Dar es Salaam: Gharama za kujifungua ni Tshs 75,000. Uchaguzi huu unakupa nafasi ya kukataa uharamia huu

Kama umeona ghali si uende kwa bibi uzalie nyumbani? Ulitaka nani akulipie kwenye starehe zako? Hakuna cha bure hapa ulimwenguni, wewe kila siku umo humu ulitaka nani akulipie hizo MB? Wacha kelele!
 
Kadema bwana! kujifungua ni jambo la furaha...yaani miezi 9 yote najiandaa kupata mtoto nashindwaje kuweka hela kidogo kidogo hadi nifikishe hizo pesa? Ila pia hiyo ni gharama kwa wale wanaotaka kujifungua kwa huduma za "private" ...ndio kuna sehemu private kwenye hospitali za umma kwa wasiopenda bugudha!
 
Vya bure viliisha enzi ya Mwalimu JK Nyerere kwa sababu ya ujinga wa wengi, wao kila kitu wanataka bure wakati kodi hawataki kulipa. Hata nchi kubwa zilizoendelea kama UK huwezi kutibiwa kama wewe huna uraia wa hiyo nchi na wewe sio mlipa kodi/raia wa nchi hiyo. USA wameshindwa itakuwa Tanzania? Hatutaki watalii wagonjwa kufilisi manufaa ya walipa kodi wa Tanzania.
 

Ata Kama ni bure lakini sioni kosa lolote la kulipia huduma ya mama kujifungua kwa usalama zaidi kumbuka hao ndo wanaongoza kuchangiana hadi birthday za kila mtu na harusi za kila siku. Vitu vingine ni unafiki kulalamika bana akiona hiyo gharama ni kubwa basi ajifungulie nyumbani. Huduma za afya ni gharama dunia nzima. Watu tunapenda sana vya bure. Simchangui yoyote maana ata kadi ya mpiga kura sina. Kila la Heri kwa yeyote atakayeshinda
 
Hospitali ya Temeke ni hospitali ya rufaa. Gharama za matibabu pamoja na bei za dawa na huduma nyinginezo zimewekwa kwa bango na siyo kwa kificho. Kwa maneno mengine hauhitaji uwe na risiti kuthibitisha hizo gharama.
 
MKuu unalipa Kodi kweli wewe?
unajua kuw akuna mpaka ufadhili kw aajkili ya mama na mtoto, kutibiwa bure na kujifungua bure?
unajua kuna grants na loans jina la mama na mtoto?
Mkuu post zako sijaziona muda mrefu sana, karibu sana, happy to see you around.
 
Mbona serikali kujifungua hulipi kitu hata kwa operation Sana una lipia hela ya kitanda kwa siku elfu tano
 
Kwamba kuna sehemu za private kwenye hospital za uma?
Unaelewa unachoongea kweli? Umeambiwa mpk jina la hospital bado unakaza mishipa ya shingo.
Mimi naongezea Vijibweni hospital ya Kigamboni nayo wanatoza kawaida ni 40 na operation kuanzia laki moja.
Ukitaka ushahidi nenda.
 
Bro unabishana na wanafunzi? Watakutoa kibiomgo bure hao hata bando wanaomba kwa mama zao watajua wapi gharama za hospital.
 
Utakapofika tutumie risiti tuone, mimi ninavyojua hakuna malipo ndio maana nataka utupe uthibitisho hapa ili tuanzie hapo.
 
Kama umeona ghali si uende kwa bibi uzalie nyumbani? Ulitaka nani akulipie kwenye starehe zako? Hakuna cha bure hapa ulimwenguni, wewe kila siku umo humu ulitaka nani akulipie hizo MB? Wacha kelele!
Mkuu tunataka JPM atulipie , anahamasisha dada,mama,wadogo zetu wafyatue ,kwani kufyatua kwawingi nayonimaendeleo.
 
Mbona serikali kujifungua hulipi kitu hata kwa operation Sana una lipia hela ya kitanda kwa siku elfu tano
HOSPITAL YA KITETE MKOA WA TABORA UNALIPIA, ELFU 50 KAMA MZAZI AKIJIFUNGUA MTOTO WAKIUME, ELFU 40 KAMA MTOTO WAKIKE. SIJUI KAMA TOZO ZIPO KIHALALI LAKINI NILAZIMA KULIPIA
 
HOSPITAL YA KITETE MKOA WA TABORA UNALIPIA, ELFU 50 KAMA MZAZI AKIJIFUNGUA MTOTO WAKIUME, ELFU 40 KAMA MTOTO WAKIKE. SIJUI KAMA TOZO ZIPO KIHALALI LAKINI NILAZIMA KULIPIA
Labda hospital zinatofautiana aisee maana hyo hospital niliyoenda ni ya Rufaa, na ulikuwa hulipii kitu
 
Labda hospital zinatofautiana aisee maana hyo hospital niliyoenda ni ya Rufaa, na ulikuwa hulipii kitu
Hospital ya kitete niyarufaa pia, nasijui kwa nini wametofautisha gharama kwa mtoto wakike na kiume. Lakini lazima mzazi alipie baada yakujifungua .Na Mimi nashangaa kusikia hospital zingine hawalipii nilijua ndio utaratibu wa nchi nzima. Mpaka thread yake niliwahi ileta humu kuulizia kama nihalali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…