DAR: Amuua mtoto wa mdogo wake kwa kipigo, aufunga mwili kwenye ndoo kisha kuutupa Ubungo

DAR: Amuua mtoto wa mdogo wake kwa kipigo, aufunga mwili kwenye ndoo kisha kuutupa Ubungo

Sijui ndio kulewa Asubuhi subuhi ila chozi limenitoka, everything is wrong kwenye hili tukio. Kipigo Kwa 2 yrs old,kipigo kikali mpaka kufa,kuufinyanga mwili kwenye ndoo na kwenda kuutupa..

kusema kweli polisi wetu japo wanazingua ila wanakumbana na vitu vingi sana vya kushtua. Imagine polisi anayeshughulikia kesi hii kisaikolojia inamuathiri vp. Poleni sana polisi hakika mnakumbana na vingi sana,poleni sana.
 
Kwani nimekataa kuwa huko watu walikufa , unaushamba za mijadala na kukurupuka kama kibinti kilichovunja ungo Jana


USSR
Yaani hii dunia ya kijinga sana hasa kwa kizazi hiki cha kitumwa ambacho hakijui historia yake,kilichodanganywa na historia za filamu za kimagharibi na miziki.

Leo wanaona hiyo vita ya Urusi kama ya Dunia nzima,na huyo Rais wa Ukreini na wazungu wameteka akili za waafrika wajinga wakati ingekuwa inchi ya Africa au Asia usingesikia watu hata kulialia
 
Sijui aliwaza nn naumia sana kuuwa watoto Kuna lijamaa linaitwa Putin linauwa watoto kila siku


USSR
acha ulongo ,leo kauwa wangapi ?na jana wangap?
ya putin yaache kama ni matured hakuna vita iliyoua watoto wengi kama syria,iraq,libya ,afughanstan :
ACHANA NA PROPAGANDA ZA WEST
 
Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne. Mtuhumiwa huyo LATIFA BAKARI (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side UBUNGO.

Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa. Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
Pongezi Sana Kwa Majirani Kwa Kujali...
 
Not all women are meant to be mothers.

Some women are the devils immediate agents here on earth.

Sheria ifate mkondo wake jamani hatuna mengi ya kuongea.
 
Sijui aliwaza nn naumia sana kuuwa watoto Kuna lijamaa linaitwa Putin linauwa watoto kila siku


USSR
Li Bush liliua Iraq na afghanistan, Li Obama's likaenda Libya kumuua Babu yako Ghadafi.
 
Kubeba lile tumbo adi miezi 9 ifike,ije ufe ya kujifungua yale mawazo ya je ntamaliza salama au?alafu mtoto anafika miaka 2 ndugu yako anamuua?
Yesu amfariji mama mtoto!
Malaika wa Mungu apumzike kwa amani!
 
Watu wana roho za kishetani sana kuna hii moja msichana wa kazi alichokifanya mimi mwenyewe chozi limenitoka,ni Oman house girl ni mu indonesia,wakati mwingine cjui tuamini mashetani twaishi nao?
Angalia video
 
Sijui aliwaza nn naumia sana kuuwa watoto Kuna lijamaa linaitwa Putin linauwa watoto kila siku


USSR
Hapo kuna mengi ya mambo yaliyoingiliana na kuivuruga kabisa saikolojia ya huyo muuwaji!

Chanzo huenda ni kuadhibu mtoto kwa nia njema, sasa baada ya kugundua kaua, ndiyo hivyo vipande vingine vya mnyororo vikajiunga.
 
Back
Top Bottom