Dar: Aliyedai kuporwa Tsh. Milioni 60 aonesha alipozificha

Dar: Aliyedai kuporwa Tsh. Milioni 60 aonesha alipozificha

Deodatus Thadei Luhela, Mhasibu wa Kampuni ya ‘Your Home Choice’’ amekamatwa kwa kutoa taarifa za uongo akidai Majambazi walimjeruhi na kumpora fedha za Mwajiri wake.

Mtuhumiwa alifungua kesi ya unyang'anyi kituo cha Polisi Chang’ombe, baada kubanwa kwa maswali ya Askari, aliwapeleka Chanika Kitunguu na kuonesha fedha hizo.

Jeshi la Polisi limewatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani.

=====================

“Tukio limetokea November 14,2022 eneo la Chang’ombe Temeke ambapo Mtuhumiwa huyo alidai tarehe hiyo majira ya saa 3:30 asubuhi alikamatwa na Majambazi wawili waliokuwa na gari nyeusi baada ya kumtishia kwa silaha baadae akaingizwa kwenye gari ambapo walimjeruhi mkono wa kushoto na shavuni, na kumpora fedha alizokuwa nazo na baadae kumtupa maeneo ya Gongo la Mboto njia panda ya Pugu na Mbezi alijikongoja hadi kituo cha Polisi kidogo cha Gongo la Mboto ambako alipewa PF. 3 kwaajili ya matibabu.

“Baada ya tukio hilo majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa huyo alifungua kesi kituo cha Polisi Chang’ombe ya unyang’anyi na kuporwa tsh 60,000,000, Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam walimuhoji kwa kina na kubaini kuwa taarifa hizo zilikuwa ni za uongo na ilipofika tarehe 15/11/2022 majira ya saa 8 :00 mchana Mtuhumiwa aliwaongoza Askri hadi Chanika Kitunguu alipokuwa amezificha pesa hizo”

“Jeshi la Polisi linawatahadharisha Wananchi juu ya tabia ya kutoa taarifa za uongo kwa Maafisa wa Serikali kuwa ni kosa na ikibainika watachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja kufikishwa Mahakamani”

POLISI KANDA MAALUM DAR
Story za tafuta hela zilimvuruga maskini sasa kaharibu kabisa..
Vijana tutafute hela😀😀😛
 
Hiyo kampuni systems zao zina shida, muhasibu anatembeaje na hela nyingi hivyo!!!!
 
Mwamba katuangusha.
Alishindwa kujipanga mpaka mwisho na kuvumilia kichapo
Sio mishe zake huyo na ni mwoga sana..
Huyo sio mwamba ni mtoto wa mchungaji alafu alitaka kuact umwamba..
Maboss wengine wachawi pesa zao huibi kizembe zembe..🤣🤣😆
 
Mtaalam wa kupanga atupatie mbinu za kutokamatwa maana wote mnamlaumu mtuhumiwa kwamba hajui kupanga tukio.

Mimi sio askari ila huyo muhasibu story yake nisingeikubali..

Jambazi huwa hapotezi muda, sasa jambazi gani atembee na muhasibu kwenye gari mpaka akamtupe mbele mbele bila kumuua
 
Mtaalam wa kupanga atupatie mbinu za kutokamatwa maana wote mnamlaumu mtuhumiwa kwamba hajui kupanga tukio.

Alitakiwa ahakikishe anaandaa watekaji kwanza bila kutumia simu kabisa, angetafuta hata mabaunsa walioshiba watatu, angehakikisha wale jamaa wanafahamu muda halisi na wajulishwe kua eneo atalokua anatoka kuna walinzi wenye silaha au hawapo na jirani na pale kuna mazingira gani, je kituo cha polisi kiko mbali au karibu, hapo wangetafuta silaha kama mapanga na bunduki feki maana mchongo wangeujua 100% , na baruti kali za kulipua ili kutisha, ahakikishe wavamiaji wanakua na pikipiki boksa namba wanazitoa na juu wavae mask na pullneck ambapo baada ya uvamizi wataondoka kwa kasi sana dakika tatu nyingi wanatakiwa wabadili manguo yale wachome moto then wasogee mbele wabandike namba za pikipiki zao, timing ni atekwe bosi na mfanyakazi hivo pesa inachukuliwa mbele ya Bosi, yeye na watu wake watakutana mbele ya safari na pesa haingizi mwenye akaunti yake, ndio hivo mpango ukivuja ajijue lakini hadi hapo pesa ingeondoka kilaini sema ndio hivo
 
Huyu jamaa hopeless kabisa!
Si bora hata angekodi majambazi original wakaandaa script angepigwa hata ka risasi ka bega na watu wasingestukia kuliko kufanya upuuzi kama huu anakamatwa kizembe sana

Ni mwehu hivi sijui wanawaza nini? Polisi waamue kukupata wakukose labda hautishii amani kisawasawa kwa wajinga kama hao kudakwa sekunde tu kwanza eti walimteka wakamsafirisha zaidi ya kilomita kumi, hata kujipa madawa ya kulevya hakuweza halafu sijui hawajui mabosi anavokuagiza pesa nyuma anakuwekea spy wa kukufuatilia unaenda wapi wewe bila kujua unafuatwa na bodaboda hadi unakoenda
 
Mmh, najiuliza hadi akaamua kuwapeleka, ni kibano cha aina gani alipata, daah

Huyo shot za kwenye matako tu anasema kila kitu, yaani anapigwa virungu kwanza magotini na kwenye joint za mikono analegea hajiwezi, anamwagiwa maji huku anagongwa bapa za upanga mgongoni, akiinuliwa yuko uchi anatandikwa shoti za umeme matakoni lazima aseme tu
 
Nasoma comment unapata picha aina ya watu wa jamhuri ya danganyika.
Viongozi/watawala wanatoka miongoni mwetu ndio hawahawa wachangiaji wa JF, ndugu na watu wa JF n.k
Tuna safari isiyofika mwisho.
 
Back
Top Bottom