni 60 aonesha alipozificha

Unadhani ushahidi dunia nzima unapatikana kwa maongezi? Au unadanganywa na watu wa haki za binadamu? Halafu polisi japo wana madhaifu lakini kwenye kudeal na wahalifu wao hua wana ushahidi kabisa, na ndio maana kipindi cha magu walitumia elimination method unafuatwa kwako unapotezwa kimyakimya kama sio jambazi na haufanyi uhalifu kamwe hao askari hutokutana nao,
Nakubaliana na wewe 100%. Polisi kama sio mhalifu hawanaga muda kabisa.
 
Bora angeamua kutimka tu na mzigo wote,
Huo mchezo wa kitoto sana,
Police walishauliza kwenye network zao wakajuwa kabisa hakuna robbers aliyepiga pesa hizo Kwa siku hyo,jamaa mzushi ..

Police wa kitanzania umwambiye Kuna pesa mahali akili zote zinahamia kwenye pesa.

Ktk kesi za ujambazi hata police wana network fulani fulani na hawa robbers na wanajuwana vizuri sana..

Linapotokea tukio sehemu fulani,
kuna watu ambao ni retired robbers,,
au hata kama bado wapo kwenye mtandao huo,
Ambao wana link na matukio mengi sn mjini.

Police hufanya mawasiliano na hawa wahalifu na kuuliza kama wanatetesi zozote?
Au retired robbers watabanwa mwishowe wanapata link ya tukio.

Kama tukio la kweli watasema, kweli jamaa wamepiga ila ni watu wa sehem fulani

Ipo hivi,,,,
Kabla ya tukio lolote la kihalifu kufanyika.
Kwanza lazima watu wakutane wajadili deal mezani,,

Mleta deal analeta deal mezani,,
watajadili na kupanga mikakati.

Hapo watatafutwa robbers wanaoweza kufanya kazi hiyo.,,

Na hapo wakati wa mtafutano ndy hapo baadae Siri zinakuja kuvuja na kuwafikia police..,,

Hapo ndy hupelekea watu kuuzana na kukamatwa na Police.

Utasikia police wanaosema "tumepata taarifa kutoka Kwa raia mwema,"
Kumbe Kuna robbers fulani wamesaliti wenzao.
 
Deodatus Thadei Luhela, Mhasibu wa Kampuni ya ‘Your Home Choice’’ amekamatwa kwa kutoa taarifa za uongo akidai Majambazi walimjeruhi na kumpora fedha za Mwajiri wake.

Mtuhumiwa alifungua kesi ya unyang'anyi kituo cha Polisi Chang’ombe, baada kubanwa kwa maswali ya Askari, aliwapeleka Chanika Kitunguu na kuonesha fedha hizo.

Jeshi la Polisi limewatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani.

=====================

“Tukio limetokea November 14,2022 eneo la Chang’ombe Temeke ambapo Mtuhumiwa huyo alidai tarehe hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi alikamatwa na Majambazi wawili waliokuwa na gari nyeusi baada ya kumtishia kwa silaha baadae akaingizwa kwenye gari ambapo walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni, na kumpora fedha alizokuwa nazo na baadae kumtupa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi alijikongoja hadi kituo cha Polisi kidogo cha Gongo la Mboto ambako alipewa PF. 3 kwaajili ya matibabu.

“Baada ya tukio hilo majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa huyo alifungua kesi kituo cha Polisi Chang’ombe ya unyang’anyi na kuporwa tsh 60,000,000, Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam walimuhoji kwa kina na kubaini kuwa taarifa hizo zilikuwa ni za uongo na ilipofika tarehe 15/11/2022 majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa aliwaongoza Askri hadi Chanika Kitunguu alipokuwa amezificha pesa hizo”

“Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa Maafisa wa Serikali kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani”

POLISI KANDA MAALUM DAR

Hizi mambo wanaweza watu wa kaskazini tu, akiziwaza zile hela anavumilia pigo lolote
 
Mtaalam wa kupanga atupatie mbinu za kutokamatwa maana wote mnamlaumu mtuhumiwa kwamba hajui kupanga tukio.
1. Ukishajiteka cha kwanza unazima simu na kuitenganisha na laini kisha kila kimoja unakitupa eneo tofauti

2. Kafiche mzigo mahali unapopaamini

3. Unatumia boda tofauti kama tatu hivi ama zaidi kukufikisha nje ya mji

3. Utakaposhuka tembea umbali wa kilometre moja ama zaidi kwenye vichaka

4. Toa kichupa chako kidogo chenye dawa ya kulevya kisha kitupe mbali

5. Utaokotwa na was a maria we ma name kugikishwa hospital..
 
jamaa alishindwa kutumia suspense account ... ambayo vijana wengi wamekuwa wakitumia kufanyia mambo yaooo

mchongo umeshindikana ... kuzidi kuambulia maumivu
 
Back
Top Bottom