Dar es Salaam bado ni jiji la kimasikini saana! Ushahidi kwenye picha!

Bado unazidi kuthibitisha hoja yangu, mkuu.

Tajiri hawezi kujenga ghorofa halafu likapwaya kizembe hivyo. Hivi umeshawahi kujiuliza sababu za kuonekana kwa TO LET mara kwa mara?

Watu wanaachia hayo maghorofa kwa sababu yule tajiri-maskini alipojitutumua akalijenga (kwa mkopo, pesa za urithi, ufisadi au za kuazimwa), akaishia kuweka kodi isiyohimilika, akilenga kupata marejesho na utajiri wa chapuchapu.

Tajiri halisi anakadiria kodi himilivu kiasi kwamba siku zote 365 kwa mwaka, ghorofa linakuwa na wapangaji na biashara zinaendelea - hakuna gepu lolote la TO LET!

Kwa njia hiyo, hata ile kodi ndogo aliyoweka inafidiwa na uwepo wa wapangaji wakati wote - principle of continuous infinitesimal increment.

Hapo sijataja faida inayopatikana kwa eneo lake kuwa maarufu kwa sababu linajulikana vizuri wakati wote - na wafanyabiashara na wateja wao.

Sasa yule tajiri-maskini ambaye kighorofa chake anakodisha kwa madola kibao, anakaa hata zaidi ya mwaka shoroba zingine hazijawahi hta kuwapata wapangaji. Uwekezaji ni sanaa, siyo tu kuwa na vijisenti mfukoni!

Fanya feasibility study kuhusu manufaa ya jengo la ghorofa kwenye eneo fulani ambapo kodi yake ni himilivu na tumajengo twingine twa aftatu, utaona kuna tofauti kubwa kama kijito na bahari!
 
Hata marekani ukiacha yake maghorofa ya ofisi kule mjini,makazi mengi ni nyumba za chini
 
Zipo nchi ulaya hazina maghorofa marefu lakini majengo Yana structures nzuri na kupangiliwa safi, tunaweza kuwa na nyumba ambazo si maghorofa marefu lakini nzuri, siyo Kwa viboksi hivyo apo chini.
 
Mkuu umasikini haupimwi kwa kujaza magorofa mjini, neenda London uone kama kuna skyscraper kama zilioko Cairo au Dubai
Mkuu london unayoiona mara nyingi ni ile yenye historical iconic structures tu, ila london in skyscrapers za kufa mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…