Dar es Salaam hakuna sukari madukani

Dar es Salaam hakuna sukari madukani

unapokua kwenye gemu la kuongoza watu, matukio ya kukatika social services inaashiria nini kwako kama unajitathmini utendaji wako?? Just thinking out of the box....
 
Uzuri ni kwamba wananchi wameng'amua
Kuna sehemu dar, jana nimeshuhudia watu wanakimbizana saa saba usiku, ndio wanakwenda kununua huko mbagala kwa muuzaji wa jumla, na lazima uwe unajulikana ndio unauziwa, hatimaye leo tumeipata mtaani kwa 3500!!!!maisha yanakwenda japo kwa shida sanaaa!!!
 
Knockout!
EXpnjfXXQAAvh7f.jpg
 
Nimetafuta sukari maduka mengi ya nyumbani Tandika Mwembeyanga na Temeke mwisho sikufanikiwa kuipata, baadaye akaja kijana mmoja ninayefahamiana naye akaninong'oneza kwamba siwezi kupata sukari wiki hii, labda nisubiri upepo upite.

Baada ya uchunguzi wangu wa wazi nimebaini kwamba maduka karibu yote ya rejareja hayauzi tena sukari jijini Dar kutokana na mgogoro wa bei, taarifa zinaonyesha kwamba maduka ya jumla likiwemo la mfadhili wa CCM aitwaye Zakaria kilo moja ya sukari inauzwa kwa Tsh 2800 /= tena kwa masharti kwamba ni lazima ununue na vitu vingine, huku Muuzaji wa reja reja akitakiwa kuiuza kilo hiyo hiyo kwa Tsh 2600 /= kutokana na bei elekezi ya Serikali .

Wauzaji wa rejareja wameona isiwe tabu wameamua kuiachia serikali iuze yenyewe sukari kama inavyouza dawa kwenye maduka ya MSD
Kila kilicho mbele yenu mnakidandia na kuwa hoja ya kisiasa Sasa hoja ni sukari baada ya sugar ni nini kingine
 
Wapumbavu bado ni wengi Tanzania Hongera mpumbavu Ila ujue sio wote wanaweza kufanya hivyo. Mfikirie na mama ntilie nae. Hana uwezo wa kununua hata kilo 2.
Mimi sio mkulima wa miwa, mimi sina kiwanda cha sukari, mimi sio mfanyabiashara wa sukari, mimi sio bodi ya sukari, kiujumla mimi sihusiki na kupanga bei ya sukari kabisa. Mimi sijasababisha kuwepo kwa mamantilie nchini. Ukilielewa hilo na ukafikirisha akili yako kidogo kabla ya kutouch keyboard yako, nafikiri kidogo kidogo utajifunza Ustaarabu.
 
Back
Top Bottom