Dar: Bweni shule ya Ilala Islamic laungua moto, wanafunzi 3 wafariki

Dar: Bweni shule ya Ilala Islamic laungua moto, wanafunzi 3 wafariki

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,487
1593858593833.png

Wanafunzi watatu wamefariki dunia baada ya Moto uliozuka usiku wa kuamkia leo kuunguza bweni la shule ya sekondari ya Ilala Islamic iliyopo eneo la mtaa wa Arusha Ilala.

Mpaka sasa chanzo Cha Moto huo hakijajulikana ambapo wanafunzi wote wa shule hiyo wamehamishiwa kwenye shule ya msingi ya Ilala Islamic iliyopo jirani na eneo hilo kwa ajili ya kupatiwa hifadhi wakati taratibu zingine zikiendelea.

Aidha jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama imefika katika eneo hilo ambapo sasa inaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha moto huo.

Shule hiyo ya sekondari ya Ilala Islamic ina takribani wanafunzi 350 wa kutwa na bweni ambapo wengine waliokuwa bwenini walifanikiwa kujiokoa.

Naye Sheihk wa Mkao wa Dar Es Salaam, Salum amesema kilichotokea ni mpango wa Mungu na kuwataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hichi kigumu.
1593858680580.png

Credit: ITV
 
Hatari sana hii habari.Wapumzike kwa Amani
 
Wapumzike kwa Amani Marehemu wote.
 
Back
Top Bottom