Dar es Salaam bado ni jiji la kimasikini saana! Ushahidi kwenye picha!

Dar es Salaam bado ni jiji la kimasikini saana! Ushahidi kwenye picha!

Sio lazima kujenga ghorofa,kuna njia kibao tajiri anaweza invest hela zake...au haujui Dar kuna maghorofa mengi hayana wapangaji?utaona tu mabango yameandikwa"TO LET 0780 448 899"Huoni haya magorofa ni white elephant project?nenda kwenye magorofa ya serikali yapo ya magorofa kibao hawaishi watu huo ni ujanja au ujing.a?
Bado unazidi kuthibitisha hoja yangu, mkuu.

Tajiri hawezi kujenga ghorofa halafu likapwaya kizembe hivyo. Hivi umeshawahi kujiuliza sababu za kuonekana kwa TO LET mara kwa mara?

Watu wanaachia hayo maghorofa kwa sababu yule tajiri-maskini alipojitutumua akalijenga (kwa mkopo, pesa za urithi, ufisadi au za kuazimwa), akaishia kuweka kodi isiyohimilika, akilenga kupata marejesho na utajiri wa chapuchapu.

Tajiri halisi anakadiria kodi himilivu kiasi kwamba siku zote 365 kwa mwaka, ghorofa linakuwa na wapangaji na biashara zinaendelea - hakuna gepu lolote la TO LET!

Kwa njia hiyo, hata ile kodi ndogo aliyoweka inafidiwa na uwepo wa wapangaji wakati wote - principle of continuous infinitesimal increment.

Hapo sijataja faida inayopatikana kwa eneo lake kuwa maarufu kwa sababu linajulikana vizuri wakati wote - na wafanyabiashara na wateja wao.

Sasa yule tajiri-maskini ambaye kighorofa chake anakodisha kwa madola kibao, anakaa hata zaidi ya mwaka shoroba zingine hazijawahi hta kuwapata wapangaji. Uwekezaji ni sanaa, siyo tu kuwa na vijisenti mfukoni!

Fanya feasibility study kuhusu manufaa ya jengo la ghorofa kwenye eneo fulani ambapo kodi yake ni himilivu na tumajengo twingine twa aftatu, utaona kuna tofauti kubwa kama kijito na bahari!
 
Hii picha imepigwa kutoka PSSSF tower floor ya 33. Angalia vijumba zaidi ya 99% viko chini! Hii inaonyesha kiwango cha juu cha umasikini na ustawi wa jiji la Dar es Salaam! Tunataka tuwe megacity yenye skyscrapers kama New York!View attachment 3168527
Hata marekani ukiacha yake maghorofa ya ofisi kule mjini,makazi mengi ni nyumba za chini
 
Zipo nchi ulaya hazina maghorofa marefu lakini majengo Yana structures nzuri na kupangiliwa safi, tunaweza kuwa na nyumba ambazo si maghorofa marefu lakini nzuri, siyo Kwa viboksi hivyo apo chini.
 
Mkuu umasikini haupimwi kwa kujaza magorofa mjini, neenda London uone kama kuna skyscraper kama zilioko Cairo au Dubai
Mkuu london unayoiona mara nyingi ni ile yenye historical iconic structures tu, ila london in skyscrapers za kufa mtu
 
Back
Top Bottom