Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Hoja za wadau mabli mbali zimeanza kupata mashiko sasa, Bujibuji Simba Nyanaume tia neno hapa.
Huenda tukio limefanywa ili wawapange wamachinga. Maana huyu anauza mboga hapa, pembeni anauza mafuta ya taa, kulia anauza viatu.

Sasa wanataka wa mboga wakae kwao, viatu kwao. Pia wanataka pia kutengeneza barabara ili hata moto ukitokea, gari iweze kwenda hadi ndani kabisa kudhibiti majanga
 
Kimsingi hio ilikuwa ni mbinu ya kuwahamisha wamachinga mjini ili hayo maeneo wapewe wenye hela, kwahiyo mbinu nzuri ya kuwatoa bila shida bdo hiyo kuwachomea vitu vyao, kwakua moto utatafasirika kama janga la kijamii.

Ile issue ya Kariakoo mpaka Sasa serikali imekaa kimya, hâta hii tegemeeni hivyo. Huyu mama yenu haeshimiki.
 
Tuliolia kipindi cha mwendazake sasa ni wakati wa kucheka tu.

Tunataka mamalishe, machinga, wakulima & co wateseke kabisa maana ndiyo kubwa na hao ndiyo waliompa jeuri mwendazake.

Yako wapi sasa tuliwaambia wakashupaza shingo zao, acha sasa zivunjike.
Magufuli aliwatendea haki Watanzania walio wengi na waliofanya kazi halali. Ulitegemea wampinge alipowashughulikia mafisadi kama wewe?
 
Wanadeserve wanachokipata kwa kuwa wakati CCM inapora chaguzi walikenua meno.

Watulia hivyo hivyo sindano iingie vizuri hadi watakapopata akili ya kuikataa CCM na mambo yake yote.

Nashukuru sana Mungu kuwa leo wamepelekewa askari wa kikosi cha mbwa ambao wameenda kubomoa vile vibanda vyao ambavyo walikuwa wameshaanza kuvijenga jana.
kabisa yani, hapo utakuta wote ni ccm na hata wanaoonekana kulaumu wanatupia lawama kwa awamu hii na kusema ingeluwa awamu iliyopita haya yasingetokea

Yani kiufupi hawajaona tatizo la kuongozwa na ccm
 
Huenda tukio limefanywa ili wawapange wamachinga. Maana huyu anauza mboga hapa, pembeni anauza mafuta ya taa, kulia anauza viatu.

Sasa wanataka wa mboga wakae kwao, viatu kwao. Pia wanataka pia kutengeneza barabara ili hata moto ukitokea, gari iweze kwenda hadi ndani kabisa kudhibiti majanga
Unawapanga kwa kuwaunguzia Mali zao? Soko la karume ni la mitumba
 
Tuliolia kipindi cha mwendazake sasa ni wakati wa kucheka tu.

Tunataka mamalishe, machinga, wakulima & co wateseke kabisa maana ndiyo kubwa na hao ndiyo waliompa jeuri mwendazake.

Yako wapi sasa tuliwaambia wakashupaza shingo zao, acha sasa zivunjike.
Naona mabilionea mnakenua sasa, zamu ya mamalishe na machinga kukipata cha moto..dadeq!!
 
Wanadeserve wanachokipata kwa kuwa wakati CCM inapora chaguzi walikenua meno.

Watulia hivyo hivyo sindano iingie vizuri hadi watakapopata akili ya kuikataa CCM na mambo yake yote.

Nashukuru sana Mungu kuwa leo wamepelekewa askari wa kikosi cha mbwa ambao wameenda kubomoa vile vibanda vyao ambavyo walikuwa wameshaanza kuvijenga jana.
 
Katika suala la soko kuungua hakuna kitu kinanisikitisha Kama mtu mtaji wake wote aliweka hapo kupotea ,hapo Kuna watu hawana kitu mfukoni then familia inamtegemea,Kodi, mikopo etc...Tuwaangalia watu kwa jicho la ubinadamu.. huwezi kuelewa Hadi yakukute..
Amini kwamba msiba hauwi msiba mpaka ukukute, hapo hakuna hâta kiongozi mmoja anayeona wanayoyapitia hawa raia ndomaana hâta mabomu wamepigwa.
 
Machinga wameandamana kwa mkuu wa mkoa Amos Makalla kushinikiza waachiwe eneo lao waendelee na biashara zao. Lakini hawajafanikiwa na hivyo kuanza kupigwa mabomu ya machozi ili waondoke eneo hilo.
Poleni sana wamachinga wote wa Karume, sasa ni wazi hamna chenu hapo.
Ila binafsi nawaonea huruma sana, maana wamepoteza mitaji yao na eneo limeenda......!
Poleni sana

=======

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wa soko la Karume (Mchikichini) wameandamana hadi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kushinikiza kiongozi huyo atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo.

Machinga hao wameandamana leo Jumatatu Januari 17, 2022 ambapo walikuwa wanaimba "Tunataka Soko letu" wakiwa wamezingira geti la ofisi hiyo, ikiwa ni siku moja imepita tangu soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.

Mwananchi
View attachment 2084796
Piga hao wahuni kipigo cha mbwa koko. Wanataka kuichezea Dola??
 
kabisa yani, hapo utakuta wote ni ccm na hata wanaoonekana kulaumu wanatupia lawama kwa awamu hii na kusema ingeluwa awamu iliyopita haya yasingetokea

Yani kiufupi hawajaona tatizo la kuongozwa na ccm
Huenda CCM tumeichoka sana, lakini hakuna mbadala wake. Hatuna upinzani imara, ni kikundi tu cha wachumia tumbo wachache.
 
Back
Top Bottom