edwayne
JF-Expert Member
- Apr 5, 2013
- 8,919
- 9,797
Tena ya kichwaKununua simu used wajiweka kwenye hatari ya kupewa kesi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena ya kichwaKununua simu used wajiweka kwenye hatari ya kupewa kesi
Uzembe sana, sanaa yaniKuna Polisi analaumiwa hapo kwanini kazi haikuisha mapema. Sema jamaa ana bahati sana sio siku yake
sa kumi kwa dar mbona ni asubuh,mi wakati nasoma chuo nilikuwa naamka sa kumi naenda sokoni kununua matunda ya kuuza (nilikuwa sina boom na kudanga siwezi)SAA 10 za usiku mwanafunzi unatoka wapi?
Ile id nyingine yenye picha ya Nyerere umeitelekeza..?Ila za Hao majambazi wanaochinja wanachuo ndio ziko straight??
SAA 10 za usiku mwanafunzi unatoka wapi?
Upo sahihi ila nchi hii hii kuna mitaa kuanzia SAA 4 usiku hukatizi. Njoo TandikaHii nchi huru jamaniii
Mkuu kuna danger zones kama Mburahati, Tandika, Tabata kisiwani n.kmbona hakuna Sheria inayokataza mwisho wa kutembea usiku.
Kikubwa usivunje Sheria za nchi.
Nchi HURU.tusiwekeane mipaka
Ila huyo polisi aliyempiga risasi ya paja HANA SHABAHA
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yakeHow kapona huyu? Vibaka wametamalaki kila kona, anzeni fyeka fyeka wakanywe na mama zao kama wanataka kuishi.
Sime na bisi bisi nazo ni Silaha za moto?Kibaka anakuwa na silaha ya moto?
And millions of Tanzanians believed that story, that's the tragedy. Sad statement about us more than the police.Mkuu kwangu police hapa wameongopa,hakuna ukweli hapa kabisa ,huwezi kwenda site na suspect (murder)bila back up ya kutosha au bila pingu za miguuni, it's craze wenzetu mpaka wanatumia tag kwa suspect
Kesi ikishafika mahakamani,polisi hausiki tenaSasa kufungwa miaka 30 na kuachiwa kwa rufaa kwani ushahidi ulikuwa na shaka.
Sometimes polisi wakiamua wanaweza.
Mtu kuhukumiwa miaka 30 anakaa mwaka 1 anatoka haijaanza leoAliachiwa baada ya mzee baba kupumzika... Huu msimu wa mtemi hangaya miyeyusho
Saa 10 ni alfajir sio usikuSAA 10 za usiku mwanafunzi unatoka wapi?
Murder case, no discussionJeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na operasheni kali ya kuzuia vitendo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu waliotenda makosa ya kijinai ya siku za nyuma katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Katika hatua hiyo Polisi wamemkamata GADI DAUDI@ tito Jeshi la mtu mmoja (28) Mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za kumuua JULIUS FREDRICK (22) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumpora simu yake ya mkononi .Tukio hilo lilitokea tarehe 16/07/2022 majira ya saa kumi usiku huko eneo la karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam baada ya kumvizia, kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili, kupora vitu vyake ikiwemo simu na kumsababishia kifo.
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina na tarehe 27/07/2022 lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza, Kinondoni, baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyanganyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam, Uchunguzi wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mhalifu sugu ambaye amekuwa akifanya matukio ya kiuhalifu maeneo ya Mlimani city, Mwenge na Kawe, na aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA kesi No. 256/2020 na kufungwa miaka 30 kuanzia tarehe 6 Julai 2020, na aliachiwa huru Aprili 2022 kwa sababu za kisheria baada ya kukata rufaa.
Tarehe 1.8.2022 majira ya saa kumi na nusu jioni Mtuhumiwa alikubali kuwapekeleka askari kuwaonesha alipoficha silaha anazotumia katika uhalifu na simu ya marehemu aliyoipora katika vichaka vilivyopo eneo la katikati ya Mlimani city na Hostel za Magufuli.
Baada ya kufika eneo hilo alikurupuka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye vichaka vya ndani zaidi. Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha kusimama lakini alikaidi na hivyo kulazimika kumzuia kwa risasi iliyomjeruhi kwenye paja la mguu wa kushoto, kuanguka chini na kukamatwa kutoka katika jaribio la kutoroka chini ya ulinzi huku akikabiliana na tuhuma nzito za mauaji . Alipelekwa hospitali kwa matibabu. Eneo hilo Polisi imepata panga moja, sime, bisibisi na simu mbili za mkononi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam liendelea na msako mkali kuwakamata wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na malengo ni kuhakikisha watu wanafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama , bila hofu na kwa kuzingatia sheria za nchi.
Muliro J. MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.