Dar: Anayedaiwa kumuua mwanafunzi wa UDSM akamatwa, akiri kufanya tukio hilo

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na operasheni kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu waliotenda makosa ya kijinai ya siku za nyuma katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.​

Katika hatua hiyo Polisi wamemkamata GADI DAUDI@ tito Jeshi la mtu mmoja (28) Mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za kumuua JULIUS FREDRICK (22) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumpora simu yake ya mkononi .Tukio hilo lilitokea tarehe 16/07/2022 majira ya saa kumi usiku huko eneo la karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam baada ya kumvizia, kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kupora vitu vyake ikiwemo simu na kumsababishia kifo.

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina na tarehe 27/07/2022 lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza, Kinondoni, baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyanganyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mhalifu sugu ambaye amekuwa akifanya matukio ya kiuhalifu maeneo ya Mlimani city, Mwenge na Kawe, na aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA kesi No. 256/2020 na kufungwa miaka 30 kuanzia tarehe 6 Julai 2020, na aliachiwa huru Aprili 2022 kwa sababu za kisheria baada ya kukata rufaa.

Tarehe 1.8.2022 majira ya saa kumi na nusu jioni Mtuhumiwa alikubali kuwapekeleka askari kuwaonesha alipoficha silaha anazotumia katika uhalifu na simu ya marehemu aliyoipora katika vichaka vilivyopo eneo la katikati ya Mlimani city na Hostel za Magufuli.

Baada ya kufika eneo hilo alikurupuka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye vichaka vya ndani zaidi. Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha kusimama lakini alikaidi na hivyo kulazimika kumzuia kwa risasi iliyomjeruhi kwenye paja la mguu wa kushoto, kuanguka chini na kukamatwa kutoka katika jaribio la kutoroka chini ya ulinzi huku akikabiliana na tuhuma nzito za mauaji . Alipelekwa hospitali kwa matibabu. Eneo hilo Polisi imepata panga moja, sime, bisibisi na simu mbili za mkononi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam liendelea na msako mkali kuwakamata wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na malengo ni kuhakikisha watu wanafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama , bila hofu na kwa kuzingatia sheria za nchi.

Muliro J. MULIRO – ACP​

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
Murder case siyo mchezo ni very serious hata kwenye nchi zenye weak judiciary system kama yetu. Hongereni Sana polisi kwa kazi nzuri. Ila mmenisikitisha kwa Nini mngesema tu alijaribu kutoroka tukamfumua kichwa kisogoni na risasi. Siyo wakucheleweshwa huyo atafungwa na kukata rufaana kurudi uraiani.
 
Ila pale kipande cha kutoka TCRA usawa wa hosteli za Magufuli kwann usiku hakuna taaa yan taa za barabarani zote haziwaki uzembe
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na operasheni kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu waliotenda makosa ya kijinai ya siku za nyuma katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.​

Katika hatua hiyo Polisi wamemkamata GADI DAUDI@ tito Jeshi la mtu mmoja (28) Mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za kumuua JULIUS FREDRICK (22) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumpora simu yake ya mkononi .Tukio hilo lilitokea tarehe 16/07/2022 majira ya saa kumi usiku huko eneo la karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam baada ya kumvizia, kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kupora vitu vyake ikiwemo simu na kumsababishia kifo.

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina na tarehe 27/07/2022 lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza, Kinondoni, baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyanganyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mhalifu sugu ambaye amekuwa akifanya matukio ya kiuhalifu maeneo ya Mlimani city, Mwenge na Kawe, na aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA kesi No. 256/2020 na kufungwa miaka 30 kuanzia tarehe 6 Julai 2020, na aliachiwa huru Aprili 2022 kwa sababu za kisheria baada ya kukata rufaa.

Tarehe 1.8.2022 majira ya saa kumi na nusu jioni Mtuhumiwa alikubali kuwapekeleka askari kuwaonesha alipoficha silaha anazotumia katika uhalifu na simu ya marehemu aliyoipora katika vichaka vilivyopo eneo la katikati ya Mlimani city na Hostel za Magufuli.

Baada ya kufika eneo hilo alikurupuka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye vichaka vya ndani zaidi. Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha kusimama lakini alikaidi na hivyo kulazimika kumzuia kwa risasi iliyomjeruhi kwenye paja la mguu wa kushoto, kuanguka chini na kukamatwa kutoka katika jaribio la kutoroka chini ya ulinzi huku akikabiliana na tuhuma nzito za mauaji . Alipelekwa hospitali kwa matibabu. Eneo hilo Polisi imepata panga moja, sime, bisibisi na simu mbili za mkononi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam liendelea na msako mkali kuwakamata wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na malengo ni kuhakikisha watu wanafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama , bila hofu na kwa kuzingatia sheria za nchi.

