Dar es Salaam: Gharama za kujifungua ni Tshs 75,000. Uchaguzi huu unakupa nafasi ya kukataa uharamia huu

Dar es Salaam: Gharama za kujifungua ni Tshs 75,000. Uchaguzi huu unakupa nafasi ya kukataa uharamia huu

Huu ni uongo kabisa. Mwanafamila wangu amejifungulia kaloleni hospitali. Hatukulipa hata senti moja. Ilkua mwezi wa sita, na huduma ilikuwa Safi Sana, usafi wodini, huduma ya mama na mtoto imeimarishwa Sana Tanzania. Hakuna hizo garama kwenye hospitali ya serkali

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app

Ukiwa na bima hakuna tozo yoyote, muziki kwa kina sie tusio na bima mzeee!!! Si swala la ushabiki, hiyo ni kweli kabisa kuna tozo na bado hujatoa vifuta viatu la sivyo mgonjwa wako anadanja!!!
 
Mkuu Wacha kwahio JPM anatupiga saundi, kila mahala kuna tozo.
Unaweza kuniambia kitu cha bure hapa duniani? Usiniambie Oxygen, Jua, Mwezi, Usiku/Mchana. Vya bure hakuna isipokuwa vile tu alivyoweka Mwenyezi mungu. Angalia gharama za kumtunza mtoto hadi kufikia umri wa kujitegemea? Ukielewa hilo changanya na zako.
 
Mbona serikali kujifungua hulipi kitu hata kwa operation Sana una lipia hela ya kitanda kwa siku elfu tano
Cariha...
Mie wifi yako katoka huko leo kufanya dressing.
Hizo gharama kwa mie zilikuwa za vifaa tiba na madawa. Unanunua pharmacy kwao na risiti ya mashine kabisa unapewa. Japo baadhi zilikosekana nikanunua nje.
 
Acheni Mzee Apumzike Mtamuua Kwa Pressure
Sasa Katibu Mkuu Wa Wizara Hayupo
Aje Ajibu Hili

Mnapiga Counter Attack Nyingi Mpaka Beki Zimepoteana Halafu, Muda Mchache Watu Wana Hoja Tele
 
Sasa elfu 75 nayo hela ya kulalamika wakati unaenda kupata huduma ya kujifungua?

Unataka kuzaa tu bila kujua gharama za kuzaa?
.
Kama uanalalama 75 elfu ya kuzaa utaweza gharama za malezi kweli wewe?

Watanzania udhaifu wetu upo hapa! Hatupo tayari kujadili jambo linalofanywa na mamlaka isivyo sawa sababu ya ushabiki wa kichama\ linalojadiliwa lina maslahi na wewe!

Chief Mangungo!! Anadhihirisha uTanzania wetu!!
 
Sasa elfu 75 nayo hela ya kulalamika wakati unaenda kupata huduma ya kujifungua?

Unataka kuzaa tu bila kujua gharama za kuzaa?
.
Kama uanalalama 75 elfu ya kuzaa utaweza gharama za malezi kweli wewe?
We unazo, maana ndio miongoni mwa watu wachache mnaonufaika na utawala wa kimafia wa jiwe!!
 
We unazo, maana ndio miongoni mwa watu wachache mnaonufaika na utawala wa kimafia wa jiwe!!
Wewe subiria za Lisu atakuwekea mfukoni.

Yani mtu unalalama kuchangia gharama za 75 elfu kwa ajili ya kujifungua, utaweza gharama za kulea kweli wewe?
 
Kibena hospitali kujifungua ni bure ww na vifas vyako

Hiyo siyo Hospital ya Rufaa.hizo ghara za wamama wajawazitoni hosptali zote za mikoa.Ila ukienda Muhimbili hata kama ni referal ndiyo gharama zake utakimbia. Ile huduma bure kwa mama mjamzito ni huko kwenye vi hospital vya huko vichochoron
 
Hebu kuwa mkweli kwa nafsi yako!! Kati ya jiwe na Lisu nani kashikwa vibaya!!???
Sasa magu kashikwaje vibaya kama ni kampeni anafanya vizuri shazi mpaka pomoni,shida ni nyie chadema hamna hoja mnabaki kudandiadandia tuu.vile vitu ambavyo ilani yenu ya 2015 ndo anavifanyia kazi so mmebaki speechles na kutengeneza matukio tuu mara mjifanye mnaonewa na polisi nk.
 
Hospital ya kitete niyarufaa pia, nasijui kwa nini wametofautisha gharama kwa mtoto wakike na kiume. Lakini lazima mzazi alipie baada yakujifungua .Na Mimi nashangaa kusikia hospital zingine hawalipii nilijua ndio utaratibu wa nchi nzima. Mpaka thread yake niliwahi ileta humu kuulizia kama nihalali.
Ni bure Ila dawa unajinunulia mwenyewe na kulipia kitanda basi
 
Cariha...
Mie wifi yako katoka huko leo kufanya dressing.
Hizo gharama kwa mie zilikuwa za vifaa tiba na madawa. Unanunua pharmacy kwao na risiti ya mashine kabisa unapewa. Japo baadhi zilikosekana nikanunua nje.
Hongera kwenu kwa baby na mwambie mkeo awe anafanya mazoezi ya kutembea atapona haraka, na hzo Bei kwa serikali iko cheap private operation kuanzia milion hivi
 
Wajawazito wanaojifungulia kwenye Hospitali ya Rufaa ya Temeke , wale wanaojifungua kwa njia ya kawaida inawalazimu kulipia pesa taslimu ya kitanzania shilingi elfu 75 kama gharama ya kuzaa , Wale wanaojifungua kwa njia ya upasuaji wanapaswa kulipa zaidi ya Tsh laki 2 na yaweza hata kufika laki 2 unusu kutegemeana na complications .

Gharama hizi hazijumuishi gharama ya vifaa ambavyo mjamzito anapaswa kuingia navyo chumba cha uzazi ikiwemo pamba na gloves.

Kwahiyo basi uchaguzi huu unakupa nafasi ya kuchagua kuendelea kulipia gharama ya kuzaa au la , wale waliotuaminisha kwamba tuendelee kufyatua watoto kwa vile elimu ni bure ni vema wangeanzia kuondoa hii kodi ya kuzaa ili mambo yawe mepesi zaidi na kuwezesha wananchi kufyatua watoto kwa amani zaidi .
Tafuta daktari kabisa, maana unaweweseka Sana. Hapa tu bado 30 days uchaguzi ufanyike, matokeo yakitoka si utazirai kabisa.
 
Sasa 75,000 ina gharama gani wakati inakuletea mwana.
Mbona mnalala na wanawake mbaka kwa laki 1 na hamsini ili ukojoe tu.
Kwani tumebisha basi mkuu , tunatahadharisha tu wale mlioingizwa chaka kwamba mufyatue bila breki
 
Watu hawawazi hayo watu wako busy kwenda kwenye mikutano ya ccm kuangalia show za bure za muziki,Diamond na Ali kiba wanamuona live tena bure kabisa.

Hao ndio watanzania,unakuta mtu analalamika kuwa maisha yamekuwa magumu kwenye huu utawala wa jiwe ila bado ana mapenzi na ccm humwambii kitu.
 
Back
Top Bottom