Muliro J. MULIRO – ACP​

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
kwahiyo kaiba simu na kuitelekeza hapo kichakani siku zote?
 
Eti aliachiwa kwa rufaa ya kosa la unyanganyi na anarudia tena kufanya unyanganyi
 
mwanafunzi wa chuo ni raia tu kama wewe.

saa 10 za usiku toka umezaliwa mpaka ulipofikia imekukutia ndani kwako?

hujawahi kutoka mida hiyo kuwahi basi usafiri,kuenda kuona wagonjwa,night clubs nk.?

kwahiyo kwa kuwa ni saa 10 usiku halali yake kuuliwa?
Msamehe bure wa mkoani huyo anaamshwa na miale ya jua la asubuhi.

Saa 10 usiku unakuta wanafunzi wa sekondari wapo vituoni anasubili daladala za kuunga awahi shule.
 
Afande Mulilo, ina maana mlimpeleka bila kumtia pingu? Eleza ukweli kwamba hamkutaka kusumbuana mahakamani maana anaweza kutoka kwa technicalities
Huyo wangemuua tu, Polisi Ni wabaya wakiuwa Raia wasio na hatia au wanasiasa, ila Haya majambazi nawa support, imagine maumivu aliyosababisha kwa familia ya huyo dogo !!!

Sema Haya majambazi yanaendaga kwa waganga,Kuna poti alimuua jambazi Miaka ya zamani katika majibizano ya Risasi, yule poti alianza Kama kuwa mwehu, ikabidi apelekwe kwa mganga ndio akapona
 
Chuo kilifungwa jana yake tar 15 Julai, mi nadhani dogo alidamka ili kuwahi mabasi ya mikoani
Yaani mida hiyo inabidi wawe wanatembea kimakundi. Kuna vibaka wengi sana maeneo hayo
Huyo wangemuua tu, Polisi Ni wabaya wakiuwa Raia wasio na hatia au wanasiasa, ila Haya majambazi nawa support, imagine maumivu aliyosababisha kwa familia ya huyo dogo !!!

Sema Haya majambazi yanaendaga kwa waganga,Kuna poti alimuua jambazi Miaka ya zamani katika majibizano ya Risasi, yule poti alianza Kama kuwa mwehu, ikabidi apelekwe kwa mganga ndio akapona
Alifungwa miaka 30 akatumikia mwaka 1 akashinda kesi, sheria zetu hizi!!
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na operasheni kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu waliotenda makosa ya kijinai ya siku za nyuma katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.​

Katika hatua hiyo Polisi wamemkamata GADI DAUDI@ tito Jeshi la mtu mmoja (28) Mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za kumuua JULIUS FREDRICK (22) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumpora simu yake ya mkononi .Tukio hilo lilitokea tarehe 16/07/2022 majira ya saa kumi usiku huko eneo la karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam baada ya kumvizia, kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kupora vitu vyake ikiwemo simu na kumsababishia kifo.

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina na tarehe 27/07/2022 lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza, Kinondoni, baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyanganyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mhalifu sugu ambaye amekuwa akifanya matukio ya kiuhalifu maeneo ya Mlimani city, Mwenge na Kawe, na aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA kesi No. 256/2020 na kufungwa miaka 30 kuanzia tarehe 6 Julai 2020, na aliachiwa huru Aprili 2022 kwa sababu za kisheria baada ya kukata rufaa.

Tarehe 1.8.2022 majira ya saa kumi na nusu jioni Mtuhumiwa alikubali kuwapekeleka askari kuwaonesha alipoficha silaha anazotumia katika uhalifu na simu ya marehemu aliyoipora katika vichaka vilivyopo eneo la katikati ya Mlimani city na Hostel za Magufuli.

Baada ya kufika eneo hilo alikurupuka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye vichaka vya ndani zaidi. Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha kusimama lakini alikaidi na hivyo kulazimika kumzuia kwa risasi iliyomjeruhi kwenye paja la mguu wa kushoto, kuanguka chini na kukamatwa kutoka katika jaribio la kutoroka chini ya ulinzi huku akikabiliana na tuhuma nzito za mauaji . Alipelekwa hospitali kwa matibabu. Eneo hilo Polisi imepata panga moja, sime, bisibisi na simu mbili za mkononi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam liendelea na msako mkali kuwakamata wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na malengo ni kuhakikisha watu wanafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama , bila hofu na kwa kuzingatia sheria za nchi.

Muliro J. MULIRO – ACP​

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
Hii ni kutuonesha mambo yamebadilika baada ya teuzi? Nguvu za soda! Ni wale wale tu.
 
Back
Top Bottom